Jumamosi, 9 Desemba 2017

*RC MAKONDA ATOA RUNINGA 69 KWA MAGEREZA NA HOSPITAL ZA DAR, AJUMUIKA NA WAFUNGWA KWENYE CHAKULA CHA PAMOJA*

Posted by Esta Malibiche on DEC 9,2017 IN NEWS



Mkoa wa Dar es Salaam umeadhimisha miaka 56 y a Uhuru wa Tanzania bara kwa   Kuwatembelea Wafungwa na Maabusu kisha kupata Chakula cha Pamoja na kutoa huduma ya  Masaada wa Kisheria na Ushauri na Saha kwa Wafungwa na Mahabusu.

Katika Maadhimisho hayo Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam  Mhe. PAUL MAKONDA ametoa Msaada wa  Runinga za Kisasa 69   (Flat Screen)  Touch zenye ukubwa wa Inch 40 kwa Magereza na Hospital zote za Dar es Salaam  kuwezesha Wafungwa na Wagonjwa kupata haki ya kikatiba ya kupata Habari. 

*Hii ni Historia kwa Dar es salaam kuwa Mkoa wa kipekee wenye Runinga Magerezani* zinazowawezesha Wafungwa na Mahabusu kupata *Habari na Hotuba za Rais* ili kuwapunguzia *Msongo wa Mawazo* ili wasiwe na Mawazo ya kujiua ambapo zitagawanywa kwenye Magereza ya *Segerea, Keko na Ukonga*.  

*RC MAKONDA* aliongozana na *Viongozi wa Dini* waliowafariji Wafungwa na Kuwafanyia *Sala na Dua* huku Watu wa *Ustawi wa Jamii* wakitoa Msaada wa *Ushau na Saha* kwa Wafungwa. 

*MAKONDA* ambae *amepokelewa kwa Furaha kubwa*na Wafungwa wa Gereza hilo amewasihi *kutokata Tamaa* kwakuwa bado wanayo nafasi ya *kutimiza ndoto zao baada ya kumaliza kifungo* ambapo amewahimiza kuwa *Mabalozi Wazuri kwa Jamii.* 

Ili kupunguza msongamano wa Mahabusu Gerezani *RC MAKONDA* amesaidia zaidi ya Mahabusu na Wafungwa *200* wa Gereza la Segerea kupata  *Msaada wa Sheria* ambao walikuwa hawana uwezo kifedha.

Aidha *MAKONDA* ametoa *Magodoro 100, Vifaa vya Usafi na Sabuni za Kuoga na Kufua* kwa Wafungwa na Mahabusu.

Baadhi ya Maabusu na Wafungwa wamemshukuru *RC MAKONDA* kwa kuwa *kiongozi wa Kwanza na wa pekee* aliewatembelea na *kupata chakula cha pamoja, kuwapatia Runinga, kusikiliza changamoto zao na kuwapatia Wanasheria na watu wa Ustawi wa Jamii* kitendo kilichowafariji. 

Aidha Wameshukuru pia kitendo cha *RC MAKONDA* kusikiliza Changamoto zao na kuzipatia majibu ambapo *wamemuahidi kuwa wamebadilika na watakuwa mabalozi wazuri kuhimiza jamii kuzingatia Sheria.*

0 maoni:

Chapisha Maoni