Posted by Esta Malibiche on DEC 29,2917 IN NEWS
Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mh Anthony Mavunde amewahakikishia wafanyabiashara wadogo wadogo wa stendi ya mabasi ya vijijini katika eneo la Kikuyu Kusini juu ya ujenzi wa soko kwa ajili ya matunda na mboga mboga na kuondokana na adha ya kufanya biashara katika maeneo ambayo siyo rasmi.
Mavunde ameyasema hayo wakati akijibu kero za wafanyabiashara hao alipotembelea stendi ya mabasi hiyo eneo la Kikuyu Kusini na kuwahakikishia wafanyabiashara hao juu ya ujenzi na ukamilishaji wa soko ambalo litagharimu kiasi cha Shilioni Milioni Tisini na Mbili(*92,000,000*)
Aidha katika Mkutano wa hadhara wa wananchi Kikuyu Kusini,Mh Mavunde amewataka wananchi kushirikiana na viongozi wao katika ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule ya Msingi Kikuyu B ambapo Mbunge huyo ameahidi kuwachangia matofali 500 na mifuko ya saruji 50.
Wananchi wa Kata ya Kikuyu Kusini wamempongeza Mbunge Mavunde kwa jitihada kubwa anazofanya za kuwaletea maendeleo na kumuahidi kumpa ushirikiano katika uongozi wake.
Ijumaa, 29 Desemba 2017
MAVUNDE AWAHAKIKISHIA WAFANYABIASHARA WADOGO WADOGO SOKO LA MBOGA MBOGA KIKUYU KUSINI -DODOMA*
09:57
No comments
0 maoni:
Chapisha Maoni