Jumamosi, 9 Desemba 2017

MAADHIMISHO YA MIAKA 56 YA UHURU WA TANZANIA BARA:RAIS MAGUFULI ASAMEHE WAFUNGWA 8157

Posted by Esta Malibiche on DEC 9,2017 IN NEWS

1
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiingia kwa gari maalum akiwa na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo wakati wa maadhimisho ya miaka 56 ya Uhuru wa Tanzania yaliyofanyika kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma ambako ndiyo makao makuu ya Nchi. maadhimisho hayo yamehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali ,Mabalozi wa wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini, viongozi wa vyama vya siasa, Viongozi wa dini pamoja na wananchi wa viunga vya mji wa Dodoma, Mh. Rais Dkt. John Pombe Magufuli pia amemsamehe Nguza Viking “Babu Seya” na Mwanaye  Johnson Nguza “Papii Kocha” waliokuwa wamefungwa Kifungo cha Maisha Gerezani.

22
Rais Dkt. John Pombe Magufuli amesamehe jumla ya wafungwa 8,157 katika maadhimisho ya miaka 56 ya Uhuru wa Tanzania Bara yaliyofanyika leo katika uwanja wa Jamhuri, Mjini Dodoma.
Msamaha huo umehusisha wafungwa 1828 ambao watatolewa kaunzia leo na wengine 6329 wamepunguziwa muda wa vifungo vyao, aidha kati ya wafungwa watakaoachiwa huru wafungwa 61 ni wafungwa ambao walihukumiwa kunyongwa.
“Kuna wafungwa ambao wamehukumiwa kunyongwa wana umri wa miaka 85 na wapo waliokaa gerezani zaidi miaka ya miaka 45, ambao wametubu na kukiri makosa na wapo ambao hawakuwauwa maalbino wala hawakuwa majambazi,” amesema Dkt. Magufuli.
Dkt. Magufuli ametoa mfano wa mfungwa anayejulikana kama Mganga Matonya mwenye umri wa miaka 85 yupo kwenye orodha ya wafungwa watakaoachiwa huru  leo ambapo amekaa gerezani kwa miaka 37 na mahabusu miaka saba (7)  kabla hajahukumiwa.
Katika hatua hiyo, Rais Dkt. Magufuli amewaachia huru Nguza Viking na  Johson Nguza (Papii Kocha) waliohukumiwa kifungo cha maisha.
Aidha Mhe. Rais amesema kuwa msamaha huo alioutoa leo umetokana na mamlaka aliyonayo kutoka kwenye Ibara ya 45 (a) (b) (c) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayomruhusu Mhe. Rais kutoa msamaha, kumuachia huru, kubadilisha adhabu au kufuta adhabu kwa mtu yoyote aliyehukumiwa kwa kosa lolote.
Wakati huo huo, Rais Magufuli ametoa wito kwa watanzania wote kuenzi na kudumisha tunu na amani zilizoachwa na waasisi wa Taifa.
Aidha, Rais Magufuli ameeleza kuwa tangu nchi ipate uhuru kumekuwa na maendeleo katika nyanza mbalimbali ikiwemo barabara, madaraja, vituo vya afya, shule za msingi na shule za sekondari.
“Wakati nchi inapata uhuru kulikuwa na jumla ya kilometa 32,600 za barabara ambapo kilometa 1360 zilikuwa katika kiwango cha lami, lakini mpaka sasa nchi inapotimiza miaka 56 ya uhuru kuna jumla ya kilometa 122,500 za barabara ambapo kati ya hizo kilometa 12,679.55 zipo katika kiwango cha lami, kilometa 2,480 zinaendelea kujengwa katika kiwango cha lami na kilometa 7087 zipo kwenye hatua mbalimbali za maandalizi za kujengwa katika kiwango cha lami” anasema Rais Magufuli.
Aidha, Rais Magufuli amesema kuwa, Mfalme wa Morroco amemtuma Spika wa nchi hiyo kuja kuangalia eneo litakalojengwa uwanja mkubwa wa Kimataifa Mkoa wa Dodoma ambapo unatarajiwa kuwekwa jiwe la msingi mwezi Machi au Aprili mwaka 2018.
Mbali na hayo Sherehe hizo zilipambwa na gwaride kutoka Majeshi ya Tanzania, onesho la kikundi cha Komando, onesho la gwaride la Uzalendo la wanafunzi, vikundi mbalimbali vya kwaya, ngoma za alisi na Tanzania Allstars.
2  4
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikagua gwaride huku akiongozwa  na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo wakati wa maadhimisho ya miaka 56 ya Uhuru wa Tanzania yaliyofanyika kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma
567
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akielekea jukwaa kuu mara baada ya kukagua gwaride huku akiongozwa  na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo wakati wa maadhimisho ya miaka 56 ya Uhuru wa Tanzania yaliyofanyika kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma
8
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mh.Jenista Mhagama Waziri Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu baada ya kukagua gwaride katika maadhimisho ya miaka 56 ya Uhuru wa Tanzania yaliyofanyika kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma
9
Picha mbalimbali zikionyesha Vikosi vya Ulinzi vikitoa heshima kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli Amiri jeshi mkuu wa majeshi ya Uinzi wakati wa maadhimisho ya miaka 56 ya uhuru kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma leo.
3
1011121314
Kikosi cha Makomandoo wa Jeshi la Ulinzi JWTZ kikipita kwa Gwaride la heshima mbele ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli.
1516
Baadhi ya wananchi mbalimbali waliohudhuria katika maadhimisho hayo wakiwa jukwaa kuu.
18
Makomandoo wakionyesha onyesho lao la kuokoa kiongozi aliyetekwa kwa kushuka na Helkopta ya kijeshi.
20
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia wakati wa maadhimisho hayo yaliyofanyika kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma.

0 maoni:

Chapisha Maoni