Posted by Esta Malibiche on NOV.201,2017 IN NEWS
Afisa
Kilimo na Ufugaji wa kikosi cha 822 Jeshi la Kujenga Taifa (JKT)
Rwamkoma, Kapteni M. Kinana (kulia) akiongea na Ujumbe kutoka Benki ya
Kilimo (hawapo pichani) walipotembelea mradi huo uliopo wilayani Bunda.
Kushoto ni Msimamizi wa Mradi wa Ufugaji wa Samaki wa JKT Kiteule cha
Bulamba, Luteni Kelvin Gondo.
Bodi
ya Wakurugenzi ya Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB)
imetembelea mradi wa ufugaji wa vifaranga vya samaki unaotekelezwa na
kikosi cha 822 Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Rwamkoma wilaya ya Butiama
kupitia Kiteule chake cha Bulamba, wilayani Bunda.
Akizungumza
lengo la ziara hiyo, mkuu wa msafara huo ambaye ni Mwenyekiti wa Bodi
ya Wakurugenzi ya Benki hiyo, Bibi Rosebud Kurwijila amesema lengo kubwa
la kutembelea Mradi huo ni kujionea juhudi za serikali za kuchagiza
mapinduzi ya kilimo hasa katika tasnia ya ufugaji na uvuvi wa samaki
nchini.
Bibi
Kurwijila aliongeza kuwa tasnia ya ufugaji wa samaki kwa njia ya
vizimba ni mojawapo ya minyororo ya mwanzo inayopatiwa mikopo kwa ajili
ya uongezaji wa thamani mazao na mifugo mbalimbali hasa katika uongezaji
wa thamani wa ufugaji wa samaki nchini.
Aliongeza
kuwa Benki ya Kilimo imejipanga kuendeleza uongezaji wa thamani wa
Ufugaji wa Samaki na uvuvi nchini ili ziweze kuchangia ukuaji wa uchumi
nchini.
Mradi
huo wa ufugaji wa samaki unaotekelezwa na JKT Wilaya ya Bunda, Kiteule
cha Bulamba ulizinduliwa rasmi mwezi Novembea, 2014 kwa kupandikiza
vifaranga vya samaki katika vizimba ndani ya Ziwa Victoria.
Mradi
huo unatekelezwa kwa ushirikiano na wadau mbalimbali wakiwemo Economic
Social Research Foundation (ESRF) na Shirika la Maendeleo la Umoja wa
Mataifa (UNDP).
Ufugaji
wa samaki kwa kutumia teknolojia ya vizimba ndani ya Ziwa Victoria,
umekuwa maarufu zaidi katika nchi za Afrika Mashariki ikiwemo Uganda na
Kenya ambapo umepunguza kwa kiasi kikubwa uvuvi haramu katika fukwe za
ziwa hilo.
Maafisa
wa Jeshi la Kujenga Taifa wanaotekeleza Mradi wa Ufugaji wa Samaki kwa
Vizimba Kiteule cha Bulamba wakifuatilia mkutano wa pamoja kati ya JKT
na Ujumbe kutoka Benki ya Kilimo.
Mwenyekiti
wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB),
Bibi Rosebud Kurwijila (kulia) akizungumza wakati walipotembelea Mradi
wa Ufugaji wa Samaki kwa Vizimba Kiteule cha Bulamba uliopo wilaya ya
Bunda, Mkoani Mara. Kushoto ni Afisa Uvuvi wa wilaya ya Bunda, Bw.
Steven Ochieng’.
Mjumbe
wa Bodi ya Wakurugenzi wa TADB, Bw. Dome Malosha (kulia) akizungumza
wakati walipotembelea Mradi wa Ufugaji wa Samaki kwa Vizimba Kiteule cha
Bulamba uliopo wilaya ya Bunda, Mkoani Mara. Wengine pichani ni
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki hiyo, Bibi Rosebud Kurwijila
(kushoto) na Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi, Bw. Joseph Mutashubilwa
(katikati).
Afisa
Uvuvi wa wilaya ya Bunda, Bw. Steven Ochieng’ (kushoto) akichangia
wakati wa mazungumzo hayo. Anayemsikiliza ni Mwenyekiti wa Bodi ya
Wakurugenzi wa Benki hiyo, Bibi Rosebud Kurwijila (kulia).
Msimamizi
wa Mradi wa Ufugaji wa Samaki wa JKT Kiteule cha Bulamba, Luteni Kelvin
Gondo akitoa maelezo juu ya maendeleo ya ufugaji wa samaki katika hatua
mbalimbali.
0 maoni:
Chapisha Maoni