Kwa Habari za kitaifa na kimataifa

Tembelea Kali ya habari

Kwa habari za michezo na burudani

Tembelea Kali ya habari

Kwa habari za afya

Tembelea Kali ya habari

Kwa habari za Kilimo

Tembelea Kali ya habari

Kwa habari za uchumi na biashara

Tembelea Kali ya habari

Kwa habari za elimu

Tembelea Kali ya habari

Jumamosi, 30 Desemba 2017

MKUU WA WILAYA YA NACHINGWEA RUKIA MUWANGO AWATAKA WANANCHI KUZITUMIA FEDHA ZA KOROSHO KWA UANGALIFU

Poated by Esta Malibiche on DEC 30. 2017 IN NEWS
Mkuu wa wilaya ya Nachingwea mkoani Lindi Mh.Rukia Muwango akizungumza na wananchi wa kijiji cha Ruponda mapema leo hii katika zoezi la usafi wa Mazingira 
 MKUU wa Wilaya ya Nachingwea Mkoani Lindi Rukia Muwango amewataka wananchi kuwa makini na matumizi ya fedha za korosho ili ziweze kuwasaidia katika kuboresha maisha yao pamoja na kusomesha watoto.

Kauli hiyo ameitoa mapema leo hii Katika kijiji cha Ruponda mara baada ya   zoezi la usafi  wa Mazingira lililofanyika katika kijiji hicho,  alipoungana na wananchi kusafisha Mazingira ikiwa ni  ni moja ya utekerezaji wa Agizo la Mh.Rais Dkt.John Magufuli kuwa kila Mwisho wa Mwezi iwe ni siku ya usafi wa Mazingira kote Nchini.

Akizungumza na wananchi hao Muwango alisema kuw, matumizi ya fedha hizo yalenge katika kuleta mabadiriko ndani ya familia na kuwaletea maendeleo na si vinginevyo.
"Hakikisheni fedha mnazozipata kutokana na korosho mnazitumia vizuri ikiwa nipamoja na kujiretea maendeleo kwa kujenga nyumba,kujenga vyoo bora,kuwapeleka watoto shule  huku mkiwa na akiba kwa ajili ya  k Maendeleo"" Alisema Muwango na kuongeza kuwa
"" Kila Mwananchi anatakiwa awe na uchungu na fedha za korosho kutokana na maumivu mnayoyapata  kutokana na zao hili,mnapoteza muda mwingi na fedha kununulia  dawa  za kupulizia,hivyo mnapaswa kuwa na uchungu   na fedha  mnazozipata m zitumieni kwa uangalifu na umakini mkubwa""Alisema Muwango.

Aidha aliwataka wazazi kuhakikisha wanawaandikisha watoto shule wale wote waliofikia umri wa kuanza masomo ya shule ya Msingi.Pia kwa wale waliofauhuru na kujiunga na kidato cha kwanza mwaka 2018 wahakikishe wanaenda shule,na mazazi atakaezembea hatua za kinidhamu zitachukuliwa dhidi yao.
"Sitamvumilia Mzazi,Mlezi aunmtu yeyote yule atakaebainika kutompeleka mtoto shule,nitamchukulia hatua kali,hivyo ninawaomba tuwapekeke watoto shule mara tu zitakapofunguliwa.

Akizungumzia kuhusu kilimo aliwataka kuzitumia mvua zinazoendelea kunyesha kupanda mazao ya muda mfupi,ili waweze kupata chakula cha kutosha hivyo kuondokana na adha ya njaa.Pia aliwasihi kukitumia vizuri  na kwa uangalifu chakula kilichopo ili waweze kuondokana na adha ya njaa.

"Nawaomba twende shambani kulima,tusikae vijiweni na majumbani wakati wa msimu huu wa kilimo, tuzitumie hizi mvua zinaoendelea kunyesha kwa kilimo,  tupande mbegu za  bira kwa kuzingatia  Elimu tuliyoipata kutoka kwa wataalamu wetu wa kilimo 
ili tuoate chakula cha kutosha na hatimae kuondokana na baa la njaa kwa wilaya yetu.


