Jumamosi, 9 Desemba 2017

Uzinduzi wa Kitabu cha Kampeni na Utaifa Dodoma.

Posted by Esta Malibiche on DEC 9,2017 IN NEWS

DSC_6811
WANANCHI wakiwa katika ukumbi wa Chuo Kikuu cha Dodoma wakifuatilia uzinduzi wa katika cha Kampeni ya Uzalendo na Utaifa katika  Utaifa ukumbi huo na kuzinduliwa na Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.
DSC_6852
MSANII Patrisha Hilal akiwa na wasanii wezake jukwaani akiimba moja ya nyimbo yake iliokuwa ikizungumzia uzalendo, wakati wa uzinduzi wa Kitabu cha Kampeni ya  Uzalendo na Utaifa  Kwanza katika ukumbi wa Chuo Kikuu cha Dodoma kushoto Saidi Mabera, Mzee Makasi, Mzee Hiza,Cosmas Chidumule, Zahir Zoro na Hamza Kalala. Wakati wao walitumia usania kuzungumzia uzalendo kupitia nyimbo zao.
DSC_6865
BAADHI ya Viongozi na Wananchi waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa Kitabu cha Kampeni ya Uzalendo Utaifa Kwanza wakifuatilia hafla hiyo wakati,  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akihutubia hafla hiyo katika ukumbi wa Chuo Kikuu cha Dodoma.
DSC_6900
WAZIRI Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akihutubia wakati wa hafla ya Uzinduzi wa Kitabu cha Kampeni ya Uzalendo na Utaifa Kwanza katika ukumbi wa Chuo Kikuu cha Dodoma
DSC_6908
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akihutubia katika hafla ya Uzinduzi wa Kitabu cha Kampeni na Utaifa Uzalendo Kwanza kilichozinduliwa katika ukumbi wa Chuo Kikuu cha Dodoma na Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan
DSC_6947
BAADHI ya Viongozi na Wananchi waliohudhulia hafla ya Uzinduzi wa Kitabu cha Kampeni Uzalendo  na Utaifa  wakituatilia hafla hiyo iliofanyika katika Ukumbi wa Chuo Kikuu cha Dodoma
DSC_6982
MAKAMU wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan akizundua Kitabu cha Kampeni  Uzalendo na Utaifa  Kwanza katika ukumbi wa Chuo Kikuu cha Dodoma wakishuhudia uzinduzi huo Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa na Waziri wa Habari Utamaduni na Michezo Dkt. Herrison Mwakyembe, uzinduzi huo umefanyika katika ukumbi wa Chuo Kikuu cha Dodoma.
DSC_7010
MAKAMU wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan akionesha picha ya Kitabu cha Kampeni Uzalendo na Utaifa Kwanza baada ya kukizundua katika Ukumbi wa Chuo Kikuu cha Dodoma, akiwa na Waziri wa Habari Utamaduni na Michezo Dk Herrison Mwakyembe, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, na Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassima Majaliwa
DSC_7030
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akikabidhiwa nakala ya Kitabu cha Kampeni  Uzalendo na Utaifa Kwanza na Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan, baada ya kukizindua kitabu hicho katika ukumbi wa Chuo Kikuu cha Dodoma.
DSC_7048
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akisoma kitabu cha Uzalendo Kwanza baada ya kuzinduliwa na kukabidhiwa nakala ya kitabu hicho katika ukumbi wa Chuo Kikuu cha Dodoma akiwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.
Picha na Ikulu

0 maoni:

Chapisha Maoni