Jumatatu, 11 Desemba 2017

HERRY JAMES MWENYEKITI MPYA WA UVCCM, MAKAMU WAKE NI TABIA MAULID MWITA

Posted by Esta Malibiche on DEC 12,2017 IN SIASA

01
Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi  Rais Dkt Ali Mohamed Shein akimpongeza Mwenyekiti mpya wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana UVCCM Bw. Herry James mara baada ya kushinda katika uchaguzi wa jumuiya hiyo uliofanyika  kwa siku mbili katika ukumbi wa Chuo Cha Mipango mjini Dodoma wa pili kutoka kulia anayeangalia ni Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na kulia ni Makamu Mwenyekiti wa UVCCM Bi. Tabia Mwita.(PICHA NA JOHN BUKUKU-FULLSHANGWE-DODOMA

1
Mwenyekiti mpya wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana UVCCM Bw. Herry James na Makamu Mwenyekiti wa UVCCM Bi. Tabia Mwita wakipongezana mara baada ya kutangazwa washindi katika uchaguzi huo uliofanyika kwenye Chuo Cha Mipango mjini Dodoma.
02
Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi  Rais Dkt Ali Mohamed Shein akimpongeza Makamu Mwenyekiti wa UVCCM Bi. Tabia Mwita baada ya ushindi wake katikati anayeshuhudia ni Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
2
Mwenyekiti mpya wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana UVCCM Bw. Herry James na Makamu Mwenyekiti wa UVCCM Bi. Tabia Mwita wakifurahi kwa pamoja  mara baada ya kutangazwa washindi katika uchaguzi huo uliofanyika kwenye Chuo Cha Mpiango mjini Dodoma.
4
Makamu Mwenyekiti wa UVCCM aliyemaliza muda wake Mh. Mboni Mhita akimpongeza Makamu Mwenyekiti mpya Bi. Tabia Mwita.
6
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi CCM Mh. Kassim Majaliwa akionekana kufurahia wakati Makamu Mwenyekiti wa UVCCM aliyemaliza muda wake Mh. Mboni Mhita alipokuwa akimpongeza Mwenyekiti mpya wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana UVCCM Bw. Herry James.
8
Makamu Mwenyekiti wa UVCCM Taifa Bi. Tabia Mwita akihutubia kuwashukuru wajumbe wa mkutano mkuu huo wa 9 mara baada ya kumchagua katika uchaguzi huo.
9
Mbunge wa Bunge la Jamhuru ya Muungano ya Tanzania kupitia vijana Mh. Halima Bulembo akiwa pamoja na wajumbe wenzake katika mkutano huo.
10
Mwenyekiti mpya wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana UVCCM Bw. Herry James akihutubia mkutano huo na kuwashukuru wajumbe kwa kumchagua kwa kura nyingi kuwa kiongozi wa umoja huo kwa miaka mitano ijayo.
11
Makamu Mwenyekiti wa CCM na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mh. Dkt Ali Mohamed Shein akuhutubia wakati akifunga mkutano huo leo kwenye ukumbi wa Chuo cha Mipango mjini Dodoma.
12
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi CCM Mh. Kassim Majaliwa akiteta jambo na Mwenyekiti wa UVCCM Bw. Herry James kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa UVCCM Bw. Hamidu Shaka.
13
Baadhi ya wajumbe wa Halmashauri Kuu na Mkutano mkuu wa CCM wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kutangazwa washindi katika mkutano huo.
14
Picha mbalimbali zikiwaonyesha wajumbe  wakiwa katika mkutano huo.
1517
Mh. Mboni Mhita Makamu Mwenyekiti wa UVCCM aliyemaliza muda wake akizungumza na kuwashukuru wajumbe wote kwa ushirikiano waliompa wakati wote alipokuwa akishikilia Umakamu Mwenyekiti wa Umoja huo.
19
Msimamizi wa Uchaguzi huo Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Mh. William Lukuvi akitangaza matokeo ya uchaguzi huo katika uchaguzi wa UVCCM uliofanyika kwenye Chuo cha Mipango mjini Dodoma.
20
Picha mbalimbali zikionyesha wajumbe  wakifurahia mara baada ya matokeo hayo kutangazwa.
2122

0 maoni:

Chapisha Maoni