Alhamisi, 14 Desemba 2017

MWENYEKITI WA UVCCM MKOA WA IRINGA AANZA KUTEKELEZA AGIZO LA MWENYEKITI WA UVCCM TAIFA

Posted by Esta Malibiche on DEC 14,2017 IN SIASA

Mwenyekiti wa Uvccm Mkoa wa Iringa Kenani Kihongosi akikagua nyalaka mbalimbali katika chuo cha Mafunzo ya Itikadi Cha Uvccm,kilichopo eneo la Ihemi Mkoani Iringa.
MWENYEKITI wa jumuiya ya Vijana CCM mkoa wa Iringa Kenani Kihongosi amefanya ziara katika chuo cha Ihemi na kukuta changamoto mbalimbali zinazokikabili chuo hicho.

Katika ziara hiyo Mwenyekiti Kihingosi aliambatana na viongozi mbalimbali wa Uvccm akiwemo Katibu wa Uvccm Mkoa wa Iringa Jemsi Mgego pamoja na mjumbe wa baraza kuu la vijana Zawadi Abdalah.

Akizungumza na blog hii ya "KALI YA HABARI"mara baada ya kuhitimisha ziara hiyo alisema kuwa Lengo la ziara hiyo ilikuwa ni kukagua na kuanaglia changamoto mbalimbali zinazokikabili chuo hicho na kutekeleza wa agizo la Mwenyekiti wa Uvccm Taifa Kheri Jemsi alililolitoa jana kuwa kila Mwenyekiti wa Uvccm katika mkoa wake ahakikishe anahakiki mali zote za jumuiya ili kuweza kusaidia jumuiya hiyo kufanya kazi kwa ufanisi.

"Kwa pamoja tumekuja tumekuja kuangalia changamoto na tumebaini miundombinu ya umeme barabara na  majengo yaliyochoka ambayo yanahitaji kuboresha ili chuo kiweze kufanya kazi vizuri ukizingatia chuo hki ni hazina ya chama na kimetoa viongozi wengi wa serikali na chama chetu cha Mapinduzi." Alisema Kihongosi na kuongeza kuwa

"Wito wangu kwa viongozi wa Chama na Uvccm Taifa kuangalia kwa jicho la pekee kutusaidia maboresho ili chuo hiki kiendelee kupika viongozi wetu.Pia chuo hiki kinawapika vijana katika itikadi ya chama cha MapinduI pia kuna fursa nyingi za vijana kama ujasiliamali" Alisema Kihongosi na kuongeza kuwa

Kama walivyotuagiza na kutuamani kuwa tunaweza kusimamia na kukagua miundombinu hiyo,tumetekeleza agizo hilo hivyo basi tunaomba watusaidie namna gani wanaweza kusaidia kuhakikisha chuo hiki kimakuwa imara na hatimae kuwa hazina kubwa kwa vijana wa mkoa wa Iringa na Taifa kwa ujumla.

"Ndani ya uongozi wangu katika mkoa wa Iringa ninawaomba viongozi wenzangu watimize wajibu wao katika maeneo yao.Mwenyekiti ahakikishe anatekeleza agizo hili kwa kuhakiki mali za uvcvm zilipo katika wilaya yake.Pia watendaji wa jumuiya ambao ni makatibu wahakikidhe wanasimamia rasilimali zote za jumuiya na wadumishe umoja na mshikamano katika kutekeleza haya" Alisema Kihongosi na kuongeza kuwa

"Vilevile katika uongozi wangu sitaweza kumvumilia mtu yeyote atakaediriki kuvuruga umoja uliopo katika jumuiya hii."Alisema Kihongosi.

"Nikiwa Mwenyekiti wa umoja wa vijana wa mkoa wa Iringa ninawaasa na kuwaomba vijana wote wa mkoa wa Iringa kuwa wasiwepo watu wa kuwagawa wala watu wa kuipasua jumuiya hii,sitamvumilia mtu yeyote atakaeonyesha dalili au chembechembe yeote ya kuigawa jumuiya ya Umoja wa Vijana Mkoani Iringa,ninawaomba wote kwa pamoja tushirikiane kwa pamoja kumuunga mkono Mwenyekiti wa ccm Taifa Dkt.John Magufuli kuhakikisha Taifa hili linasonga mbele kimaendeleo,na maendeleo yataletwa na vijana waadilifu." Alisisitiza Kihongosi.





























0 maoni:

Chapisha Maoni