Jumatano, 13 Desemba 2017

WAZIRI MWIGULU AMALIZA MGOGORO WA ARDHI ULIODUMU KWA MIAKA TISA KONDOA ARUDISHA AMANI KWENYE KATA*

Posted by Esta Malibiche on DEC 13,2017  IN  NEWS

 Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi Dr Mwigulu Nchemba amefanikiwa kumaliza mgogoro wa ardhi ambao umedumu kwa miaka zaidi ya tisa ambao ulifikia hadi kuhatarisha amani ya kijiji cha Hurui katika kata kikole jimbo la kondoa vijijini wilaya ya kondoa mkoa wa Dodoma

Mgogoro huo ambao umesababishwa na baadhi ya watu ambao si wajumbe wa kijiji kuuza eneo la kijiji la malisho mwaka 2009 bila mkutano wa kijiji kushirikishwa na kusababisha hali ya sitofahamu mpaka leo. Jitihada za wananchi kutafuta haki ya eneo hilo kwa njia za kisheria hazikuzaa matunda kwani walishindwa katika kesi zote mbili walizofungua katika mhakama ya ardhi ya wilaya na mkoa hali iliyopelekea sasa mbunge wa jimbo la kondoa vijijini Dr Ashatu Kijaji kumwita waziri wa mambo ya ndani kusaidia kutuliza taharuki hiyo.

Waziri Dr Mwigulu Nchemba baada ya kusikiliza pande zote za kijiji na serikali ya wilaya ameagiza eneo hilo liendelee kutumika kama lilivyopangwa tangu mwaka 1972 kuwa eneo la malisho, amewataka wananchi na viongozi wa vijiji waache kuuza maeneo kinyemela kwani ndio chanzo kikubwa cha migogoro ya ardhi

Wananchi wa kata ya kikole wamemshukuru waziri wa mambo ya Ndani  ya nchi  kwa kuwarudishia maeneo yao kwani kwasasa amani itarudi tena katika kata yao na maendeleo yatakuja  kwani watafanya shughuli kwa amani.










0 maoni:

Chapisha Maoni