Alhamisi, 9 Machi 2017

KIKAO CHA BARAZA LA MADIWANI HALMASHAURI YA MJI WA MAFINGA CHAMSIMAMISHA DIWANI WA KATA YA BOMA KUTOSHIRIKI VIKAO NA KAMATI ZA MADIWANI KWA KOSA LA KUKATAA KUSOMA TAARIFA YA KATA YAKE

Posted by Esta Malibiche on MARCH 9,2017 IN NEWS
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Mafinga Charles Makoga,ambae pia ni Diwani wa kata ya Isalavavu
 Akizungumza jana mara baada ya kikao kifupi,kufanyika na kumjadili Diwani huyo,Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa MAFINGA Charles Makoga ambae ni Diwani wa kata ya Isalavanu alisema kuwa kanuni ya 18[1] inasema kuwa  katika Mkutano wowote wa Halimashauri kama mjumbe ataonyesha kukosa heshima kwa madaraka aliyonayo mwenyekiti  kudharau kanuni za Halmashauri kwa kuzuia kwa makusudi shughuli za Halmashauri zisiendelee au vinginevyo,Mwenyekiti ataelekeza Mutano  kwa tukio hilo kwa kumtaja  jina mara tatu mtu anaeyehusikana.

 Makoga alisema,endapo baada ya kutajwa jina mjumbe ataendelea kudharau madaraka ya mwenyekiti,basi mwenyekiti ataliomba baraza kuairisha shughuli za mkutano na kutafakari jambo hilo.
 ‘’Baada ya kukaa na kutafakari jambo hili, Mh.Julius kisoma anakosa la kutoheshimu kiti,kukaidi kusoma taarifa na kwenda kukaa bila kuamliwa na Mwenyekiti,hivyo basi kwa mamlaka niliyopewa kwa kosa hilo ninamsimamisha kutohudhuria vikao vitatu vya baraza na kamati za madiwani na kupoteza haki zake za msingi alizokuwa akizipata kipindi hicho,pia kwa kosa la kukataa kusoma taarifa naiagiza kamati ya maadili ndani ya mwezi mmoja wafanye kikao chao na kuleta taarifa sahihi katika kikao kijacho,na baraza litafikiria maamuzi mengine,Hivyo ninamuomba Julist Kisoma atoke Nje akaendelee na Shughuli nyingine ili kikao kiendelee ’’’alisema Makoga
Diwani wa kata ya Boma kupitia chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema JULIST kisoma aliyesimamishwa kushiriki vikao vya baraza la madiwani


  Michael Msite diwani wa kata ya Upendo Halmashauri ya Mji wa Mafinga,akisoma taarifa ya utekelezaji wa kata kwa  kipindi cha robo ya pili ya mwaka kuanzia October hadi Dec 2016, kwenye kikao cha baraza la madiwani kilichofanyika tarehe 8,3,2017


  Michael Msite diwani wa kata ya Upendo Halmashauri ya Mji wa Mafingakupitia chama chama cha Mapinduzi ccmkisoma taarifa ya utekelezaji wa kata kwa  kipindi cha robo ya pili ya mwaka kuanzia October hadi Dec 2016, kwenye kikao cha baraza la madiwani kilichofanyika tarehe 8,3,2017

 Ezekiel Kihndo Diwani wa kata ya Bumilayinga kupitia chama chama cha Mapinduzi ccmkisoma taarifa ya utekelezaji wa kata kwa  kipindi cha robo ya pili ya mwaka kuanzia October hadi Dec 2016, kwenye kikao cha baraza la madiwani kilichofanyika tarehe 8,3,2017
 Denis Kutemile Diwani wa kata ya Sao Hill kupitia chama cha Mapinduzi ccmkisoma taarifa ya utekelezaji wa kata kwa  kipindi cha robo ya pili ya mwaka kuanzia October hadi Dec 2016, kwenye kikao cha baraza la madiwani kilichofanyika tarehe 8,3,2017
 Chesco Luvyale Diwani wa kata ya Kinyanambo kupitia chama cha Mapinduzi ccmkisoma taarifa ya utekelezaji wa kata kwa  kipindi cha robo ya pili ya mwaka kuanzia October hadi Dec 2016, kwenye kikao cha baraza la madiwani kilichofanyika tarehe 8,3,2017

 
Damiani Kyando  diwani wa kata ya  Wambi kupitia chama cha Demokrasia na Maendeleo chadema,akishiriki kiao
 Kikao cha baraza la Madiwani kikiendelea
 Madiwani wakiwa kwenye kikao
  Kikao cha baraza la Madiwani kikiendelea

0 maoni:

Chapisha Maoni