Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru Askofu Msaidizi wa Kanisa
Katoliki la Watakatifu Wote Jimbo la Mtwara Fr. Patrick Mwaya mara baada
ya mahubiri katika Kanisa hilo. Rais Dkt. Magufuli amechangia Kanisa
hilo Mifuko 200 ya Saruji kwa ajili ya kuendeleza kazi ya ujenzi wa uzio
Kanisani hapo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwasalimia Waumini wa Kanisa
Katoliki la Watakatifu Wote Jimbo la Mtwara mara baada ya mahubiri.
Kaimu Katibu wa Rais Ikulu, Ngusa
Samike(Kushoto) akimkabidhi Askofu Msaidizi wa Kanisa Katoliki la
Watakatifu Wote Jimbo la Mtwara Fr. Patrick Mwaya mifuko 200 ya Saruji
ili kutimiza Ahadi ya Rais aliyoitoa kanisani hapo.
Kaimu Katibu wa Rais Ikulu, Ngusa
Samike(Kushoto) akimkabidhi fedha kiasi cha Shilingi Milioni 35 kwa Mkuu
wa Mkoa wa Lindi Godfrey Zambi ili kutekeleza ahadi aliyoitoa Rais
wakati alipopita katika Kijiji cha Somanga na Mnonela. Katika kijiji cha
Somanga Rais Dkt. Magufuli aliahidi kuchangia kiasi cha Shilingi
Milioni 20, kwa ajili ya ujenzi wa Kituo cha Afya na kwa upande wa
Mnonela aliahidi kiasi cha Shilingi milioni 15 kwa ajili ya kumalizia
ujenzi wa Kituo cha Afya.
Mkuu wa Mkoa wa Lindi Godfrey
Zambi akisaini kuthibitisha kupokea kiasi hicho cha fedha ambazo ni
utekelezaji wa Ahadi za Rais Dkt. Magufuli wakati alipofanya ziara
mkoani humo.
Rais Dkt. John Pombe Magufuli
akizungumza katika kituo cha Afya mnonela katika Jimbo la Mtama ambapo
aliahidi kuchangia kiasi cha fedha Shilingi Milioni 15 ambazo tayari
Mkuu wa Mkoa wa Lindi ameshakabidhiwa.
PICHA NA IKULU
0 maoni:
Chapisha Maoni