Jumatano, 8 Novemba 2017

GOODLUCK MDUGI AMEWATAKA WATANZANIA KUHAKIKISHA WANAYATUNZA MAZINGIRA

Posted by Esta Malibiche on Nov 8,2017 IN NEWS
 Goodluck Mdugi ambae ni mfamasia wa Manispaa ya Iringa,Mkoani Iringa,akizungumza na vyombo vya habari mapema leo hii katika kampeni ya kitaifa ya usafi wa Mazingira inayoendelea Mkoani hapa,yenye kauli mbiu isemayo"NIPO TAYARI"
Mdugi amewataka watanzania kuyatunza mazingira yanayowazunguka ili kujienpusha na magonjwa ya mlipuko.

 Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza amewahimiza wananchi mkoani Iringa kuhakikisha wanajenga vyoo bora na wanakuwa mabalozi wa kutunza  mazingira yanayowazungunguka ili kujiepusha na Magonjwabya Mlipuko.

Kauli hiyo ameitoa leo hii wakati akizungumza na blog hii ya "KALI YA HABARI" ambapo alisema kuwa kila mwananchi anapaswa kuwa balozi wa kuhamasisha mazingira yanakuwa safi.
Akizungumzia swala la ujenzi wa vyoo bora,alisema kila kaya inatakiwa kuwa na choo bora na si bora choo.
Ninaendelea kuzunguka kila wilaya kuhamasisha utunzaji wa mazingira na ujenzi wa vyoo bora katika hii kampeni ya kitaifa,ninawaomba wananchi tuitikie kwa pamoja kwa vitendo.Nitaendelea kukagua na pale itakapobainika kaya haina choo bora basi bendera nyekundu itafungwa ili kumhamasisha mwenye nyumba ujenzi wa choo bora"Alisema Masenza.















Maoni 1 :