Posted by Esta Malibiche on MARCH 27,2017 IN NEWS
Kamati ya Kudumu ya Bunge Hesabu za
Serikali za Mitaa (LAAC)imewaagiza watendaji wa Manispaa ya Iringa kuhakikisha
wanasimamia miradi ya Maendeleo ili iweze kukamilika kwa wakati na kwa kiwango cha ubora unaotakiwa.
Kauli hiyo imetokea baada ya Kamati hiyo kutetembelea miradi mbalimbali iliyopo Manispaa ya Iringa ukiwemo mradi wa maji, barabara na machinjio ya kisasa,ambapo mradi huo umechukua muda mrefu zaidi ya miaka kumi bila kukamilika,hali iliyoishangaza kamati hiyo na hatimae kutoa agizo kwa manispaa.
Akizungumza wakati wa majumuisho ya
ziara ya siku moja ya kamati hiyo kwenye ukumbi wa Manispaa ya Iringa Makamu Mwenyekiti
wa kamati hiyo Abdallah Chikota alitoa maelekezo kwa Manispaa kusimamia miradi na kuhakikisha inatekelezwa
kwa wakati na kwa kiwango kinachotakiwa.
Akizungumzia uboreshaji wa Miundombinu
ya barabara alisema kuwa Manispaa ya Iringa imeelekeza nguvu kubwa katikati ya mji
na kusahau barabara za pembezo ambazo zitasaidai kutoa huduma kwa wananchi.
Chikota alisema kuwa barabara hizo
hazina viwango vinavyotakiwa pamoja na
kukamilika ujenzi wake,ikiwemo alama za barabarani na vivuko vya watembelea kwa
miguu,hali inayosababisha kutokuwa rafiki kwa mwananchi.
Kamati ya Kudumu ya Bunge za Hesabu
za Serikali za Mitaa ilitembelea barabara za Mkimbizi- kihesa Sokoni-Chuo kikuu
cha Iringa na Ngome na kukuta barabara hizo hazina vivuko ambavyo vinaweza kwa
kuwarahisishia wananchi kufika kwa urahisa katika makazi yao.
Mradi wa ujenzi wa barabara
unajumuisha vipande vitatu vya barabara za Mkimbizi TBA (1.10km), Kihesa Sokoni-University
of Iringa (zamani Tumaini University (0.70km) na Ngome–Mwang’ingo (0.45km)
uliyobuniwa ili kuinua kiwango cha barabara hizi kutoka changarawe hadi kiwango
cha lami.
‘’’’Kuna tofauti kubwa kati ya
wananchi waishio pembezoni na katikakti. Barabara za pembezoni mwa mji hazina
kiwamgo vya ubora…,” alisema Chikota.
Awali kitoa taarifa kwa kamati hiyo,
Mhandishi wa Ujenzi wa Manispaa ya Iringa, Mashaka Luhamba alisema kuwa mradi
huo ulianza kutekeleza tarehe 1/11/2013 na uilikamilika tarehe 18/09/2014.Alisema
kazi hiyo ilitekelezwa na Mkandarasi G’S Contractors kwa mkataba wa gharama ya
1,088,505,000/-.
Luhamba alisema kuwa kazi hiyo
ililenga na pia kupunguza kero kwa wananchi wa eneo la mkimbizi ambalo halina
barabara ya uhakika na lina wakazi wengi.
Kwa upande wake Katibu Tawala wa
Mkoa wa Iringa, Wamoja Ayubu alisema amepokea maagizo hayo kutoka kamati ya
kudumu ya bunge za hesabu za serikali za mitaa (LAAC)na kuahidi kuyafanya kazi
mapendekezo hayo.
Wamoja alisema kuwa kupitia sekretarieti
ya mkoa atahakikisha wanasimia utekelekezaji wa maagizoyote yalitotolewa na
kamati hiyo kwa manispaa ya Iringa na kuhakikisha yanatekelezwa ipasavyo.
Halmashauri ya Manispaa ilifanya
matengenezo ya barabara hizi kwa kiwango cha lami kwa kutumia fedha za mfuko wa
barabara (Road Fund) kwa bajeti ya mwaka 2013/2014 ambazo zilivuka mwaka.
0 maoni:
Chapisha Maoni