Posted by Esta Malibiche on NOV.20,2017 IN SIASA
Kada wa chama cha mapinduzi (CCM) Albert Chalamila akiwa jukwaani na mgombea udiwani kupitia chama hicho Baraka Kimata katika uchaguzi mdogo wa kata ya Kitwiru manispaa ya Iringa
Kada wa chama cha mapinduzi (CCM) Albert Chalamila akiwa jukwaani na mgombea udiwani kupitia chama hicho
Baadhi
ya wananchi waliojitokeza kumsikiliza mgombea udiwani wa kata hiyo
Baraka Kimata akiwa jukwaani kuomba kura kwa wananchi wa kata hiyo.
MAKADA mbalimbali wa chama cha mapinduzi (CCM) Manispaa ya Iringa mkoani hapa,wamemtaka mgombea udiwani wa kata ya Kitwiru Baraka Kimata kufanya kazi kwa kujituma na kuhakikisha anawaletea maendeleo wananchi wa kata hiyo pindi atakapopewa ridhaa ya kuwaongoza.
Akiwahutubia wananchi wa kata ya Kitwiru mtaa wa wa Kitwiru Stand kada wa chama hicho Albert Chalamila alimtaka mgombea huyo kufanya kazi kwa uadilifu na kuhakikisha atatua kero za wananchi wa kata ya Kitwiru kwa ndio waliompa dhamana ya kuwa kiongozi katika eneo hilo.
“Leo
hii tunapanda kwenye majukwaa mbalimbali kukunadi kwa kutumia akili
zetu na nguvu zetu sasa ukishinda sio uanze kuwaletea kiburi wananchi wa
kata hii,hapo hatuta kuwa sawa kabisa hivyo nakuomba uwaheshi na
kuwatumikia vilivyo wananchi wa kata ya Kitwiru ukipewa ridhaa ya
kuwaongoza” alisema Chalamila
Chalamila
alisema kuwa wananchi wamekuwa wakijitokeza katika mikutano yako ya
kampeni kwa lengo la kutaka kujua hoja na ahadi zako juu ya kuleta
maendeleo ya kata hivyo unatakiwa kuthamini utu wao kwa kuwaletea
mandeleo na kutatua changamoto zinazowakabili.
“Wananchi
hawa wamekuja kwenye mkutano sio kwasasababu ya kuja kukushangaa
mkutano,sio wanansimama kwa ajili kwao hawana viti,wamekuja hapa bila
kupewa fedha kuja kukuona wewe bali wamekuja kukusikiliza hoja zako na
kuangalia jinsi gani watapata maendeleo hivyo ni lazima uje uwatumikie
vilivyo” alisema Chalamila
Chalamila
akaongeza kuwa wananchi wanaojitokeza kwenye mikutano ya chama cha
mapinduzi mtu anayegombea kupitia chama hicho huwa anakuwa ni
shupavu,Imara na muadilifu hivyo Baraka Kimata inatakuwa kuendelea
kuwapa ushirikiano wananchi hawa.
“Wananchi
wa Kitwiru wamejitolea kuja kwenye mikutano ya chama hiki na kuona kuwa
chama kimesiamamisha mtu ambaye anasifa za kuwa kiongozi wa kuleta
maendeleo kwa wananchi wake sasa ole wako uje uwageuge na uute mapembe
kama walio upande wa pili” alisema Chalamila
Aidha
Chalamila alimtaka Kimata kuacha kufanya kazi za wananchi kwa faida
yake na kuwasahau wananchi waliokuchagua kuwa diwani wa kata hivyo chama
cha mapinduzi hakiwezi kukuvumilia hata kidogo.
“Ukipewa
kura na wananchi hawa unatakiwa kuwa makini sana na ukijiunga na
magenge ya wahuni kwa kula rasilimali za taifa hili utalaaniwa nikwambia
kweli Kimata maana saizi umebatiwa upya hivyo unatakiwa kuwa muadilifu
ipasavyo” alisema Chalamila
Chalamila
alimalizia kwa kuwaomba wananchi wa kata ya Kitwiru kumpa kura nyingi
ili awe diwani wa kata hiyo kwa ajili ya maendeleo ya wananchi wa kata
hiyo.
“Jamani
naombeni mumpe kura za ndio Baraka Kimata kwa maendeleo ya kata na
mumnyime kura Yule mgombea mwingine kwa kuwa Kimata yupo katika chama
makini” alisema Chalamila
Kwa
upande wake Kimata alisema kuwa ameamua kugeuka kwa lengo la
kuhakikisha kuwa wananchi wa kata ya kitwiru wanapata maendeleo ndio
maana aliamua kugeuka.
Kimata
ameendelea kuwaomba wananchi wa kata ya Kitwiru kumpigia kura nyingi
siku ya tarehe ishirini na sita (26) mwezi huu ili awe diwani wa kata ya
hiyo.
0 maoni:
Chapisha Maoni