Posted by Esta Malibiche Nov.5,2017 in SIASA
Katibu wa chama cha mapinduzi CCM Mkoa wa Iringa, Christopher Magala,akimnadi Amos Kikoti ambae ni Mgombea wa udiwani kupitia chama cha Mapinduzi ccm kata ya Kimala wilayani Kilolo,katika uzinduzi wa kampeni ya uchaguzi mdogo wa udiwani . |
CHAMA cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kilolo Mkoani Iringa,kimezindua kampeni za uchaguzi mdogo wa udiwani katika kata ya Kimala, wilayani humo.
Akizungumza katika uzinduzi huo, Katibu wa chama cha mapinduzi CCM Mkoa wa Iringa, Christopher Magala aliwataka wapiga kura wa kata hiyo kujihadhari na matapeli wa kisiasa wanaobadili rangi za hoja zao kila kukicha.
“Kabla Rais Magufuli haijaingia madarakani hoja zao zilikuwa rushwa, ufisadi, ubadhilifu wa mali za umma na nyingine nyingi. Baada ya hayo yote kuanza kushughulikiwa katika awamu hii ya uongozi, wamebadilika na sasa wanatetea watu wanaojihusiha na vitendo hivyo, nchi haihitaji viongozi wa aina hiyo,” alisema.
Kwa upande wake Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa kupitia wilaya ya Mufindi, Jamuhuri William alisema; “sioni ni kwa namna gani, wananchi wa kata hii mtamchagua mgombea kutoka katika chama kilichoshindwa vibaya katika Uchaguzi Mku wa 2015.”
Naye kada wa chama cha Mapinduzi ccm, Asia Abdalla,ambae pia ni mkuu wa wilaya ya Kilolo mkoani hapa, alisema Kikoti atashinda kwa kishindo katika uchaguzi huo kwasababu wapiga kura wa kata hiyo wanajua mengi yaliyofanywa na yanayoendelea kufanywa na serikali ya Dk John Magufuli.
Asia alitaja miradi mbalimbali ya maendeleo ambayo serikali ya CCM imeitekeleza katika kipindi cha miaka miwili iliyopita na akasema mengi yanakuja ndani ya awamu ya kwanza ya serikali hiyo.
Akimuombea kura mgombea huyo, Mbunge wa Jimbo la Kilolo, Venance Mwamoto alisema; “Kikoti ana sifa za kuwa msaidizi wangu kwa kuwa ni mwadilifu, mwaminifu na mchapakazi, hivyo mchagueni yeye.”
Naye Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Iringa, Zainabu Mwamwindi alisema kata ya Kimala ni kata iliyoongozwa na CCM kwa miaka yote itakuwa miujiza kama watakengeuka.
Kwa upande wake Mgombea wa udiwani, Amoni Kikoti akiomba kura kwa wananchi hao, alisema atakuwa tayari kutembea kwa miguu kwenda kusikiliza kero mbalimbali za wananchi wa vijiji vya kata hiyo na kuziwasilisha katika mamlaka zinazohusika kwa utatuzi.
“Nitaanzia pale alipoishia diwani aliyetutangulia mbele za haki, nitafanya kazi kwa maarifa na juhudi zangu zote ili kero zilizopo katika kata hii zishughulikiwe ndani ya muda stahiki, uwezo huo ninao” alisema.
Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa kupitia wilaya ya Mufindi, Jamuhuri William akizungumza katika uzinduzi wa kampeni ya uchaguzi mdogo wa udiwani kata ya kimala wilayani kilolo,mkoani Iringa. |
0 maoni:
Chapisha Maoni