Posted by Esta Malibiche on NOV.20,2017 IN NEWS
Askari
Polisi wakishirikiana na ndugu wa Mwanafunzi aliyepotea Humphrey
Makundi wakifukua Kaburi ulimozikwa mwili wa mtu aliyeokotwa Mto Ghona
katika wilaya ya Moshi.
Na Dixon Busagaga wa Globu
ya Jamii Kanda ya Kaskazini.
UTATA
umeighubika familia ya Jackson Makundi ambayo kijana wake
aliyetambulika kwa jina la Humphrey Makundi,Mwanafunzi wa shule ya
Sekondari ya Scolastica iliyopo mji mdogo wa Himo kupotea katika
mazingira tatanishi.
Utata
wa kupotea kwa mwanafunzi huyo unatiliwa shaka zaidi na familia hiyo
baada ya kufukuliwa kwa kaburi ulimozikwa mwili uliookotwa mto Ghona
mita 300 ,jirani na shule hiyo ukidaiwa kushabihiana na wa mwanafunzi
huyo.
Humphrey
Makundi, mwanafunzi wa kidato cha pili katika shule ya sekondari ya
Scolastica anatajwa kupotea tangu Novemba 7 mwaka huu akiwa shuleni hapo
huku wanafunzi wenzake wakiendelea na mitihani ya kidato cha Pili ya
upimaji ya kitaifa .
Familia
ya kijana huyo yenye makazi yake mkoani Dodoma ikalazimika kutumia
mitandao ya kijamii kutoa taarifa za kupotea kwake ikidai mazingira ya
kutoweka kwake ni ya kutatanisha na baadae kuwasilisha taarifa katika
kituo cha Polisi cha Himo .
Kutokana
na kuwepo kwa taarifa za kuokotwa kwa mwili huo ,familia iliwasilisha
maombi katika mahakama ya Hakimu Mkazi, Moshi na mahakama ikaamuru
kufukuliwa kwa Kaburi hilo zoezi lililoanza majira ya saa 8:30 mchana na
kudumu kwa zaidi ya saa moja.
Jeshi
la Polisi liliongoza zoezi hilo katika makaburi ya Karanga huku
likishuhudiwa na ndugu wa mtoto aliyepotea ambapo baada ya mwili
kutolewa kaburini hali ya simanzi ilionekana katika nyuso za baadhi ya
ndugu wa Mwanafunzi huyo akiwemo baba mzazi wa kijana huyo.
Kamanda
wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro,Kamishna Msaidizi wa Polisi ,Hamis Issa
akathibitisha uwepo wa tukio hilo huku akieleza kuwa tayari jeshi la
Polisi linawashikilia wati 11 akiwemo mmiliki wa shule hiyo Edward Shayo
huku likifanya uchunguzi wa kina kuhusu matukio hayo mawili.
Mwili
uliofukuliwa katika makaburi ya Karanga upande wa marehemu wasiokuwa na
ndugu ulipelekewa katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya KCMC kwa
uchunguzi zaidi chini ya uangalizi wa jeshi la Polisi wakishirikiana na
madaktari kutoka KCMC.
Jeshi
la Polisi likiwa limezungushia utepe eneo ambalo kuna kaburi ulimozikwa
mwili ambao familia ya Mwanafunzi wa shule ya sekondari ya Scolastica
iliyopo mji mdogo wa Himo aliyepotea ,Humphrey Makundi ulitilia shaka.
Kaburi ulimozikwa mwili wa mtu aliyezikwa na Manispaa ya Moshi baada ya kuokotwa Mto Ghona jirani na ilipo shule ya Sekondari .
Kaburi likifukuliwa.
Baba
mzazi wa Mwanafunzi wa shule ya Sekondari ya Scolastica
aliyepotea,Jackson Makundi (Katkati) akijadili jambo na wanandugu wakati
zoezi la kufukua kaburi likiendelea.
Baba
mzazi wa Mwanafunzi Humphrey ,Jackson Makundi (Mwenye suti nyeupe)
akitizama mwili (haupo pichani) baada ya kaburi kufukuliwa.
Baba
mzazi wa Mwanafunzi Humphrey ,Jackson Makundi (Mwenye suti nyeupe)
akionekana akiwa amekaa chini baada ya kutizama mwili uliofukuliwa
katika kaburi .
Askari
Polisi na Wanandugu wa kijana aliyepotea wakijaribu kusaidia kumnyanyua
mzazi wa Mwanafunzi huyo kutoka katika eneo lilipo kaburi
lililofukuliwa .
Baba
mzazi wa Mwanafunzi Humphrey ,Jackson Makundi (Mwenye suti nyeupe)
akisindikizwa kutoka katika eneo la Makaburi ya Karanga katika manispaa
ya Moshi.
Mwili
uliofukuliwa katika makaburi hayo ukiwekwa katika gari la Polisi kwa
ajili ya kwenda kuhifadhiwa katika Hosptali ya Rufaa ya KCMC.
Gari la Polisi likiwa na mwili uliofukuliwa katika Makaburi ya Karanga.
0 maoni:
Chapisha Maoni