 Mkuu wa wilaya ya Nachingwea mkoani Lindi Mh.Rukia Muwango akizungumza na wananchi wa kijiji cha Ruponda mapema leo hii katika zoezi la usafi wa Mazingira 

 Wananchi wa kijiji cha Ruponda wilayani Nachingwea waliojitokeza kushihiriki katika  zoezi la usafi wa Mazingira leo hii wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya hiyoRukia Muwango.  
Wananchi wa kijiji cha Ruponda wilayani Nachingwea waliojitokeza kushihiriki katika  zoezi la usafi wa Mazingira leo hii wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya hiyoRukia Muwango. 
Wananchi wa kijiji cha Ruponda wilayani Nachingwea waliojitokeza kushihiriki katika  zoezi la usafi wa Mazingira leo hii wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya hiyoRukia Muwango. 
Wananchi wa kijiji cha Ruponda wilayani Nachingwea waliojitokeza kushihiriki katika  zoezi la usafi wa Mazingira leo hii wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya hiyoRukia Muwango. 
Wananchi wa kijiji cha Ruponda wilayani Nachingwea waliojitokeza kushihiriki katika  zoezi la usafi wa Mazingira leo hii wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya hiyoRukia Muwango. 
Wananchi wa kijiji cha Ruponda wilayani Nachingwea waliojitokeza kushihiriki katika  zoezi la usafi wa Mazingira leo hii wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya hiyoRukia Muwango. 
Wananchi wa kijiji cha Ruponda wilayani Nachingwea waliojitokeza kushihiriki katika  zoezi la usafi wa Mazingira leo hii wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya hiyoRukia Muwango. 

Wananchi wa kijiji cha Ruponda wilayani Nachingwea waliojitokeza kushihiriki katika  zoezi la usafi wa Mazingira leo hii wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya hiyoRukia Muwango. 
Wananchi wa kijiji cha Ruponda wilayani Nachingwea waliojitokeza kushihiriki katika  zoezi la usafi wa Mazingira leo hii wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya hiyoRukia Muwango. 
Wananchi wa kijiji cha Ruponda wilayani Nachingwea waliojitokeza kushihiriki katika  zoezi la usafi wa Mazingira leo hii wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya hiyoRukia Muwango. 
Wananchi wa kijiji cha Ruponda wilayani Nachingwea waliojitokeza kushihiriki katika  zoezi la usafi wa Mazingira leo hii wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya hiyoRukia Muwango. 

Wananchi wa kijiji cha Ruponda wilayani Nachingwea waliojitokeza kushihiriki katika  zoezi la usafi wa Mazingira leo hii wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya hiyoRukia Muwango. 













Ijumaa, 29 Desemba 2017

MAVUNDE AWAHAKIKISHIA WAFANYABIASHARA WADOGO WADOGO SOKO LA MBOGA MBOGA KIKUYU KUSINI -DODOMA*

Posted by Esta Malibiche on DEC 29,2917 IN NEWS


Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mh Anthony Mavunde amewahakikishia wafanyabiashara wadogo wadogo wa stendi ya mabasi ya vijijini katika eneo la Kikuyu Kusini juu ya ujenzi wa soko kwa ajili ya matunda na mboga mboga na kuondokana na adha ya kufanya biashara katika maeneo ambayo siyo rasmi.

Mavunde ameyasema hayo wakati akijibu kero za wafanyabiashara hao alipotembelea stendi ya mabasi hiyo eneo la Kikuyu Kusini na kuwahakikishia wafanyabiashara hao juu ya ujenzi na ukamilishaji wa soko ambalo litagharimu kiasi cha Shilioni Milioni Tisini na Mbili(*92,000,000*)

Aidha katika Mkutano wa hadhara wa wananchi Kikuyu Kusini,Mh Mavunde amewataka wananchi kushirikiana na viongozi wao katika ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule ya Msingi Kikuyu B ambapo Mbunge huyo ameahidi kuwachangia matofali 500 na mifuko ya saruji 50.

