Posted by Esta Malibiche on MARCH 2,2017 IN NEWS
Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akiwa tayari kwa uzinduzi
wa Ripoti ya hali ya ndoa za utotoni Nchini.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akionesha Ripoti ya hali ya ndoa za utotoni Nchini.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akionesha Ripoti ya hali ya ndoa za utotoni Nchini.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akiwa na viongozi wa dini
katika picha ya pamoja mara baada ya kuzindua Ripoti ya hali ya ndoa za
utotoni Nchini
……………………………………………………………………..
Na Anthony Ishengoma
Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Ally Mwalimu ameagiza walimu wakuu
wote wa shule za msingi chini kutekeleza marekebisho ya sheria ya elimu
ya mwaka 2016 kwa vitendo kwa kuwataka kuwasilisha taarifa za wasichana
waliopata mimba shuleni kwa kila kamishina wa elimu kama ilivyo agizo la
sheria hiyo.
Aidha amewaagiza watendaji wa
Wizara yake kufuatilia taarifa za wanafunzi wakike walioacha shule
kutoka kwa kila Afisa Maendeleo wa Jamii katika ngazi ya Wilaya
kuwapatia mrejesho wa kina kuhusu agizo lake kwa walimu wakuu kama hatua
muhimu ya kutekeleza agizo la sheria ya elimu kama ilivyofanyiwa
marekebisho na bunge mwaka 2016.
Amesema hayo katika hotuba yake
ya ufunguzi wa ripoti ya hali ya mimba za utotoni hapa nchini
iliyofanyika kote nchini chini ya mtandao wa mashirika yasiyo kuwa ya
kiserikali ikiongozwa na shirika la Jukwaa la Utu wa Mtoto Tanzania,
ufunguzi huo umefanyika leo jijini Dar es Salaam.
Waziri Ummy amewambia wajumbe
walioshiriki ufunguzi huo kuwa kwa kuwa mabadiliko ya sheria ya ndoa
hususani kifungu namba kumi na tatu cha sheria ya ndoa ya mwaka 1971
hayajafanyika ni bora kwenda mbele zaidi kutekeleza sheria ya elimu kama
ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2016 ili kutekeleza kwa vitendo hatua
za kupinga ndoa za utotoni.
Amesema kuwa sheria ya ndoa ya
mwaka 1971 kimsingi inahalalisha uwepo wa vitendo vya ndoa za utotoni na
kuahidi kuwa ataendelea kupigania marekebisho katika ndoa hiyo mara
baada yakuwasiliana na waziri wa sheria na mambo ya katiba.
Katika kuhakikisha Serikali na
Mashirika yasiyo ya kiserikali yanapambana na tatizo la ndoa za utotoni
ameyataka mashirika hayo kuweka nguvu zake katika maeneo ya vijijini
kwani ofisi nyingi za mashirika hayo zimejikita maeneo ya mjini hasa
katika jiji la Dar es Salaam.
Aidha amehaidi kuwa serikali
itaboresha mazingira ya mtoto wa kike kusoma ikiwemo ujenzi bora wa vyoo
pamoja na uendelezaji wa sera rafiki na sheria kwa mtoto wa kike
kujipatia elimu bila vikwazo ikiwemo elimu ya Afya na uzazi ili mtoto wa
kike aweze kutambua thamani yake katika jamii na taifa kwa ujumla.
Ufunguzi huo umefanyika wakati
serikali na mashirika ya yasiyo ya kiserikali wakiendelea kuadhimisha
siku ya kimataifa ya wanawake ambayo kilele chake ni Machi 8, mawaka
huu.
0 maoni:
Chapisha Maoni