Posted by Esta Malibiche on MARCH 9,2017 IN NEWS
Na Esta Malibiche
Iringa.
Wakazi mkoani hapa wameshauriwa kujenga utamaduni wa kununua hisa
kutoka katika makapuni mbalimbali ili kuwa sehemu ya wanufaika wa faida
zitokanazona biashara inayofanywa na makampumi hayo.
Akizungumza kwenye mkutano ulioandaliwa na Kampuni
Chambe ya Wafanyabiashara wa Viwanda na Wakulima Pubalic Investment
Campany (TCCIA PLC) mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi Injiani Alois
Mwamanga alisema watu wengi waliopiga hatua kimaendeleo duniani ni
wale walionunua hisa katika kampuni mbalimbali.
Alisema hapoa nchini elimu ya watu juu ya umuhimu wa kununua hisa
ni ndogo na ndioa sababu kampuni hiyo imepita katika mikoa mbalimbali ikiwamo
Iringa kuhamasisha watu kununua hisa.
“Suala la kununua hisa kwa hapa nchini ni geni,watu wetu hawana
utamaduni huo lakini ukweli ni kwamba hii ni fursa pekee ya mtanzania wa
kawaaida kuwekeza kwenye uchumi”alisema Mwamanga na kuongeza:
“Hatua hii itawawezesha wananchi kupata gawio takribani kila mwaka
nah ii itawezesha wananchi wengi kuondokana na umasikini unaokabili taifa
kwa sasa.
Alitolea mfano watalii wanaotka nchi z aulaya kuja kutembelea
nchini kuwa wengi wao wamewekeza katika kununua hisa kwenye kampuni mbalimbali
na hutumia fedha zitokanazo na gawio kufanya safari katika nchi mbalimbali.
Mwamanga alisema zipo faida za kudumu kwa mtu anayenunua hisa
kwakuwa anapata fursa ya kupata gawio litokanalo na faida iliyopatikana kwenye
kampuni hiyo kila mwaka jambo ambalo linaweza kuwafanya waaondokani na
umasikini.
Alisesma lengo la kukutana na wafanyabiashara pamoja na wakazi wa
mkoa wa Iringa ni kuwahamasisha ili kujenga utamaduni wa kununua hisa
zikiwamo hisa 112.5 milioni zinazouzwa na Kampuni ya TCCIA PLC.
Kwa upande wake Judith Ndawi ambaye alishiriki mkutano huo
alisema ni muhimu wsatu kununua hisa ili kukabiliana na changamoto z auchumi wa
sasa.
“Mimi ninamfano mme wangu amewekeza kwenye Kampuni ya Bahaco
lakini kila mmoja anapata mgao,tupo sisi na watoto wetu wane katika familia na
wote tunapata mgao katika Akaunti zetu mimi nimefarijika sana ninawashauri
wananchi wengine kununua hisa”alisema Ndawi.
Afisa Mtendaji wa TCCIA Mkoa wa Iringa James Sizya alisema mkutano
huo uliandaliwa na TCCIA PLC lengo likiwa kutoa elimu ya umuhimu wa
wananchi kununua hisa katika kampuni hiyo na kampuni mbalimbali ili kuwa sehemu
ya uwekezaji katika kampuni mbalimbali.
Aliwataka wananchi hao kujitokez akununua hisa hizo kwa kuwaa
lengo la kampuni hiyo ni kuwajenga wananchi kiuchumi na kuwawezesha kumdu
gharama za maisha ya sasa na baadae.
0 maoni:
Chapisha Maoni