Posted by Esta Malibiche on Nov.5,2017 IN NEWS
NAIBU waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso amewataka wakandarasi wa maji hapa nchini kufanya kazi kwa bidii ili maji safi na salama yapatikane na kuweza kufikia azma ya serikali ya awamu ya tano ya kumtua mama ndoo ya maji kichwani kwa kuhakikisha maji mijini yanapatikana kwa asilimia 95 na vijijini asilimia 85 ifikapo 2020.
Maagizo
hayo ameyatoa jana Wilayani Bahi Mkoani Dodoma, wakati
akikagua chanzo cha maji cha Mkakatika,eneo la tanki la maji,kituo cha
kuchota maji cha wananchi kilichopo katoka mradi wa maji wa halmashauri
hiyo na mradi wa maji wa kijiji cha Mchito miradi ambayo kukamilika
kwake itaongeza upatikanaji wa maji hadi asilimia 48.73 kutoka asilimia
16 iliyopo sasa.
"Uhandisi
wa maji maana yake maji yapatikane, wananchi hawataki kusikia mambo ya
dizaini,upembuzi wala usanifu wanataka maji, fanyeni kazi watu wapate
maji na sio vinginevyo"" Alisema Aweso na kuongeza kuwa
"Ndugu
zanguni mi unaibu waziri bado nautaka hivyo sitokubali
kutumbuliwa,kabla sijatumbuliwa mimi nitakutumbua wewe timizeni majukumu
yenu,"alisisitiza Aweso
Alisema
serikali ina dhamira ya dhati ya kuhakikisha wilaya ya Bahi inapata
maji ambapo katika mwaka wa fedha wa 2017/2018 jumla ya shilingi
bilioni moja zimetengwa.
"Katika
kuhakikisha mkoa wa Dodoma unakuwa na maji ya uhakika tumeamua kutumia
bwawa la Farkwa kwa ajili ya kusambaza maji katika wilaya ya Chemba,Bahi
na Dodoma mjini,ndugu zangu unapobebwa kiuno kikaze,ukikilegeza
utaanguka,nawaomba mtunze miradi ya maji,"alisema Aweso.
ata
hivyo Naibu waziri amemtaka mkandarasi wa maji Deus Mchele kuhakikisha
ifikapo novemba 18 mwaka huu miradi yote ya maji iliyopo katika
majaribio iwe imekamilika na kukabidhiwa kwa wananchi na sambamba na
kuziba bomba linalovuja ambalo linapeleka maji kwenye tenki.
Akiwa
njiani kuelekea kijiji cha Mchito Aweso alisimamisha msafara wake
kijiji cha Bankolo na kuwasikiliza wananchi waliosimama kando ya
barabara ambapo alipokea changamoto ya ukosefu wa maji na kuahidi
kuondoa changamoto hiyo kama serikali ya awamu ya tano chini ya rais
John Magufuli ilivyoahidi.
Wakizungumza
baadhi ya wanachi Abeid Juma aliempongeza Rais Magufuli na serikali
yake kwa kuonyesha dhamira ya kutatua shida ya maji iliyokuwa inawafanya
waamke alfajiri na kulala usiku sana hali iliyoleta changamoto katika
ndoa zao.
Kwa
upande wake makamu mwenyekiti wa halmashauri hiyo Sosthenes Mpandu
alimshukuru naibu waziri kwa ziara yake inayolenga kutatua tatizo la
maji ambapo kwa sasa wananchi wa Bahi wananunua dumu moja shilingi mia
tano hadi mia sita.
"Mh
Aweso ziara yako imeleta manufaa,umetuonyesha na kudhihirisha kuwa rais
hakufanya makosa katika kukuteua unaendana na kauli mbiu yake ya hapa
kazi tu,,tunashukuru na kukuomba tena utukumbuke wilaya ya Bahi,"alisema
makamu mwenyekiti.
Mhandisi wa Maji wa wilaya ya Bahi Deus Mchele akitoa maelezo ya mradi wa kijiji cha Mchito mbele ya naibu waziri wa maji na umwagiliaji Jumaa Aweso. |
0 maoni:
Chapisha Maoni