Jumatatu, 27 Machi 2017

ZANTEL YAZINDUA MTANDAO WENYE KASI ZAIDI WA 4G NA HUDUMA ZA KIBENKI KWA NJIA YA SIMU KISIWANI PEMBA

Posted by Esta Malibiche on MARCH 27,2017

Naibu Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Mohamed Ahmada akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa mtandao wenye kasi zaidi wa 4G na huduma za kibenki zinazofuata kanuni za kiislamu zitakazotolewa kwa njia ya simu na Kampuni ya Zantel kwa kushirikiana na Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) kisiwani Pemba. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mawasiliano ya Zantel Tanzania Benoit Janin na Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Kibenki zinazofuata misingi ya Kiislamu wa Benki ya watu wa Zanzibar (PBZ) Said Mohamed Said. Hafla hiyo ilifanyika katikati ya wiki Kisiwani Pemba.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mawasiliano ya Zantel Tanzania Benoit Janin (kulia) akimsikiliza Mkuu wa Zantel-Zanzibar, Mohamed Musa Baucha wakati wa hafla ya uzinduzi wa mtandao wenye kasi zaidi wa 4G na huduma za kibenki zinazofuata kanuni za kiislamu zitakazotolewa kwa njia ya simu na Kampuni ya Zantel kwa kushirikiana na Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) kisiwani Pemba. Hafla hiyo ilifanyika katikati ya wiki Kisiwani Pemba.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mawasiliano ya Zantel Tanzania Benoit Janin (wa pili kushoto) na Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Kibenki zinazofuata misingi ya Kiislamu wa Benki ya watu wa Zanzibar (PBZ) Said Mohamed Said wakipongezana mara baada ya uzinduzi wa mtandao wenye kasi zaidi wa 4G na huduma za kibenki zinazofuata kanuni za kiislamu zitakazotolewa kwa njia ya simu na Kampuni ya Zantel kwa kushirikiana na benki hiyo kwa wananchi wa kisiwani Pemba. Katikati ni Naibu Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Mohamed Ahmada. Hafla hiyo ilifanyika katikati ya wiki Kisiwani Pemba.

Naibu Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Mohamed Ahmada (wa tatu kushoto) akifurahia jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mawasiliano ya Zantel Tanzania Benoit Janin (wa pili kushoto), Mkuu wa Zantel-Zanzibar, Mohamed Musa Baucha (kushoto) na Meneja wa Benki ya watu wa Zanzibar-Pemba Mohamed Musa (kulia) mara baada ya kuzindua mtandao wenye kasi zaidi wa 4G na huduma za kibenki zinazofuata kanuni za kiislamu zitakazotolewa kwa njia ya simu na Kampuni ya Zantel kwa kushirikiana na Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) kisiwani Pemba. Hafla hiyo ilifanyika katikati ya wiki Kisiwani Pemba.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Mohamed Ahmada akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya kuzindua rasmi mtandao wenye kasi zaidi wa 4G na huduma za kibenki zinazofuata kanuni za kiislamu zitakazotolewa kwa njia ya simu na Kampuni ya Zantel kwa kushirikiana na Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) kwa wananchi wa kisiwani Pemba. Hafla hiyo ilifanyika katikati ya wiki Kisiwani Pemba. 
Naibu Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Mohamed Ahmada (wa pili kushoto) na Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Kibenki zinazofuata misingi ya Kiislamu wa Benki ya watu wa Zanzibar (PBZ) Said Mohamed Said wakizindua huduma za mtandao wenye kasi zaidi wa 4G wa Zantel na huduma za kibenki zinazofuata kanuni za kiislamu zitakazotolewa kwa njia ya simu na Kampuni hiyo kwa kushirikiana na Benki hiyo kisiwani Pemba. Wanaoshughudia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mawasiliano ya Zantel Tanzania Benoit Janin (kushoto) na Mkuu wa Zantel-Zanzibar, Mohamed Musa Baucha. Hafla hiyo ilifanyika katikati ya wiki Kisiwani Pemba. 