Wananchi wa Kata ya Kikuyu Kusini wamempongeza Mbunge Mavunde kwa jitihada kubwa anazofanya za kuwaletea maendeleo na kumuahidi kumpa ushirikiano katika uongozi wake.

JAFO AWASHUKIA TBA KWA KUKWAMISHA MIRADI

Posted by Esta Malibiche on DEC 28,2017 IN NEWS


   Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,TAMISEMI Mhe.Selemani Jafo akikagua ujenzi wa majengo mbalimbali wilaya ya Ikungi 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,TAMISEMI Mhe.Selemani Jafo(Mbele kulia) akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe. Miraji Mtaturu akifuatiwa na Mbunge wa Singida Magharibi Mhe. Elibariki Kingu wakati wa ukaguzi wa ujenzi wa miundombinu ya wilaya hiyo.



 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,TAMISEMI Mhe.Selemani Jafo(Mbele kulia) akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe. Miraji Mtaturu akifuatiwa na Mbunge wa Singida Magharibi Mhe. Elibariki Kingu wakati wa ukaguzi wa ujenzi wa miundombinu ya wilaya hiyo.

      ................................................................................

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe.  Selemani Jafo ameushukia Wakala wa Majengo nchini ( TBA) kutokana na kusuasua katika ujenzi wa miradi mbalimbali ya serikali waliyopewa na Tawala za Mikoa na Mamlaka za serikali za Mitaa(Tamisemi). 

Jafo ameonyesha kutoridhishwa na utendaji kazi wa TBA alipotembelea miradi mbalimbali ya maendeleo wilayani Ikungi mkoani Singida.

Katika ziara yake, Jafo ametembelea ujenzi wa makazi ya viongozi wa wilaya wa Ikungi ambapo muda uliopangwa kukamilisha kazi hiyo umeshapita huku kazi bado haijakamilika ambazo zinagharimu kiasi cha Sh.Milioni 700.

Kufuatia hali hiyo, Jafo ametoa miezi miwili kwa TBA kukamilisha ujenzi wa nyumba nne kwa ajili ya mkuu wilaya ya Ikungi mkoani Singida, Katibu tawala wa wilaya pamoja na watumishi wengine wa wawili ambazo zilitakiwa kukamilika tangu mwezi Septemba mwaka huu.

Jafo amesema mbali na nyumba hizo za Ikungi kuna nyumba nyingine katika wilaya ya Nkarama na wilaya mbalimbali hapa nchini ambazo zote ujenzi wake unasuasua sana licha ya Ofisi za Makatibu Tawala wa mikoa  kufanya malipo ya ujenzi wa majengo hayo TBA, pia
baadhi ya shule kongwe zinazo karabatiwa na TBA kasi ya utekelezaji ni ndogo.

“TBA mmekuwa na matatizo katika maeneo mengi sana kama hamuwezi mtuambie muendelea na kazi mnazopewa na serikali kuu sisi huku serikali za mitaa mtuache tuwape watu wengine wapo watu wanajengaa vizuri na kwa wakati kuliko nyinyi  tutawapa hata Suma JKT ambao pia wanao  tu katika kazi kama hizi “amesema Jafo.

Jafo ameitaka TBA kuyakamilisha majengo hayo haraka kabla ya mwezi Februari mwaka 2018 kwani viongozi wa wilaya wanateseka kwa kukosa makazi na Ofisi na pia ujenzi wa shule Kongwe walizopewa watoto wanakosa miundombinu bora.


