Posted by Esta Malibiche on NOV.20,2017 IN MICHEZO
Mshambuliaji
wa timu ya VodaStar, ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu wa Vodacom Tanzania
PLC, Ian Ferrao (wapili kulia)akishangilia goli baada ya kuifungia timu
yake wakati wa mchezo wakirafiki dhidi ya timu ya Nokia uliofanyika
katika uwanja wa Gymkhana jijini Dar es Salaam,VodaStar iliiadhibu Nokia
kwa magoli 8-1.
Wachezaji
wa timu ya VodaStar,wakiongozwa na Mkurugenzi mtendaji wa Vodacom
Tanzania PLC, Ian Ferrao (wapili kulia mwenye miwani) wakishangilia
kombe lao baada ya kuihadabisha timu ya Nokia kwa magoli 8-1 wakati wa
mchezo wakirafiki uliofanyika katika viwanja vya Gymkhana jijini Dar es
Salaam mwishoni mwa wiki.
Kikosi
cha timu ya VodaStar kilichoisambaratisha timu ya Nokia kwa magoli 8-1
wakati wa mechi yakirafiki wakiwa katika picha ya pamoja baada ya mechi
hiyo kuisha iliyofanyika katika viwanja vya Gymkhana jijini Dar es
Salaam mwishoni mwa wiki.
Mashabiki
watimu ya VodaStar, wakifurahia kombe lao baada ya timu yao kiichakaza
timu ya Nokia kwa magoli 8-1 wakati wamchezo wakirafiki uliofanyika
katika viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Vodacom Tanzania PLC, Ian Ferrao (kushoto) akimshuhudia
Mkurugenzi wa Nokia Tanzania,Martin Talbot ( kulia) akimvisha medali
nahodha wa timu ya VodaStar, Ngayama Matongo baada ya kuilaza timu hiyo
kwa magoli 8-1 wakati wa mechi yakirafiki uliofanyika katika viwanja
vya Gymkhana jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Mshambuliaji
wa timu ya VodaStar, Ian Ferrao ambaye pia ni Mkurugenzi mtendaji wa
Vodacom Tanzania PLC, (kushoto) akipongezwa na Mkurugenzi mtendaji wa
Nokia Tanzania, Martin Talbot kwa kuchaguliwa kuwa mchezaji bora wa
mchezo wakati wa mchezo wa kirafiki kati ya kampuni hizo ambapo
VodaStar iliichapa Nokia kwa magoli 8-1 mwishoni mwa wiki katika viwanja
vya Gymkhana jijini Dar es Salaam.
Nahodha
wa timu ya Nokia Tanzania,Charles Domingos(kulia) akiachia shuti kali
na kuifungia goli timu yake na lapekee wakati wa mechi yakirafiki
iliyofanyika katika viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam kati ya
timu yake na VodaStar ambapo VodaStar waliichakaza timu hiyo kwa magoli
8-1.
0 maoni:
Chapisha Maoni