Posted by Esta Malibiche on DEC 28,2017 IN NEWS
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,TAMISEMI Mhe.Selemani Jafo akikagua ujenzi wa majengo mbalimbali wilaya ya Ikungi
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,TAMISEMI Mhe.Selemani Jafo(Mbele kulia) akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe. Miraji Mtaturu akifuatiwa na Mbunge wa Singida Magharibi Mhe. Elibariki Kingu wakati wa ukaguzi wa ujenzi wa miundombinu ya wilaya hiyo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,TAMISEMI Mhe.Selemani Jafo(Mbele kulia) akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe. Miraji Mtaturu akifuatiwa na Mbunge wa Singida Magharibi Mhe. Elibariki Kingu wakati wa ukaguzi wa ujenzi wa miundombinu ya wilaya hiyo.
................................................................................
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Selemani Jafo ameushukia Wakala wa Majengo nchini ( TBA) kutokana na kusuasua katika ujenzi wa miradi mbalimbali ya serikali waliyopewa na Tawala za Mikoa na Mamlaka za serikali za Mitaa(Tamisemi).
Jafo ameonyesha kutoridhishwa na utendaji kazi wa TBA alipotembelea miradi mbalimbali ya maendeleo wilayani Ikungi mkoani Singida.
Katika ziara yake, Jafo ametembelea ujenzi wa makazi ya viongozi wa wilaya wa Ikungi ambapo muda uliopangwa kukamilisha kazi hiyo umeshapita huku kazi bado haijakamilika ambazo zinagharimu kiasi cha Sh.Milioni 700.
Kufuatia hali hiyo, Jafo ametoa miezi miwili kwa TBA kukamilisha ujenzi wa nyumba nne kwa ajili ya mkuu wilaya ya Ikungi mkoani Singida, Katibu tawala wa wilaya pamoja na watumishi wengine wa wawili ambazo zilitakiwa kukamilika tangu mwezi Septemba mwaka huu.
Jafo amesema mbali na nyumba hizo za Ikungi kuna nyumba nyingine katika wilaya ya Nkarama na wilaya mbalimbali hapa nchini ambazo zote ujenzi wake unasuasua sana licha ya Ofisi za Makatibu Tawala wa mikoa kufanya malipo ya ujenzi wa majengo hayo TBA, pia
baadhi ya shule kongwe zinazo karabatiwa na TBA kasi ya utekelezaji ni ndogo.
“TBA mmekuwa na matatizo katika maeneo mengi sana kama hamuwezi mtuambie muendelea na kazi mnazopewa na serikali kuu sisi huku serikali za mitaa mtuache tuwape watu wengine wapo watu wanajengaa vizuri na kwa wakati kuliko nyinyi tutawapa hata Suma JKT ambao pia wanao tu katika kazi kama hizi “amesema Jafo.
Jafo ameitaka TBA kuyakamilisha majengo hayo haraka kabla ya mwezi Februari mwaka 2018 kwani viongozi wa wilaya wanateseka kwa kukosa makazi na Ofisi na pia ujenzi wa shule Kongwe walizopewa watoto wanakosa miundombinu bora.
Kwa upande wake, Mkuu wa wilaya hiyo Miraji Mtaturu, amesema kutokana na jengo la ofisi ya mkuu wa wilaya kutokamilika anatumia jengo ambalo lilikuwa darasa.
0 maoni:
Chapisha Maoni