Kampuni ya mawasiliano ya ZANTEL imezindua mtandao wenye kasi zaidi wa 4G sambamba na huduma za kibenki zinazozingatia kanuni za kiislamu kwa njia ya simu ikiwa ni hatua ya kuboresha na kupanua huduma zake kwa wateja.

Katika hatua ya kuboresha huduma za kibenki kwa njia ya simu, Zantel imeshirikiana na BENKI ya watu wa Zanzibar (PBZ) katika kuhakikisha wateja wake wanapata huduma zote za kibenki kama vile kuweka au kutoa fedha, mikopo, kulipia ankara zao za huduma mbalimbali kama vile maji, umeme au kununua vocha za simu n.k.

Akizindua huduma hizo leo (23/03/2017) kisiwani Pemba, Naibu Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhe. Mohamed Ahmada alisema huduma hizo kutoka Zantel zimekuja katika wakati muafaka kwa wananchi wa Pemba na kuongeza kuwa yeye na Wizara yake wanaendelea kufanya kazi kwa ukaribu na mitandao mingine ya simu katika kuhakikisha huduma za simu zinaboreshwa zaidi visiwani humo.

“Uzinduzi wa huduma ya mtandao wenye kasi zaidi wa 4G sambamba na huduma ya kibenki kwa njia ya simu ni vitu ambavyo wananchi wa Pemba wamekua wakivisubiria kwa muda mrefu. Niipongeze Kampuni ya mawasiliano ya Zantel kwa kulitambua jambo hili na kulifanyia kazi kwa haraka” alisema.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Zantel, Benoit Janin amesema uzinduzi wa huduma hizo mpya ni moja kati ya jitihada zinazofanywa na kampuni yake katika kutoa huduma zenye ubora nchini ili kutimiza mahitaji mbalimbali ya wateja wao.

Aliongeza kuwa huduma ya kibenki kwa njia ya simu za mkononi imewalenga watu wote ila zaidi ikiwa ni jamii ya kiislamu kwani inazingatia kanuni na misingi yote ya kiislamu wakati wa utoaji wa huduma.

“Pamoja na kurahishisha huduma za kibenki huduma kwa njia ya simu, huduma hii pia itasaidia kuokoa muda, ni huduma rafiki kwa kila mtu na yenye usalama mkubwa” alisema Benoit.

Kwa mujibu wa Taarifa za Benki kuu ya Tanzania (BoT) ni kuwa watumiaji wa huduma za kifedha kupitia simu za mikononi wamefanya miamala yenye thamani ya bilioni 988.9 katika kipindi cha pili cha mwaka jana,huku mitandao ya simu ikigeuka kuwa njia muhimu katika miamala ya malipo mbalimbali.

Janin aliendelea kuwahakikishia wateja wa Zantel kuwa kampuni ya Zantel imekuwa katika ushindani kwa muda mrefu na kuwa bado wanaendelea kuwekeza ili kuhakikisha wateja wake wanapata huduma bora zaidi kwa kiwango kikubwa na teknolojia bora zaidi

“Tutaendelea kufikisha huduma hizi kwenda sehemu mbalimbali za hapa nchini, huu ni mwanzo tu kwa wateja wa Zantel ningependa wategemee mambo mazuri zaidi”.

Kampuni ya Mawasiliano ya simu ya Zantel, inaongoza kwa asilimia 80 kwenye soko la mitando ya simu kwa Zanzibar na ndiyo kampuni ya kwanza kutambulisha huduma za kibenki kwa njia ya simu hapa nchini.

Ni hivi karibuni tu ambapo, Zantel kwa kushirikiana na Baraza kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) walizindua huduma mpya ya “Zantel Madrasa” inayolenga kutoa mafundisho ya dini na kuwaunganisha wadau wa dini hiyo kujifunza zaidi juu ya uislamu kwa kupitia simu zao za mikononi au kujipatia jumbe mbalimbali na mawaidha ya kiislamu kwa kutuma ujumbe mfupi wa maneno kwenda namba 15586.

0 maoni:

Chapisha Maoni