Posted by Esta Malibiche on MARCH 27,2017 IN NEWS
HALMASHAURI ya Manispaa ya Iringa,
mkoani Iringa imetoa mkopo kwa vikundi 35 vya wanawake na vijana ikiwa ni
utekeleza wa agizo la serikali la kutenga asilimia kumi (10%) ya mapato ya
ndani kwa ajili ya kutoa mikopo kwa vijana na wanawake.
Akikabidhi hundi yenye
thamani ya shilingi milioni 70,000,000/- kwa vikundi hivyo katika awamu ya pili
ya kipindi cha mwaka 2016/2017, Mstahiki Meya wa Manispaa ya Iringa, Alex Kimbe
amewataka kinamama na vijana kutumia fedha hizo kwa shughuli zilizokusudiwa ili
ziweze kuleta manufaa na kuwatoa katika lindi la umasikini.
Alisema mkopo huo umetolewa
kwa awamu ya pili, ambapo kwa awamu ya kwanza kipindi cha mwaka 2016/2017
Halmashauri ya Manispaa ya Iringa ilitoa kiasi cha shilingi milioni
70,147,000/- kutoka mapato ya ndani kwa vikundi 35 vya wanawake na vijana.
Aidha, jumla ya 647,000/- zilitumika
kwa ajili ya kuwajengea uwezo viongozi wa vikundi vilivyokopeshwa, ambapo
vikundi 18 vya vijana na vikundi 17 vya wanawake vilinufaika.
Kwa upande wake Kaimu Ofisa Maendeleo ya Jamii
Manispaa ya Iringa, Eliah Kasanga alisema kuwa ofisi yake kwa kushirikiana na
watendaji wa kata wameendelea kufanya ufautiaji kwa vikundi vilivyokopeshwa, na
mpaka Januari, 2017 jumla ya 39,788,000/- zimerejeshwa na ufualiaji unaendelea.
Kasanga alisema Halmashauri ya Manispaa
ya Iringa imekuwa ikitekeleza agizo la serikali la kutenga asilimia kumi ya
mapato ya ndani kwa ajili ya kutoa mikopo kwa vikundi vya wanawake na vijana.
'''Kuanzia mwaka 2012/2013
mpaka 2016/2017 kiasi cha shilingi 175,100,000/- zimenufaisha walengwa 1,243 wa
vikundi vya wanawake na vijanaalisema Kasanga'''
Nae Mratibu wa Mikopo
ya Vijana Manispaa ya Iringa, Maria Sangana alisema mfuko huo umekuwa
ukikabiriwa na changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na vikundi kutorejesha
fedha walizokopeshwa kwa wakati.
Sangana alisema kuwa hali hii imekuwa
ikichelewesha utoaji wa mikopo kwa vikundi vingine na kuongeza kuwa baadhi ya
vikundi kutotumia fedha kwa shughuli walizopanga wakati wa kuomba mkopo.
''Katika kukabiliana na
changamoto hizo ofisi ya maendeleo ya jamii katika Halmashauri ya Manispaa ya
Iringa imeeandaa mfumo wa ufuatilaji wa marejesho ya fedha za mfuko huo, pamoja
na kuendelea kutoa elimu ya stadi za kazi na ujasiliamali kwa kivundi vya
ujasiliamali'''Alisema Sangana.
0 maoni:
Chapisha Maoni