Kwa upande wake, Mkuu wa wilaya hiyo Miraji Mtaturu, amesema kutokana na jengo la ofisi ya mkuu wa wilaya kutokamilika anatumia jengo ambalo lilikuwa darasa.

Alhamisi, 28 Desemba 2017

WAZIRI WA TAMISEMI SELEMANI JAFO APONGEZA UJENZI WA MIUNDOMBINU YA AFYA IKUNGI

Posted by Esta Malibiche on DEC 29,2017 IN NEWS

 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,TAMISEMI Mhe.Selemani Jafo(katikati) akipokelewa na Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe. Miraji Mtaturu(Pili Kulia) wakati alipofanya ziara ya Kikazi katika Halmashauri hiyo mapema leo.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,TAMISEMI Mhe.Selemani Jafo akisaini Kitabu cha wageni katika Kituo cha Ihanje wakati wa ziara yake Wilayani Ikungi.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,TAMISEMI Mhe.Selemani Jafo(Mbele kulia) akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe. Miraji Mtaturu akifuatiwa na Mbunge wa Singida Magharibi Mhe. Elibariki Kingu wakati wa ukaguzi wa ujenzi wa miundombinu ya Afya katika kituo cha Afya Ihanje.

 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,TAMISEMI Mhe.Selemani Jafo(Tatu kushoto) akimskiliza Mhandisi wa Ujenzi Sembua Mrisho wakati wa ukaguzi wa Jengo la upasuaji linalojengwa katika Kituo cha Afya Ihanje. 
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,TAMISEMI Mhe.Selemani Jafo (mbele) akiwa pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe. Miraji Mtaturu pamoja na Mbunge wa Singida Magharibi Mhe. Elibariki Kingu wakiongozwa na Mhandisi wa Majengo kukagua ujenzi wa miundombinu mbalimbali ya Afya inayojengwa katika Kituo cha Afya Ihanje kilichopo Ikungi.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,TAMISEMI Mhe.Selemani Jafo akifurahi jambo na Mbunge wa Singida Magharibi Mhe.Elibariki Kingu wakati wakikagua ujenzi wa miundombinu ya Afya katika Kituo cha Afya Ihanje.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,TAMISEMI Mhe.Selemani Jafo(Kulia) akikagua Ujenzi wa Kichomea Taka katika kituo cha Afya Ihanje.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,TAMISEMI Mhe.Selemani Jafo(katikati) akiwa na Viongozi wa Wilaya ya Ikungi katika picha ya pamoja na watumishi wa Kituo cha Afya Ihanje.

     ............................................................................................................................
Nteghenjwa,Hosseah,Ikungi-Singida.

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi) Mhe.Selemani Jafo amepongeza kazi nzuri  ya ujenzi wa miundombinu mbalimbali inayoendelea kujengwa katika Kituo cha Afya Ihanje kilichopo kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida.

Mhe.Jafo alitoa pongezi hizo wakati wa ziara yake Wilayani humo ya kukagua  miradi ya maendeleo na kuzungumza na watumishi wa Halmashauri ambapo akiwa kituoni hapo alisema ameridhishwa na usimamizi, ubora na maendeleo ya ujenzi wa Kituo cha Afya Ihanje.

Aliongeza kuwa Kituo cha Ihanje ni miongoni mwa Zaidi ya Vituo 200  vitakavyopekea/vilivyopokea Fedha kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya Afya ambayo ilikosekana hapo awali na kukifanya kituo hiki kutotoa huduma ipasavyo na agizo langu la awali ilikua kumaliza kazi ya ujenzi mnamo Dec 30,2017 lakini kwa Ikungi walichelewa kuanza utekelezaji kutokana na kupokea maelekezo mengine baadae ila wamefanya kazi nzuri hivyo wao watakamilisha Jengo hili mnamo January 2018.

