Posted by Esta Malibiche on MARCH 15,2017 IN NEWS
NEW YORK:
Naibu Waziri wa Afya , Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mheshimiwa Dkt. Hamisi Kigwangalla (Mb)
ameongoza ujumbe wa Tanzania wa wizara zinazohusika na mambo ya
uwezeshaji wa wanawake kiuchumi za Tanzania Bara na Zanzibar juu ya
uwezeshaji wa Wanawake Waliopo kwenye sekta isiyo rasmi, mjini New York
City, Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa, kwenye Mkutano wa 61 wa Kimataifa
wa Kamisheni ya Hali ya Wanawake Duniani.
Katika hotuba yake katika mkutano huo
wa Mawaziri wa Wanawake Duniani, Dk. Kigwangalla ameeleza mambo
mbalimbali ikiwemo hatua tulizofikia kama nchi kwenye kuleta usawa wa
kijinsia na ukombozi wa mwanamke wa kitanzania hususani kiuchumi ikiwemo
vikwazo vya kimila vinavyomfanya mwanamke kuwa wa hali ya chini kwenye
jamii, pamoja na changamoto anazokumbana nazo mwanamke kwenye ajira
zisizo rasmi (informal sector) ambapo wanawake ni wengi (asilimia 82)
ukilinganisha na wanaume (asilimia 72).
“Ilikufikia malengo, Jitihada za
serikali za nchi yetu kuanzia kuweka usawa wa kijinsia na kupinga
ubaguzi kuanzia kwenye katiba yeti, sera ya mikopo midogo midogo, sheria
zinavyoweka sharti la mali za wanandoa kutowekwa dhamana ama kuuzwa
kama mwanandoa mmoja hajaridhia, uanzishwaji wa mfuko wa maendeleo ya
wanawake kwenye halmashauri zote 114 Tanzania bara ambapo asilimia 5 ya
bajeti ya mapato ya ndani ya halmashauri ni lazima iende kwa wanawake.
Pia jitihada tunazofanya
kuwahamasisha wanawake wamiliki mali, warasimishe biashara zao
(Mkurabita), pia waraimishe vikundi vyao vya kuweka akiba na kukopa na
vya kusaidiana” Ameeleza Dk. Kigwangalla kwenye mkutano huo.
Aidha, Dk. Kigwangalla amebainisha
kuwa, kwa upande wa Tanzania, Serikali imepiga jitihada kubwa
kuhakikisha inamkomboa mwanamke kutoka kwenye utegemezi kwa kuunda
vyombo mbalimbali na kuandaa sera na miongozo inayoelekeza usawa katika
kufikia malengo ya kumkomboa mwanamke kiuchumi ambapo mwanamke anakuwa
na haki na uwezo wa kukopa katika taasisi mbalimbali ili kuanzisha au
kukuza mtaji wa biashara yake katika kufikia malengo aliyotarajia.
Vile vile imeanzisha mfuko wa maendeleo
katika halmashauri zote 114 nchini ili kuwafikia wanawake walio wengi
zaidi, imeendelea kuhamasisha Jamii kuanzisha mifuko mbalimbali ya
kuweka na kukopa kama vile (VIKOBA) , kuwahamasisha kushiriki katika
maonyesho mbalimbali ya kitaifa na hata mikutano mikubwa ya kimataifa
ili kujitangaza na kukuza bidhaa mbalimbali kwa lengo la kujipatia
kipato na kukuza mitaji yao.
Ameongeza k uwa, kufanya hivyo,
kunawasaidia kutengeneza mitandao ya kibiashara itakayowasaidia kukua
kimataifa na kufanya biashara Kubwa za kimataifa na pia kutoa ajira kwa
Wanawake wenzao . Pia Serikali imeanzisha benki ya Wanawake ambayo Kazi
yake Kubwa ni kutoa mikopo na ushauri ambao utawasaidia kukuza biashara
zao na kuongeza kipato kwani Wanawake ni Jeshi kubwa ambalo linachangia
uchumi wa nchi kwa kiasi kikubwa.
Mheshimiwa
Dkt. Hamisi Kigwangalla (Mb) , Naibu Waziri wa Afya , Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto akichangia mada katika kikao cha
ngazi ya Mawaziri kuhusu uwezeshaji wa Wanawake Waliopo kwenye sekta
isiyo rasmi .
0 maoni:
Chapisha Maoni