Posted by Esta Malibiche,on Nov.15,2017 IN NEWS
Wazazi
hususa ambao ni jamii ya kimasai wametakiwa kuachana na zana ya kuwatenga na
kutowapeleka shule watoto wa kike na wale ambao ni walemavu badala yake
wawapeleke mashuleni kwani wao ndio viongozi wa baadae
Hayo
yamebainishwa na mbunge wa viti maalumu kupitia chama cha mapinduzi
(CCM) Amina Mollel wakati alipokuwa akizungumza kama mgeni rasmi katika
sherehe za kupandisha ngazi rika kutoka katika rika la kurianga kuingia katika rika la Nyangulo ,sherehe ambazo zilifanyika katika Kijiji cha Oldenderet Kata ya Nduruma mkoani Arusha
Alisema
kuwa kunabaadhi ya wazazi wamekuwa wakiwaficha watoto wao kisa ni
walemavu jambo ambalo linawakosesha haki zao ikiwemo ya kupata elimu
kutokana na kufichwa huko
“kwakweli
wazazi wanavyoficha watoto wao hususa ni walemavu wanawanyima haki yao
mfano kama mimi ningefichwa leo kweli ndugu zangu ningeweza kuwa
kiongozi hivyo napenda kuwasihi wazazi wasiwafiche watoto hawa kwani
wakiwapeleka shule kupata elimu itakuwa vizuri kwani pale watakapo
maliza shule wanakuja kuwasaidia “alisema Amina
Aidha
pia aliwataka wazazi hawa wa jamii ya kimasai na hata wale wa makabila
mengine kuacha kuwaozesha watoto wakike mapema kwani watoto hao wakike
nao wanahaki ya kupata elimu kwani elimu ni bure ,kuanzia ngazi ya
msingi hadi sekondari hivyo ni vyema kama wazazi wakawasimamia watoto
hususa ni wakike wakaenda shule
Aliongeza
kwa kuwasihihi watoto wa kike kuweka kipaumbele swala la elimu kwani
elimu ndio kila kitu katika maisha yao na iwapo watasoma kwa bidii
wanaweza kuwa viongozi wakubwa wa serikalini hapo baadae
Alisema
kuwa kunabaadhi ya watoto wa kike wamekuwa wanaacha kusoma kisa
wanakimbilia maisha kitu ambacho sio kizuri kwani wanaweza kukimbilia
maisha yakawapiga hivyo ni muhimu sana kama watasoma kwanza alafu maisha
watayapata baadae baada ya kumaliza kusoma na kupata kazi zao nzuri
mbunge akiwa na wananchi waliouthuria katika sherehe hizo
mbunge wa viti maalumu CCM Amina Mollel akiwa anasalimia na moja na mzee aliekuwa rrika la kurianga ambae kwa sasa ameingia katika rika la Nyangulo
0 maoni:
Chapisha Maoni