Nimekagua majengo yote sita yanayojengwa kupitia uboreshaji huu hakika yanavutia na kupendeza, kuanzia Maabara, Wodi ya Kinamama, Chumba cha Upasuaji, Chumba cha kuhifadhia Maiti pamoja na kichomea Taka na ukizingatia ujenzi huu umewahusisha mafundi  kutoka kwenye Vijiji na Kata zetu ambapo kwa kuwatumia wao gharama za ujenzi hupungua ukilinganisha na  wakandarasi; Hii  inanipa faraja kubwa kuona kazi zinaenda vizuri kutoka kwa watalaam walioko kwenye jamii yetu, Alisema Mhe.Jafo.

Awali akitoa taarifa hiyo  Mhandishi wa Ujenzi, Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi  Sembua Mrisho amesema Fedha zilizopokelewa ni Tsh. Mil 720 kati ya hizo Mil 220 zimepelekwa bohari ya dawa kwa ajili ya  vifaa Tiba na Dawa mara majengo hayo yatakapokamilika na Tsh Mil 500 ndizo zinazotumika katika Ujenzi wa miundombinu yote sita na hali ya ujenzi mpaka sasa inaonyesha Fedha hizo zitakamilisha kabisa mradi huo kwa ubora unaotakiwa.

“Mara baada ya kupokea Fedha hizo na kupata Muongozo toka OR-TAMISEMI, Fedha zile zililetwa kwenye Kata na zikaundwa kamati Tatu ya Mapokezi, Manunuzi na Ujenzi na kazi yote hii imefanyika kwa kutumia “Local fund” na  inasimamia na Wakandarasi wa Halmashauri kwa kushirikiana na kamati za Ujenzi zilizopo” alisema Mrisho.

Akizungumza wakati wa Ziara hiyo Mbunge wa Ikungi Mhe.Elibariki Kingu amesema Ihanje ni Kata pia ni Makao Makuu ya Tarafa ya Ihanje na mradi huu umejibu shida za wananchi wa Ihanje na Ikungi kwa Ujumla kwa sababu Kituo hicho kinatoa huduma kwa wakinamama wengi wa Kata zaidi ya Tano zinazonguka eneo hili.

Aliongeza kuwa  Kituo cha Afya kilichkuwepo awali kilikuwa hakikidhi  mahitaji kutokana na kutokua na maeneo muhimu kama wodi nzuri na kubwa ya kina mama, maabara, sehemu ya kuhifadhia maiti nk lakini kwa sasa sisi wananchi wa Ikungi tunaishukuru sana Serikali yetu kwa kututatulia hangamoto hii.

Akizungumza kwa furaha Angelina Naaman(Mama Yasinta) amesema “Wakinana mama sasa tutaona raha Zaidi ya kujifungua kwa sababu tumepata mpaka chumba cha Upasuaji wakati awali ilikua ukishindwa kujifungua kawaida inakua mtihani sana kwako na kwa wauguzi wenyewe hivyo sasa zoezi la kujifungua kwetu litakua salama Zaidi kwa masiah yetu nay a mtoto.

Ukarabati sambamba na uboreshaji wa vituo vya Afya vinavyoendelea Nchini Kote utafanyika katika awamu na awamu ya kwanza ilianza Mwezi Sept 2017 na utakamilika January, 2018 na umehusisha vituo 44 wakati awamu ya Pili itaanza mwenzi January 2017 utahusisha Vituo vya Afya 161.

