Posted by Esta Malibiche on DEC 2,2017 IN SIASA
Na Esta Malibiche
Iringa
UMOJA
wa vijana ccm mkoa wa Iringa umeandika historia mpya kumpata Mwenyekiti wa
jumuiya hiyo mara baada ya kukaa takribani miaka 4 bila Mwenyekiti wa Uvccm
mkoa.
Akitangaza
matokeo ya kura za Mwenyekiti wa Uvccm Mkoa katika mkutano mkuu wa 9,Msimamizi
mkuu wa uchaguzi Deogratius Ndejembi ,ambae pia ni Mkuu wa Wilaya ya Kongwa
Mkoani Dodoma,aliwasihi washindi wa umoja wa vijana ccm walioshinda katika
ngazi mbalimbali za jumuiya hiyo i kuwa
wazalendo kwa kutanguliza maslai ya chama na jumuiya ya vijana mbele pamoja
na kukipigania chama ili kiendelee kushika hatamu.
Ndejembi
alisema hakuna Taifa linalosonga mbele kimaendeleo pasipo kumtegemea
kijana,hivyo aliwataka kuweka maslai ya chama mbele na wasikubali kutumika na watu
kwa maslai yao binafsi hivyo kukivuruga chama na jumuiya ya Vijana.
"Kura
zilizopigwa ni 294,halali 193 iliyoharibika ni kura 1.Amoni..kapata kura
7,Jafari kikoti kapata kura 45 na Kenani Kihongosi kapata kura 235.Hivyo basi
kutokana na matokeo haya ninamtangaza Kenani Kihongosi kuwa ndiye Mwenyekiti wa
Uvccm Mkoa wa Iringa.Uchaguzi umeisha kikichobaki ni kumpa ushirikiano,tuwe na
sauti moja juu ya maslai mapana ya jumuiya na chama"" Alisema
Ndejembi.
Kwa
upande wa Msimamizi msaidizi ambae pia ni Mkuu wa wilaya ya Kilolo Asia Abdalah
aliwataka wawe viongozi wenye kuleta mabadiliko katika jumuiya,kujiepusha na
makundi ambayo yanaweza kuwagawa vijana.
‘Msikubali
kubezwa na vyama vya upinzani,tembeeni kifua mbele kwa kufanya kazi kwa bidii
ili kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Mwenyekiti wetu wa ccm Taifa Rais
Magufuli’’Alisema Asiah na kuongeza kuwa
‘’Uongozi wa jumuiya ya
vijana siyo ajira bali ni uzalendovijana moja wa vijana wa chama cha
mapinduzi (UVCCM) mkoa wa Iringa umempata mwenyekiti mpya bwana Kenani
Kihongosi alichaguliwa kwa kura nyingi za kishindo na kurudisha matumaini mapya
ya kuanza safari ya kuijenga CCM mpya kwa vijana wa mkoa huu wa Iringa’’Alisema
Asia
Nae
katibu wa jumuiya ya umoja wa vijana ccm mkoa wa Iringa,Jemsi Mgego akitoa
pongezi kwa washindi walioshinda katika ngazi mbalimbali za uongozi wa umoja
huo alisema kazi kubwa ya uvccm ni kuwapika vijana kwa imani na itikadi
ya ccm,na kwa mtu yeyote atakae hubiri utengano na kuleta mpasuko ndani ya
umoja wa vijana wa ccm basi hastahili kuwa kiongozi na kuwa mwanaccm.
""Huu
sasa ni wakati wakujenga jumuiya imara na madhubuti ikiwa nipamoja na
kuvujna makundi ya uchaguzi na kuwa kitu kimoja ili kuiletea
hedhima jumuiya hii iliyopotoea kwa miaka minne bila juwa na Mwenyekiti
wa uvccm mkoa wa Iringa"" Alisema Mgego na kuingeza kuwa
""Mbele
yetu tuna kazi kubwa ya kulikomboa jimbo la Iringa mjini,tukishirikiana kwa
pamoja kama tulivyoshirikiana katika uchaguzi mdogo wa udiwani kata ya kitwiru
hakika tutafanikiwa na hatimae jimbo kurudi katika mikono ya chama cha
Mapinduzi"" Alisema Mgego
Akiwashukuru
kwa kumchagua kuwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya umoja wa Vijana ccm MKOA WA
Iringa,Kenani Kihongosi alisema kuwa atahakikisha jumuiya zote za umoja wa
vijana wa chama cha mapinduzi zinarudi na kufanya kazi kwa ushirikiano mkubwa
na kuhakikisha wanapata wanachama wapya ambao itakuja kuwa nguzo ya chama hicho
hapo baadae.
“Ninawashukuru
wajumbe kwa kuniona kuwa ninafaa,ni miaka mine tumekaa kwa unyonge bila kuwa na
Mwenyekiti,ninawaomba tushirikiane kwa pamoja katika kufanya kazi na
kuhakikisha kila kitu kinaenda kama kilivyokusubiwa na kuhakikisha chama
kinapata matokeo chanya kutoka kwetu vijana hivyo naomba mniunge mkono
kuhikikisha tunakuwa wamoja” alisema Kihongosi
Kihongosi
aliwataka vijana kufanya kazi na kuhakikisha wanaendelea kumuunga mkono Rais wa
jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr John Pombe Magufuli kwa kazi kubwa anayoifanya
ya kuijenga CCM na Tanzania mpya.
“Sisi
ndio vijana ambao tunatakiwa kuonyesha mfano kwa kufanya kazi na kuonyesha
wapinzani wa mkoa wa Iringa kuwa sasa kuna UVCCM ambavyo inania ya kuhaikisha
inaumaliza upinzani uliopo hapa mkoana na CCM ikachukua jimbo la Iringa Mjini”
alisema Kihongosi
0 maoni:
Chapisha Maoni