Posted by Esta Malibiche on NOV 28,2017 IN NEWS
Mamlaka
ya mafunzo ya ufundi VETA leo imekabidhi vyeti vya kuhitimu masomo ya
ufundi stadi kwa vijana 8 wa mkoa wa Dar es saalam baada ya kuhitimu
masomo yao ya ufundi wa umeme wa majumbani pamoja na ufundi wa simu mara
baada ya kumaliza kusoma kupitia aplikesheni ya VSOMO na kuhitimu
katika viwango vya VETA.
Akikabidhi
vyeti hivyo Mkurugenzi wa VETA Kanda ya Dar es saalam , Habibu Bukko
aliishukuru Airtel kwa ushirikiano wake na VETA kupitia Aplikesheni ya
VSOMO ambapo imekuwa ikifaidisha wanafunzi walioko mbali na vyuo vya
VETA kuweza kusoma VETA wakiwa popote, vilevile alipongeza vijana hao
kwa kutumia simu zao za mkonononi vyema na kuhitimu masomo ya ufundi
Alisema
jitihada hizi za Kufanikiwa kutoa Masomo ya Ufundi stadi kupitia
Aplikesheni ya VSOMO zinaenda sambamba na mikakati iliyojiwekea VETA na
serikali kwa ujumla katika kutanua wigo ili kutoa wa elimu ya Ufundi
stadi hata kwa jamii ambayo bado haifikiwa na miundombinu ya vyuo vya
VETA mahali walipo ili nao kuwawezesha kushiriki maendeleo ya jamii.
“Hadi
sasa tunao zaidi ya vijana takribani 54 waliohiti masomo yao kupitia
VSOMO na kukabithiwa vyeti vyao. “nawapongeza kwa dhati vijana hawa kwa
kuhitimu masomo yao leo. Pia tunao wanafunzi 25 wanasubiri kupangiwa
masomo ya Vitendo ili kuhitimu na kupata vyeti . Nitoe wito kwao
kujiandaa vyema kuingia kwenye mafunzo ya viyendo laikini pia kwa
watanzania hususani vijana kutumia fursa hii kujisomea masomo ya ufundi
kwa kupitia mfumo huu wa VSOMO wakiwa popote VETA itawahudumua” alisema
Bukko
Akitangaza
majina ya wanafunzi hao waliohitimu mafunzo hayo Mkuu wa chuo VETA
Kipawa, Eng Lucian Luteganya VSOMO nae alibainisha kuwa, mfumo wa kusoma
mafunzo ya ufundi kupitia mtandao umekuwa na tija kubwa na kuongeza
wigo kwa VETA kupokea maombi ya kutengeneza kozi maalum kulingana na
uhitaji wa wanaotaka kusoma kwa manufaa ya jamii zao. Tunachofanya leo
ni udhihirisho thabiti kuwa inawezekana kutumia mifumo mibadala katika
kutoa elimu na kufikia malengo tuliyojiwekea, tusiwe wangumu kwenda na
mabadiliko yanayoletwa na technologia kwani kwa kufanya hivyo tutazuia
fursa ya kufanya shughuli zetu kwa ufanisi.
Napenda
kuwataja wahitimu wanaomaliza leo na kutunukiwa vyeti vya VETA ni
Hamadan Salum, Elvis Mahenge Simon, Mohamed Ibrahim Mohamed, Sunday
Jabil, Avitus Paul, Ridhuwani Hamidu Muhimu, Eliud Mwaikamila na
Deogratius
Kwa
upande wake Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel, Bi Beatrice Singano
Mallya alisema “Airtel kupitia mradi wetu wa kusaidia jamii wa Airtel
FURSA Tunajisikia fahari kuona tunaleta mabadiliko katika jamii kwa
kupitia technoligia ya mtandao wa simu. Lengo letu ni kuiwezesha jamii
kujiinua kiuchumi na kuzifikia fursa mbalimbali zinazohitaji wao kuwa na
ueledi wa kutosha. Tunaamini VSOMO italeta mabadiliko katika sekta ya
elimu na kuchochea ongezeko na nguvukazi yenye uledi ili kukudhi
mahitaji ya soko la ajira na kujiajiri
Tunaahidi
kuendelea kushirikia na VETA na taasisi mbalimbali katika kuhakikisha
tunatumia techologia ya mawasiliano katika kutatua changamoto zao
mbalimbali na kuchangia katika kuboresha maisha ya jamii zinazotuzunguka
na uchumi wan chi kwa ujumla.
Mfumo
wa masomo kwa njia ya Mtandao VSOMO toka kuzinduliwa umekuwa na
mafanikio makubwa ambapo hadi sasa takwimu zinaonyesha zaidi ya vijana
33,000 tayari wamepakua application ya VSOMO kupitia simu zao za Androad
BURE, na wengine 9500 wamejiandikisha ili kujisoma kozi mbalimbali
zikiwemo za Huduma ya chakula na mbinu za kuhudumia wateja, Matengenezo
ya kompyuta, umeme wa viwandani, ufundi Bomba wa Majumbani, Umeme wa
magari. Vilevile Ufundi umeme wa manyumbani, Ufundi pikipiki, Ufundi wa
simu za mkononi, Ufundi Alluminium, Utaalamu wa maswala ya urembo
pamoja ma Ufundi wa kuchomea vyuma.
0 maoni:
Chapisha Maoni