Posted by Esta Malibiche on NOV30,2017 IN NEWS
Na Esta Malibiche
Mufindi
Mkoa wa Iringa kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo na wawekezaji wanatarajia kuanza kutekeleza sera ya uchumi wa viwanda kwa kuanzisha viwanda mbalimbali ndani ya Mkoa wa Iringa,hivyo kutekeleza agizo la serikali.
Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa Amina Masenza wakati wa ufunguzi wa sehemu ya upanuzi wa kiwanda cha Chai cha Unilever kilichopo eneo la Kilima kata ya Kibao wilayani Mufindi,Mkuu wa wilaya ya Mufindi Jamhuri alisema mkoa wa Iringa umeanza utekelezaji wake wa agizo la Serikali lililotolewa na Waziri wa Tamisemi Suleiman Jafo kuwa kila mkoa uhakikishe unakuwa na viwanda 100.
"Jumla ya viwanda 100 vinavyotakiwa katika mkoa wetu wa Iringa,Wilaya ya Mufindi inatakiwa kuwa na viwanda 35,hivyo tumejipanga kuhakikisha kuhakikisha tunafikia lengo"Alisema Jamhuri.
Alisema upanuzi wa kiwanda hicho ni makubaloano baina ya Unilever na Serikali ya Jamhuri ya Muunga wa Tanzania kuhusu utekelezaji wa maboresho ya viwanda vya chai ili kuzalisha bidhaa zenye kukidhi haja kwa watumiaji.
Aidha Jamhuri aliwataka wawekezaji wengine kujitokeza kuwekeza Mkoani hapa ili kutekeleza Agizo la Serikali kupitia waziri wa Tamisemi Suleiman Jaffo alilolitoa kuwa kila Mkoa unatakiwa kuwa na viwanda 100.
‘Serikali imekuwa ikihamasisha kuhusu ujenzi wa viwanda nchini,hivyo kila mmoja wetu anapaswa kuwekeza katika viwanda vitavyozalisha na kuchakata mazao yanayolimwa na wakulima wetu hivyo kuongeza pato la Taifa.’Alisisitiza Jamhuri.
Naye mkurugenzi mtendaji wa kiwanda cha chai cha Unilever kilichopo wilayani Mufindi Bw. Ashton Eastman amesema upanuzi wa kiwanda hicho umegharimu kiasi cha Tsh.5 bill,hivyo wanatarajia kuendelea maboresho ya viwanda vyao ikiwemo kiwanda cha Chai cha mkoani Njombe.
Eastman alisema lengo la kupanua kiwanda hicho ni kutaka kukidhi mahitaji ya wakulima wa chai pamoja na kuongeza fursa kwa watanzania.
"Tunaendelea kuboresha taratibu zetu za uwekezaji,hivyo kwa kupitia kiwanda hiki wakulima wa chai watanufaika kwa kuuza mazoa yao pia zaidi ya vijana elfu tatu wa kitanzania wamepata ajira" Alisema Eastman
0 maoni:
Chapisha Maoni