Posted by Esta Malibiche on MARCH 9,2017 IN NEWS
Mkuu
wa Wilaya ya Kisarawe, Happyness William Seneda (katikati), akihutubia
kwenye kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yaliyofanyika
kimkoa viwanja vya Shule ya Msingi Chanzige wilayani Kisarawe jana.
Kulia ni Mwenyekiti wa Halmshauri ya Kisarawe, Khamis Dikupatile na
Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Pwani, Germana Mnga’alo.
Mwenyekiti wa Halmshauri ya Kisarawe, Khamis Dikupatile, akipima shinikizo la damu katika maadhimisho hayo.
Diwani wa Kata ya Kisarawe, Abel Mudo akipima afya.
Ofisa
Mikopo wa Benki ya Equity, Nelifyage Mbwilo (kulia), akitoa maelezo kwa
Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Happyness Seneda (wa pili kushoto), wakati
alipokuwa akitembelea mabanda ya wajasiriamali katika maadhimisho hayo.
Kutoka kushoto ni Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Pwani, Germana Mnga’alo na Mwenyekiti wa Halmshauri ya Kisarawe, Khamis Dikupatile.
Wanafunzi wa Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Wilaya ya Kisarawe wakionesha kazi wazifanyazo.
Wajasiriamali wakiwa na bidhaa zao mbalimbali wanazozalisha.
Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Happyness (katikati), akiserebuka na wanawake katika maadhimisho hayo.
DC
Seneda akiserebuka na wanawake. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi
ya Winamwanga Caltural Heritage Association, Mwajuma Motto.
Wanafunzi wakiwa kwenye maadhimisho hayo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmshauri ya Wilaya ya Kisarawe, Mussa Gama (kulia), akimuelekeza jambo Mkuu wa Wilaya hiyo, Happyness Seneda. |
Wanafunzi wakiwa kwenye maadhimisho hayo.
Wadau wa maendeleo kutoka Taasisi ya Jumuiya ya Miradi ya Maendeleo
Kisarawe na Ilala(JUMIMAKI) wakiwa kwenye maadhimisho hayo. Katikati ni Katibu wa Hatibu Baruti.
Kisarawe na Ilala(JUMIMAKI) wakiwa kwenye maadhimisho hayo. Katikati ni Katibu wa Hatibu Baruti.
Mkuu wa
Wilaya ya Kisarawe, Happyness Seneka (katikati kulia na Kaimu Katibu
Tawala Mkoa wa Pwani, Germana Mnga’alo wakiwa katika picha ya pamoja na
vijana wa Skauti wakati wa maadhimisho hayo.
Katibu Tawala wa Wilaya ya Kisarawe, Ntela Mwampamba (kushoto), akizungumza kwenye maadhimisho hayo.
Madiwani wa Wilaya hiyo wakiwa kwenye hafla hiyo.
Maadhimisho yakiendelea.
Mkurugenzi Mtendaji
wa Taasisi ya Winamwanga Caltural Heritage Association, Mwajuma Motto
akisoma risala kwa niaba ya wadau wa maendeleo wa wilaya hiyo.
Mdau wa maendeleo, Christina Lusian akisoma risala
mbele ya mgeni rasmi.
Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Pwani, Germana Mnga’alo, akihutubia kwenye hafla hiyo.
Mkuu wa
Dawati la Jinsia Mkoa wa Pwani, Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP),
Yusta Milinga akizungumzia ukatili wa kijinsia kwenye maadhimisho hayo.
Mkuu wa
Wilaya ya Kisarawe, Seneda akikabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya
sh.milioni 61,550 kwa ajili ya mikopo kwa vikundi vya wajasiriamali
wilayani humo iliyotolewa na Benki ya NMB.
Wadau wa
maendelea wakiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa wilaya hiyo baada ya
kukabidhi msaada wa magodoro na vifaa vingine vyenye thamani ya
sh.700,000.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Tanzania Kwanza Foundation, Hidaya Chomvi akisalimiana na Mkuu wa Wilaya baada ya kumkabidhi zawadi.
Brass Bandi ya Magereza ikitumbuiza kwenye maadhimisho hayo.
Na Dotto Mwaibale
MKUU wa
Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo ameziagiza Halmshauri zote za
mkoa huo kuhakikisha kuwa zinatenga asilimia tano ya mapato yao ya ndani
kwa ajili ya mfuko wa maendeleo ya wanawake.
Agizo
hilo lilitolewa kwa niaba yake na Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Happyness
Seneda kwenye kilele cha maadhimisho ya siku ya wanawake duniani
yaliyofanyika kimkoa viwanja vya Shule ya Msingi Chanzige wilayani humo
jana. Ndikilo alikuwa mgeni rasmi kwenye maadhimisho hayo.
“Wakurugenzi
wa Halmashauri ambazo hazitatekeleza wajibu wahakikishe wanajitahidi
kufanya jukumu hilo muhimu kwa maendeleo ya wanawake wa mkoa huo”
alisema Seneda.
Alisema
katika kuwawezesha wanawake kiuchumi, Serikali imeanzisha Benki ya
Wanawake Tanzania, mifuko mbalimbali ukiwemo mfuko wa maendeleo ya
wanawake (WDF) pamoja na kuhamasisha uanzishaji wa Saccos, vikundi vya
uzalishaji mali na Vicoba na kwa kupitia fursa zilizopo kuwawezesha
wanawake wajasiriamali kupata mikopo yenye masharti nafuu.
Alisema
katika mkoa huo kuna jumla ya vikundi vya uzalishaji mali 1, 350 vyenye
wanachama 5,411 lengo likiwa ni kumuwezesha mwanamke kushiriki katika
kuleta mabadiliko ya kiuchumi kuanzia ngazi ya familia na Taifa kwa
ujumla.
Seneda
akizungumzia wilaya yake alihimiza suala zima la elimu na kuwataka
wazazi kuwa mstari wa mbele kusimamia watoto wao na kupiga vita mimba za
utotoni na kuwaoza watoto wao.
Alisema serikali haitamvumilia mzazi au mlezi yeyote atakayebainika kuozesha mtoto wake na mtu atakaye mpa mimba mwanafunzi.
(Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)
(Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)
0 maoni:
Chapisha Maoni