Posted by Esta Malibiche on JAN 5,2017 IN NEWS
Naibu waziri wa Nishati ya Umeme,Subira Mgalu amewahikikishia wananchi wa ya Kiwangwa jimbo la Chalinze Mkoani Pwani kuwa mipango ya kupeleka nishati ya umeme katika vijijini vilivypo ndani ya kata hiyo imeanza kufanyiwa kazi.
Kauli hiyo ameitoa wakati akizungumza na wananchi wa kata ya Kiwangwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze Mkoani Pwani ikiwa ni moja ya ziara yake aliyoifanya hivi karibuni.
Katika ziara hiyo ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze, alitembelea Kata ya Talawanda, Kiwangwa,Kibindu na Mkange kujionea shughuli mbalimbali za Jamii ambazo zinahitaji umeme.
Akiwa Kata ya Talawanda alitembelea Kituo cha Afya cha Magulumatari, Talawanda na Kisanga ambapo yeye na Mheshimiwa Mbunge walichangia Mifuko ya Cement.
Naibu Waziri aliwaambiwa wananchi wa kata hiyo haswa katika vitongoji kuwa hakuna kitongoji kitakachoachwa kupatiwa umeme hasa maeneo yenye mahitaji maalum kama Hospitali, shuleni na kwenye shughuli za Kijamii kama Ofisi za kuhudumia wananchi
Mgalu akiwa kata ya Kiwangwa,alifafanua juu ya Mabadiliko ya Bei kufuatia taarifa kuwa bei zimebadilika toka Elfu 27 hadi Shilingi 180,000,alisema kuwa hakuna mabadiliko katika Bei.
Awali Mbunge wa Jimbo la Chalinze kupitia Chama cha Mapinduzi CCM,Ridhiwani Kikwete,akimkaribisha Naibu Waziri wa Nishati Kuzungumza na Wananchi wa kata hiyo kuhusu Mipango ya Kupeleka Nishati ya Umeme Vijijini,alimsihi Naibu Waziri kutatua kero hiyo kwa haraka ili wananchi waweze kunufaika na Nishati ya Umeme.
Ridhiwani alisema endapo kata hiyo itapatiwa umeme vijana watajipatia Ajira kutokana na nishati hiyo,hivyo kupunguza wimbi la vijana waasio na Ajira ndani ya jimbo hilo la Chalinze.
Katika Kata ya Kibindu , alitembelea mradi wa Umeme wa Jua ambao zaidi ya Kaya zisizopungua 280,zitanufaika na Umeme huu na kupunguza kero ya iliyodumu kwa mua mrefu ya ukosefu wa umeme katika kata hiyo.
“Hii ni hatua kubwa ambayo Mbunge amewezesha kuhakikisha wananchi wetu wanafaidika na nishati hii, nakupongeza sana Mheshimiwa Mbunge.” Aisema Mgalu
Naibu Waziri wa Nishati Subira Mgalu akizungumza na wanannchi wa kata ya Kiwangwa.
Mbunge wa Jimbo la Chalinze kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Ridhiwani Kikwete akizungumza na wananchi wa kata ya Kiwangwa. |
Wananchi wa kata ya Kiwangwa wakimsikiliza mbunge wao kwa makini,Ridhiwani Kikwete. |
Naibu waziri wa Nishati Subira Mgalu akipokea Maoni kutoka kwa Wananchi wa kata hiyo.
0 maoni:
Chapisha Maoni