WAZIRI MKUU AKAGUA UJENZI WA ZAHANATI MIBURE

Posted by Esta Malibiche on DEC 29,2017 IN KITAIFA


PMO_3575 airport
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Lindi Godfrey Zambi, alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa Nachingwea, kwa ajili ya mapumziko ya mwisho wa mwaka ambapo aliamua kukagua miradi ya maendeleo jimboni kwake wilayani Ruangwa, mkoani Lindi, Desemba 28, 2017.
PMO_3641 mibure
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na mwananchi wa kijiji cha Mibure, Mzee Menrad Kilian, baada ya kukagua ujenzi wa zahanati kijijini hapo, wilayani Ruangwa mkoani Lindi, Desemba 28, 2017.
PMO_3661 mibure
Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akizungumza na wananchi wa kijiji cha Mibure, wakati alipoenda kukagua ujenzi wa zahanati ya kijiji hicho Desemba 28, 2017. Waziri Mkuu yupo jimboni kwake kwa mapumziko ya mwisho wa mwaka.
PMO_3699 namakuku
Mkurugenzi Mtendaji wa KALIF Construction, Ally Mohamed Libaba akitoa maelezo kwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa (katikati) wakati wakijaribu kuvuta maji kutoka kwenye pampu ya mradi wa maji wa kijiji cha Namakuku, Desemba 28, 2017. Wa kwanza kulia ni msimamizi wa mradi huo, Bw. Fadhil Ally Libaba.
Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu
………….
*Aagiza zahanati ikiisha ipelekewe kifaa ca kutunzia watoto njiti
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameanza ziara fupi ya siku tatu, kukagua
miradi ya maendeleo jimboni kwake katika wilaya ya Ruangwa mkoani
Lindi.
Waziri Mkuu ambaye yuko kwenye mapumziko ya mwisho wa mwaka, amekagua
miradi ya maji, ujenzi wa zahanati na kuzungumza na wananchi kaika
vijiji vya Mibure, Namakuku, Chienjere, Namahema A na Namahema B.
Akizungumza na wakazi wa kijiji cha Mibure leo mchana (Alhamisi,
Desemba 28, 2017) mara baada ya kukagua zahanati ya kijiji hicho,
Waziri Mkuu alisema ameridhishwa na ujenzi unavyoendelea na akamwagiza
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Ruangwa ahakikishe zahanati hiyo
ikikamilika inapata kifaa cha kuwatunzia watoto njiti kwa sababu
kijiji hicho kiko mbali na Hospitali ya Wilaya ya Ruangwa.
“Nilileta makontena yenye vifaa vya hospitali, na humo ndani mlikuwa
na vifaa vya kuwatunza watoto njiti (watoto wanaozaliwa kabla ya muda
kutimia). Hakikisha hawa wanapata kifaa hicho kwa sababu hawana gari
la kubeba wagonjwa, na pia wako mbali na hospitali ya wilaya na pia
kituo cha afya cha jirani kiko mbali pia,” alisisitiza.
Akizingumzia kuhusu upatikanaji wa umeme kijiji hapo, Waziri Mkuu
alisema: “Mibure ipo kwenye mipango ya kupata umeme ambao unatoka
Nagurukuru, -Nghimbwa-Chienjere-Namakuku-Mibure.”
Aliwataka vijana wa kata hiyo, wachangamkie fursa kwa muanda mitaji ya
kuwa na gereji za kuchomelea vyuma, saluni na viwanda vidogo vya
usindikaji.
Mapema, akisoma taarifa ya ujenzi wa zahanati ya Mibure mbele ya
Waziri Mkuu, Mwenyeiti wa kijiji hicho, Bw. Samwel Chilemba alisema
mradi huo umekwishagharimu sh. milioni 52, ambapo kazi zilizokamiliak
ni jengo la zahanati, kichomea taka na choo chenye matundu matatu.
Alisema wanakabiliwa na changamoto ya kupanda holela kwa gharama za
vifaa vya ujenzi, kupokea michango kidogo kutoka kwa wananchi, ukosefu
wa nyumba ya mganga na wauguzi na kiasi cha fedha cha sh. milioni 8.26
za kununulia samani.
Bw. Chilemba alisema kukamilika kwa ujenzi wa zahanati hiyo kutasaidia
wakazi wa vijiji jirani vya Njawale, Namakuku, na vijiji jirani vya
wilaya ya Nachingwea ambavyo vinapakana na wilaya ya Ruangwa.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
ALHAMISI, DESEMBA 28, 2017

