Posted by Esta Malibiche on NOV.20,2017 IN SIASA
Aliyewahi kuwa Naibu katibu mkuu Chama cha Mapinduzi ccm Taifa,Mwigulu Lameck Nchemba,ambae pia ni WAZIRI wa Mambo ya Ndani, Dk Mwigulu
Nchemba amevitabiria mabaya vyama vya upinzani hapa nchini, akisema vimeanza kufa
polepole.
Nchemba aliyasema hayo jana wakati
akimnadi mgombea mgombea udiwani wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wa kata ya Kimala
wilayani Kilolo mkoani Iringa, Amoni Kikoti.
“Kubaki upinzani sasa ni kupoteza muda,
nazunguka sana mikoani, wananchi wanamuelewa sana Rais Magufuli, wananchi
wanajua dhamira ya serikali na wanauona mwanga mkubwa wa maendeleo” alisema.
Wakati CCM imemsimamisha Kikoti kujaza
nafasi ya aliyekuwa diwani wa kata hiyo Mejusi Mgeveke (CCM) aliyefariki dunia
mapema mwaka huu, Chadema imemsimamisha Tumson
Kisoma.
“Wewe
ndiye utakayekuwa mgeni wangu wa kwanza wa kikao kijacho cha bunge. Nataka uje
na shida mbalimbali za kata yako, nitakutambulisha kwa wadau mbalimbali
wakiwemo mawaziri ili wazichukue na kuzifanyia kazi,” alisema wakati akimnadi
mgombea huyo katika kijiji cha Kimala.
Dk Nchemba aliyesimama katika jukwaa la
kampeni hizo kama Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi
(CCM) alisema uchaguzi wa kata hiyo ni mwepesi kwa chama chake kwa kuwa
unalenga kujaza nafasi iliyokuwa ikishikiliwa na CCM.
“Nitashangaa sana kama suruali nyeusi
iliyotoboka itazibwa kwa kiraka cheupe, katika uchaguzi huu kuwapigia kura
wapinzani ni sawa na kupigia kura kivuli,” alisema.
Alisema watanzania wote wanajua serikali
iliyopo madarakni ni ya CCM, na sera na mipango inayotekelezwa inatokana na
Ilani ya CCM.
“Hatushindani kwa sera tena kwasababu
tulishindana 2015 na CCM ikaibuka kidedea, sasa hivi tunatekeleza. Maji,
barabara, huduma za afya, elimu, umeme na huduma zote muhimu zinaombwa na
wananchi kwa serikali ya CCM,” alisema.
Awali Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Kilolo
Kiliani Myenzi alimuomba Waziri Nchemba
kupeleka kilio chao cha miundombinu ya barabara serikalini ili kifanyiwe kazi.
“Zipo barabara ambazo kupita kwake ni
shida, lakini tunaomba kwa kiwango cha lami barabara ya kilometa 35 ya Iringa
Kilolo,” alisema.
Naye Mbunge wa Jimbo la Kilolo, Venance
Mwamoto aliwaambia wapiga kura wa kata hiyo wasiifunge kata hiyo na maendeleo.
“Chagueni mgombea mnayejua ana nafasi
nzuri ya kuwasiliana na Dk Magufuli, na huyo si mwingine zaidi ya mgombea wa
CCM,” alisema.
Akiomba kura kwa wapiga kura hao, Kikoti alisema anazifahamu changamoto za kata hiyo na yupo tayari kushirikiana na wananchi, serikali ya CCM na wadau wengine katika kuiletea maendeleo.
Kada wa chama cha Mapinduzi ccm wilayani kilolo,ambae pia ni mkuu wa wilaya ya Kilolo Asia Abdalah,akizungumza katika kampeni ya uchaguzi mdogo wa udiwani kata ya kimala wilayani kilolo. |
Wananchi wa kata ya Kimala wilayani kilolo wakiwa katika kampeni ya uchaguzi mdogo wa udiwani. |
0 maoni:
Chapisha Maoni