Posted by Esta Malibiche on NOV 20,2017 IN NEWS
Mgeni
Rasmi Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mh Mama Sophia Mjema Akizungumza
Machache wakati wa Mahafali ya kwanza ya Chuo cha Manjano Beauty
Academy .Ambapo amewataka Wanawake Kuchangamkia Fursa ya Urembo kwa kuwa
ukuaji wake kwa sasa ni kubwa na inakabiliwa na Upungufu wa Wataalamu
hivyo akiwashauri wanawake wengi Kujiunga na Kuiga Mambo Mazuri
Yanayofanywa na Chuo cha Manjano Beauty Academy.Akieleza zaidi Alisema
Sekta ya Urembo ina Fursa kubwa kwa Ajira kwa sasa,Katika Mahafali hayo
Wahitimu 120 Wametunukiwa vyeti katika katika nyanja ya urembo.
Chuo
cha Manjano Beauty Academy kimetunuku Astashahada (Certificates) na
Stashahada (Diploma) kwa wahitimu 120 wa kwanza wa chuo hicho katika
nyanja ya urembo na utengenezaji wa nywele.Urembo
na mitindo ni moja kati ya sekta zinazoajiri mamilioni ya wanawake kwa
sasa, lakini bado sekta hiyo imeendelea kuwa isiyo rasmi.
Wanawake
wengi wanaofanya kazi kwenye saluni hawana utaalamu, lakini ndiyo
wanaofuatwa na wanaume na wanawake kwa ajili ya kutengenezwa mionekano
inayovutia, wanaishi kwa kufanya kazi kubahatisha.
Akizungumza
kwenye mahafali ya kwanza ya Manjano Beauty Academy iliyofanyika
jijini Dar es Salaam, mwanzilishi wa Manjano Beauty Academy, Shekha
Nasser alisema kuwa maono hayo ndiyo yaliyosababisha yeye kuanzisha
Manjano Beauty Academy.Manjano Beauty Academy ni shule kwa ajili ya afya
na urembo ambayo ina lengo la kuwawezesha wasichana wa Kitanzania.
“Tunashauri,
tunatoa mafunzo na kuwaandaa wanafunzi kwa ajili ya soko kwa kuwapatia
ujuzi unaohitajika. Serikali haiwezi kuwaajiri wahitimu wote, hata sekta
binafsi haiwezi kwa hivi sasa, kwa hiyo mafunzo haya yanawasaidia
wasichana wadogo kuweza kujitengenezea soko kwenye sekta ya urembo,”
alisema Shekha.Kwa
mujibu wa Shekha, wasichana hao wamekuwa wakipewa mafunzo na wakufunzi
bora wanaopatikana katika sekta ya urembo ambayo yatawatasaidia wao
kutimiza malengo yao binafsi pamoja na malengo ya kitaasisi.
“Naamini
kuwa wahitimu hawa watabadilisha sekta ya urembo hapa nchini, kama
Korea na Filipino wanavyotambulika ulimwenguni kwa kuwa na bidhaa bora
za ngozi na wataalam wa matibabu wenye weledi, huko mbeleni Tanzania
itajulikana ni nchi inayotoa bidhaa bora za urembo kwa ngozi za
Kiafrika, kuanzia bidhaa za urembo wa uso zinazozalishwa kutokana na
Mwani wa baharini toka Zanzibar mpaka bidhaa za poda ambazo zina
virutubisho vya Manjano ya asili na vyakutosha,” alisema Shekha ambaye
pia ni mwanzilishi wa Shear Illusions.
Mwaka
2015, kupitia bidhaa za LuvTouch Manjano, Shekha alizindua kampeni
inayoitwa Manjano Dream Makers iliyokuwa na lengo la kuwawezesha
wasichana wenye mafunzo ya kijasiriamali kujikwamua kiuchumi ili
kutimiza ndoto zao.
“Katika
miaka miwili tangu kuanzishwa kwa taasisi ya Manjano, mtandao wa
wanawake wa Manjano Dream-Makers umeweza kuenea katika majiji na miji
Saba nchini na kuwasaidia kutengeneza ajira na kutengeneza kipato kwa
kuuza bidhaa zao kupitia mfumo wa nyumba kwa nyumba kwa wanawake wasio
na ajira,” alisema Shekha.
Mwanzilishi
wa Chuo cha Manjano Beauty Academy Mama Shekha Nasser Akitoa Hotuba
yake wakati wa mahafali ya kwanza ya chuo hicho yaliofanyika
Kwenye Viwanja vya Kijiji cha Makumbusho Jijini Dar es salaam.Mama
Shekha Nasser Amewashukuru wazazi na walezi kwa kuwapeleka Watoto wao
kwenye chuo hicho kwa LengoKupata Ujuzi wa Maswala ya Urembo,Aidha
Ametaja Changamoto kubwa Alizokabiliana nazo wakati anaanzishi Chuo
hicho Ikiwemo ukosefu wa Wataalamu wazawa wa Maswala ya Urembo.
Mgeni
Rasmi Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mh Mama Sophia Mjema Akiwa na Wageni
Waalikwa wakati wa Mahafali ya Kwanza ya Chuo cha Manjano Beauty
Academy
Baadhi
ya Wahitimu waliotunukiwa kwenye Mahafali ya Kwanza ya Chuo cha
Manjano Beauty Academy yaliofanyika Kwenye Viwanja vya Kijiji cha
Makumbusho Jijini Dar es salaam
Mshauri wa Maswala ya Kisaikolojia Anti Sadaka Akitoa Neno la Shukrani kwenye Mahafali hayo
Mgeni
Rasmi Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mh Mama Sophia Mjema Akitoa Cheti kwa
Mmoja wa Wahitimu Kwenye Mahafali ya kwanza ya Chuo cha Manjano Beauty
Academy..
Mgeni Rasmi,Uongozi wa Chuo cha Manjano Bauty Academy ,Wageni waalikwa na Wahitimu Wakiwa katika Picha ya Pamoja
Aliongeza
kuwa, “Leo tunajivunia kuwa na wasichana 360 katika mtandao wa ‘Manjano
Dream-Makers’ wenye matumaini ya kuboresha maisha yao na familia zao
kwa kuuza bidhaa za LuvTouch Manjano.
0 maoni:
Chapisha Maoni