MAVUNDE AWATAKA POLISI JAMII KUUNDA VIKUNDI VYA UZALISHAJI MALI KUJIKWAMUA KIUCHUMI

Posted by Esta Malibiche on Dec 28,2017



Naibu Waziri wa Nchi-Ofisi ya Waziri Mkuu( Kazi,Vijana na Ajira) Mh Anthony Mavunde amewataka Vijana ambao wanashiriki katika mafunzo ya Ulinzi shirikishi kupitia Polisi Jamii kuunda vikundi vya uzalishaji mali ili kujikwamua kiuchumi na kuongeza kipato.

Mavunde ameyasema hayo leo wakati akifunga mafunzo ya Ulinzi shirikishi yaliyoshirikisha Vijana 75 katika kata ya Mtumba,Manispaa ya Dodoma.

“Pamoja na jukumu kubwa mlilonalo na ulinzi na usalama wa raia na mali zao,lakini pia mhakikishe mnatumia mkusanyiko wenu kuunda vikundi vya uzalishaji mali ili kujiongezea kipato na kutengeneza nafasi za Ajira zaidi”

Mavunde amewataka vijana hao kuyatumia vyema mafunzo waliyopata kwa kuwa waadlifu,waaminifu na wazalendo kwa Taifa lao na kusimama mstari wa mbele kuhakikisha Taifa hili linaendelea kuwa na AMANI na UTULIVU.

Naye Kamanda wa Mkoa wa  Polisi wa Dodoma,SACP Muroto amewataka Vijana zaidi kujitokeza katika Ulinzi shirikishi ili kuimarisha usalama na amani katika mkoa wa Dodoma.

Jumamosi, 23 Desemba 2017

*MAVUNDE KUENDESHA OPARESHENI MAALUM YA KUKAGUA WAAJIRI AMBAO HAWAJATEKELEZA AGIZO LA WAZIRI MHAGAMA LA KUJIUNGA NA MFUKO WA FIDIA KWA WAFANYAKAZI(WCF) NCHINI*

Posted by Esta Malibiche on DEC 23,2017 IN NEWS


 NAIBU Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu(Kazi,Vijana na Ajira) Mh Anthony Mavunde ameendelea kukazia maagizo ya Mh Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Mh Jennister Mhagama aliyoyatoa kuwataka waajiri wote wawe wamejisajili katika mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi(WCF) kwa kubainisha kwamba kwasasa inaendelea operesheni maalum ya kuhakikisha maagizo hayo ya waajiri kujisajili katika mfuko wa fidia yanatekelezwa kwa mujibu wa sheria.

Mavunde ameyasema hayo leo wakati akifungua Baraza la kwanza la Wafanyakazi wa mfuko wa fidia kwa Wafanyakazi(WCF)katika makao makuu ya ofisi za WCF Jijini Dar es salaam kwa kuwataka waajiri wote nchini kutekeleza sharti la kisheria la kujiunga na mfuko wa huo wa fidia ili kuilinda nguvu kazi ya Tanzania kutokana na madhara/magonjwa yatokanayo na kazi na kuahidi kwamba atalisimamia agizo la Waziri kwa kuendesha operesheni ya ukaguzi nchi nzima kubaini waajiri ambao bado hawajatekeleza takwa hilo la kisheria ambao kwa mujibu wa maelezo ya Mh Naibu Waziri Mavunde watachukuliwa hatua kali za kisheria.

Aidha Mkurugenzi Mkuu wa WCF Ndg Masha Mshomba amebainisha kwamba Mwajiri yoyote atakayekutwa  hajajisajili katika Mfuko atachukuliwa hatua kali za kisheria ikiwamo faini isiyozidi *Tsh 50m* au kifungo cha *miaka 5* Jela kwa Mkuu wa Taasisi husika au vyote kwa pamoja kama ilivyoainishwa katika kifungu cha *71(4) cha Sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi No. 20 ya Mwaka 2008*