Posted by Esta Malibiche on MARCH 20,2017 IN NEWS
WAfanyabiashara wa mazao ya misitu wilayani Mufindi wakiwa kwenye
mkutano wa pamoja kati ya mbunge,TRA na wafanyabiashara uliofanyika jana wilayani humo.
Mkutano wa pamoja kiendelea baina ya WAfanyabiashara wa mazao ya misitu wilayani Mufindi , mbungeu na TRA.
|
Mbunge wa mafinga mjini Cosato Chumi akiongea na Wafanyabiashara
wa mazao ya misitu katika mkutano uliofanyika jana wilayani humo, juu
ya malamiko ya wafanyabiashara na TRA mkoa wa Iringa.
MUFINDI
WAFANYABIASHARA wa mazao ya misitu
wilayani Mufindi wamesema kuwa soko la mbao limeshuka kwa kiwango kikubwa
kutoka na mrundikano wa kodi katika wilaya hiyo tofauti na wilaya nyingime.
Akizungumza
mmoja wa wafanyabiashara hao Zakayo Kenyatta Katika mkutano wa wafanyabiashara
wa mazao ya misitu na TRA alisema kuwa TRA wamekuwa wasumbufu sana check point
kwa kuwasimamisha zaidi ya siku tatu wakidai lisiti hizo huku wafanyabiashara
wakionyesha barua za watendaji kutoka vijiji walivyonunulia zikikataliwa.
"Tunawaomba TRA mkatoe elimu kwa
mkulima mmoja mmoja kwa sababu ni ngumu sana mkulima wa chini akuulizie nguzo 5
alafu awe na lisiti ya mashine kwa hiyo tunawaomba TRA wakatoe elimu hiyo na
kuwaamasisha wakulima hawa Kuwa na hizo mashine kwani wakulima hao ni wale
ambao wanauza miti yako kutokana na matatizo mbali mbali walionayo na sio
kampuni" alisema Kenyatta
Akijibu hoja hiyo meneja msaidizi wa
TRA Mkoa wa Iringa Mustapha Mkilamwenye alisema Kuwa wamekuwa wakiogopa kwenda
kutoa elimu hizo kwa wakulima kutokana na mkutano yao kuharibika kwa kuzomewa
na kutokufikia muafaka kiuelimishaji.
Mkilamwenye amewataka wafanyabiashara
hao kupata kibari cha kununua na kusafirisha kutoka TRA wilaya au mkoa kabla
hqwqjaenda vijijini kununua ili kukwepa uwumbufu huo katika vituo vya kukaguliwa
[check point].
"Ombi lenu tumelipokea hivyo
tunawaomba kabla hamjanunua mpate kibali kutoka TRA mkoa au wilayani kuokoa
usumbufu WA tozo za ushuru check point, pia tutatoa elimu ya matumizi ya
mashine kwa wakulima vijijini wauzapo miti yako kwa wafanyabiashara"
alisema Mkilamwenye.
Aidha wafanyabiasha hao wameiomba
mamlaka ya mapato mkoa wa iringa TRA kutoa kibali cha usafirishaji kwa kuondoa
usumbufu wa tozo za ushuru check point na kuombwa lisiti za mashine kutoka kwa
wakulima waliowauzia mbao na nguzo.
Kwa upande wake Mbunge wa mafinga mjini
Cosato Chumi alisema Kuwa ameamua kuwakutanisha wafanyabiashara na TRA kupata
ufafanuzi WA kuombwa ushuru check point kutokana na kulalamikiwa na
wafanyabiashara hao Kuwa magari yako wamekuwa wakikaa check point zaidi ya siku
tatu wakiombwa lisiti za mashine kutoka kwa wakulima waliowauzia nguzo na mbao.
"Mkutano huku ni mahususi kwa
wrote tukipata ufafanuzi na kujua kwa nini mnakamatwa check point na mkiobwa
ushuru au njia kila mkoa,tra wanapaswa Kuwa rafiki Wa wafanyabiashara na sio
adui kwa sababu mufindi ndio chanzo kikuu cha mapato ya nchi kutokana na zao LA
mbao" alisema Chumi
Nae Meneja wa TRA wilayani ya Mufindi
Filmoni Mwakapesile alisema Kuwa "ni kweli tuhuma hizo na lawama
tumezipata na tumekuwa tukipokea simu nyingi za wafanyabiashara na kutatua
matatizo yako lakini Leo tunashukuru Mbunge amekututanisha na tumewapa uelewa
na sisi kama TRA tumewaambia mini cha kufanya kuondoa huo usumbufu.
0 maoni:
Chapisha Maoni