Jumanne, 28 Novemba 2017

YANGA KUANZA NA JKU,SIMBA NA WABABE WA UGANDA ‘URA’ UFUNGUZI WA MICHUANO YA MAPINDUZI CUP 2018 VISIWANI ZANZIBAR

  Posted by Esta Malibiche on NOV 28,2017 IN MICHEZO

 hqdefault
Ratiba ya Michuano ya Kombe la Mapinduzi imetoka na inatarajiwa kuanza Januari 2,mwaka 2018 itakayounguruma Visiwani Zanzibar kwenye uwanja wa Amaan.
Ufunguzi rasmi wa Kombe la Mapinduzi 2018 utafanyika Desemba 30, mwaka huu kwa mechi mbili kuchezwa Uwanja wa Amaan, kwanza Zimamoto na Mlandege Saa 10:17 jioni na baadaye JKU na Shaba Saa 2:15 usiku.   
Vinara wa Ligi Kuu ya Tanzania bara Simba SC itafungua dimba na URA ya Uganda Januari 2, mwaka 2018 Uwanja wa Amaan, Zanzibar mchezo ambao utaanza Saa 2:15 usiku wakati Yanga wataanza na JKU ya Zanzibar Januari Mosi kwenye dimba hilo hilo majira ya saa 2:15 usiku
Mabingwa watetezi, Azam FC wataanza na Jamhuri katika mchezo utakaofanyika Uwanja wa Amaan pia Januari 2, utapigwa majira ya saa 10:15 uwanja wa Amaan
Simba imepangwa Kundi A pamoja na Azam FC, Jamhuri, Taifa ya Jang’ombe na URA ya Uganda, wakati Yanga imetupwa Kundi B pamoja na JKU, Mlandege, Zimamoto na Shaba.
Simba itamenyana na Azam FC Januari 6, ikitoka kukipiga na Taifa ya Jang’ombe Januari 4, kabla ya kumalizia mechi zake za Kundi A Januari 8 na Jamhuri.
Azam FC itacheza na Taifa ya Jang’ombe Januari 4 kuanzia Saa 10:15, kabla ya kumenyana na Simba na itahitimisha mechi zake za Kundi A kwa kuumana na URA Januari 8 Saa 10;15 pia jioni Uwanja wa Amaan.
Baada ya mechi na JKU, Yanga watarudi tena uwanjani Januari 3 kwa mchezo na Shaba, Januari 5 na Zimamoto kabla ya kukamilisha mechi zake za Kundi B kwa kumenyana na Mlandege Janauri 7 Uwanja wa Amaan.
Nusu Fainali zinatarajiwa kuchezwa Januari 10 na Fainali itakuwa Januari 13, mwaka 2018 Uwanja wa Amaan kuanzia Saa 2:15 usiku.

0 maoni:

Chapisha Maoni