Jumatatu, 6 Novemba 2017

MAVUNDE AZITAKA SEKTA BINAFSI KUSHIRIKIANA NA SERIKALI KATIKA KUPUNGUZA UMASKINI NA VITA DHIDI YA RUSHWA

Posted by Esta Malibiche on Nov 6,2017 IN NEWS
Naibu waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu(Kazi,Vijana na Ajira) Mh Anthony P. Mavunde akizungumza  mkoani Arusha wakati wa kufungua kongamano la majadiliano juu ya utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu chini ya umoja wa Mataifa kupitia Global Compact Network(GCNT)
 Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu(Kazi,Vijana na Ajira) Mh Anthony P. Mavunde amezitaka sekta binafsi kushirikiana na Serikali katika kusaidia kutokomeza umaskini kwa wananchi pamoja na kuunga mkono jitahada za serikali ya awamu ya Tano za kupambana na Rushwa na Ufisadi.

Mavunde ameyasema hayo leo katika  Hotel ya Mount Meru Arusha wakati akifungua kongamano la majadiliano juu ya Utekekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu chini ya UMOJA WA MATAIFA kupitia Global Compact Network Tanzania (GCNT) ambapo amewahakikishia wadau hao juu ya ushirikishwaji wa sekta binafsi katika kusaidiana na serikali kutekeleza malengo ya maendeleo endelevu hasa katika maeneo ya Kutokomeza umaskini na Vita dhidi ya Rushwa na Ufisadi.

Kwa upande Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Tanzania Bw Alvaro Rodriguez akitoa akitoa salam zake,alimpongeza Mh Rais Dr John Pombe Joseph Magufuli na serikali yake kwa hatua za makusudi wanazochukua katika kupambana na Rushwa na Ufisadi hapa nchini Tanzania.

Awali Mwenyekiti wa GCNT Bw Patrick Ngowi akimkaribisha Mgeni rasmi alisema atahakikisha anatoa ushirikiano mkubwa ikiwa nipamoja  na kusaidiana na Serikali ili kwa pamoja waweze kutekeleza malengo hayo ya maendeleo endelevu kwa mustakabali wa maendeleo ya wananchi nchini Tanzania
Naibu waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu(Kazi,Vijana na Ajira) Mh Anthony P. Mavunde akizungumza  mkoani Arusha wakati wa kufungua kongamano la majadiliano juu ya utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu chini ya umoja wa Mataifa kupitia Global Compact Network(GCNT)

Naibu waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu(Kazi,Vijana na Ajira) Mh Anthony P. Mavunde akizungumza  mkoani Arusha wakati wa kufungua kongamano la majadiliano juu ya utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu chini ya umoja wa Mataifa kupitia Global Compact Network(GCNT)

Kongamano la majadiliano juu ya utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu chini ya umoja wa Mataifa kupitia Global Compact Network(GCNT) likiendelea.

Kongamano la majadiliano juu ya utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu chini ya umoja wa Mataifa kupitia Global Compact Network(GCNT) likiendelea.

0 maoni:

Chapisha Maoni