Posted by Esta Malibiche on Dec 28,2017
Naibu Waziri wa Nchi-Ofisi ya Waziri Mkuu( Kazi,Vijana na Ajira) Mh Anthony Mavunde amewataka Vijana ambao wanashiriki katika mafunzo ya Ulinzi shirikishi kupitia Polisi Jamii kuunda vikundi vya uzalishaji mali ili kujikwamua kiuchumi na kuongeza kipato.
Mavunde ameyasema hayo leo wakati akifunga mafunzo ya Ulinzi shirikishi yaliyoshirikisha Vijana 75 katika kata ya Mtumba,Manispaa ya Dodoma.
“Pamoja na jukumu kubwa mlilonalo na ulinzi na usalama wa raia na mali zao,lakini pia mhakikishe mnatumia mkusanyiko wenu kuunda vikundi vya uzalishaji mali ili kujiongezea kipato na kutengeneza nafasi za Ajira zaidi”
Mavunde amewataka vijana hao kuyatumia vyema mafunzo waliyopata kwa kuwa waadlifu,waaminifu na wazalendo kwa Taifa lao na kusimama mstari wa mbele kuhakikisha Taifa hili linaendelea kuwa na AMANI na UTULIVU.
Naye Kamanda wa Mkoa wa Polisi wa Dodoma,SACP Muroto amewataka Vijana zaidi kujitokeza katika Ulinzi shirikishi ili kuimarisha usalama na amani katika mkoa wa Dodoma.
Alhamisi, 28 Desemba 2017
MAVUNDE AWATAKA POLISI JAMII KUUNDA VIKUNDI VYA UZALISHAJI MALI KUJIKWAMUA KIUCHUMI
19:45
No comments
0 maoni:
Chapisha Maoni