Jumanne, 21 Novemba 2017

JOSEPH MWAGALA;WAZAZI HAKIKISHENI WATOTO WA KIKE WANAPATA ELIMU

Posted by Esta Malibiche on NOV.21,2017 IN NEWS

Na Esta Malibiche
MUFINDI
WAZAZI Wametakiwa kuona umuhimu katika Elimu kwa kuwasomesha watoto wa kike ili waweze kutimiza ndoto zao.
Akizungumza jana katika mahafari ya pili ya shule ya sekondari ya wasichana ya Regina Pacis inayomilikiwa na kanisa katoliki parokia ya kibao jimbo katoliki la Iringa,Josephat Mwagala alisema kuwa kumekuwa na fikra potofu kuwa kumsomesha mtoto wa kike ni kupoteza rasilimali fedha kwani maisha ya sasa bila elimu ni changamoto kubwa kwa mtoto wa kike.

Mwagala alisema kuwa mtoto wa kike akipatiwa elimu kuna uwezekano mkubwa kwa taifa kuwa na maendeleo kutokana na kuwajibika kwao katika maisha ya kila siku hivyo wazazi na walezi ni muhimu kuwasomesha watoto wa kike kwa lengo la kuendeleza ndoto walizonazo.

"Ili kiwango cha ufahuru kiweze kuongezeka nchini walimu wanapaswakuwa na mbinu mbadala za ufundishaji na wanapaswa kufundidha kwa bidii." Alisema Mwagala.

Akijibu risala ya shule iliyosomwa na ....ambae ni Mhitimu wa kidato cha nne,na alitoa kiasi cha Tsh.300000\= kwa ajili ya walimu ikiwa ni pongezi kwa kazi nzuri wanayoifanya,aliahidi kukabidhi mifuko 100  ya saruji, na aliahidi kuchimba visima viwili vya maji vyenye thamani ya Tsh.3 Mill,kwa ajili ya matumizi ya wanafunzi.Pia aliongoza harambee ya ununuzi wa keki ambapo kiasi cha Tsh.700000 zilipatikana.
Hata hivyo aliipongeza shule ya sekondari hiyo kwa kuwa moja ya shule zinazofanya vizuri mkoani hapa kielimu na tabia kwani ni moja ya shule ambazo idara ya elimu haipati malalamiko ya mara kwa mara kutoka shuleni hapo.

Aidha aliwataka wahitimu hao kusoma mazingira ya maisha popote watakapokuwa na kuamua namna ya kujiajiri ili mradi isiwe shughuli zinazopingana na sheria na maadili ya kijamii, kama vile kuuza madawa ya kulevya, ukahaba, unyang'anyi na mambo mengine yanayofanana na hayo ambayo watajiingiza matatani na kuonekana wabaya.
‘Ninawaomba mkirudi nyumbani kwa muda huu mfupi wa kusubiri matokea,zinmgatieni maadili  mliyofundishwa mkiwa hapa shuleni,bado nyie ni wanafunzi hakikisheni  mnajiepusha na mambo yasiyofaa ambayo yanaweza kukatisha ndoto zenu za kuendelea na masomno ya juu.’’’Mwagala


Awali mkuu wa shule ya Wasichana Regina Pacis Marco Shayo akimkaribisha mgeni rasmi alisema kuwa uongozi wa shule hiyo umeweka mikakati mbalimbali inayoendelea kutekelezwa ikiwa nipamoja na ujenzi wa jengo la shule linaloendelea kujengwa,kuchimba visima vya maji ili maji yaweze kukidhi mahitaji ya wanafunzi.

Shayo aliwasihi wahitimu wayazingatie maadili waliyoyapata wakiwa shuleni hapo ili waweze kuepukana na vishawishi vitakavyoweza kukatiza ndoto zao na hatimae kuwaingiza katika mambo yasiyofaa katika jamii na Taifa kwa ujumla.

Kwa muda huu mtakaokuwa mnasubilia matokea ya kujiunga na kidato cha tanao,nyie bado ni wanafunzi,hivyo mnatakiwa mtulie msijiingize katika makundi ya kihuni ambayo yatawaharibu na hatimae kushindwa kuendelea na masomo ya juu’Alisema Shayo

 Kwa upande wao wahitimu kwa kupitia msoma risala iliyosomwa na Rehema Chang”a alisema kuwa shule hiyo ilianza mwaka 2012 ambayo imepiga hatua kubwa kitaaluma Pamoja na kwa kuongeza vyumba vya maradasa ambapo ujenzi wake umeshaanza na unatarajia kukamilika kivi karibuni Pamoja na kuongeza vitabu vya masomo,meza Pamoja na viti na imefanikiwa kuanzisha miradi mbalimbali kama duka la shule

‘’Ndugu mgeni rasmi, katika kipindi cha miaka 5 shule yetu imepiga hatua katika mambo mbalimbali likiwemo la kufanya vizuri katika mitihani ya kidato cha nne ambapo mwaka 2016  wahitimu wote walifahuru vizuri na kujiunga na masomo ya Elimu ya juu, Pamoja na kuongeza mashine za kupandishia maji kutoka katika visima hivyo kupunguza tatizo la Majikushiriki michezo katika ngazi mbalimbali kama wilaya,mkoa na Taifa kwaujumla. kuongeza vifaa vya kitaaluma kama vifa vya maabala ili kutoa fursa kwa wanafunzi wengi kujifunza kwa vitendo hasa masomo ya sayansi kwa lengo la kukuza ufaulu na kuongeza ujuzi katika masomo ya sayansi.’’Alisema Chang”a

Changa”a aliongeza kuwa Pamoja na mafanikio hayo lakini shule inakabiliwa na chanagamoto ikiwemo upungufu wa nyumba za walimu,uhaba wa chumba cha maktaba, upungufu wa visima vya maji ili kukidhi mahitaji ya wanafunzi.

Sebastiani Makilinda ni mmjoa wa wazazi ambae pia ni mwananchi wa kijiji cha Kibao,kata ya Mtwango,akimshukuru Mgeni rasmi kwa kuchangia mifuko ya saruji alimuomba kuwasaidia  kutatua kero ya ya maji kijijini hapo inayowakabili kwa muda mrefu.
Mkuu wa shule ya Sekondari ya Wasichana Regina Pacis Marco Shayo akizungumza katika mahafari ya 3 ya shule hiyo  inayomilikiwa na kanisa Katoliki Parokia ya kibao Jimbo katoliki la Iringa.

Mdau wa Elimu Josephat Mwagala akizungumza katika mahafari ya 3 ya shule ya sekondari ya wasichana ya Regina Pacis inayo,milikiwa na kanisa katoliki Parokia ya Kibao jimbo katoliki la Iringa.

Mdau wa Elimu Josephat Mwagala akizungumza katika mahafari ya 3 ya shule ya sekondari ya wasichana ya Regina Pacis inayo,milikiwa na kanisa katoliki Parokia ya Kibao jimbo katoliki la Iringa.


 
 
















 















0 maoni:

Chapisha Maoni