Jumanne, 28 Novemba 2017

MAKAMU WA RAIS AWASILI NAIROBI KUMWAKILISHA RAIS MAGUFULI KWENYE SHEREHE ZA KUAPISHWA RAIS UHURU KENYATTA LEO

Posted by Esta Malibiche on NOV 28,2017 IN NEWS

JO4A2302
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta Mjini Nairobi nchini Kenya ambako anamwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika sherehe za kuapishwa kwa Rais Mteule wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Uhuru Kenyatta zitakazofanyika katika uwanja wa Moi Kasarani Mjini Nairobi. Kushoto ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Suzan Kolimba, Balozi wa Kenya nchini Tanzania Mhe. Robinson Githae na Kulia ni Balozi wa Tanzania nchini Kenya Dkt. Pindi Hazara Chana.
JO4A2317
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akitia saini kitabu cha wageni katika chumba cha wageni mashuhuri katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta Mjini Nairobi nchini Kenya.
JO4A2305
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiongea na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Suzan Kolimba, na Balozi wa Kenya nchini Tanzania Mhe. Robinson Githae baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta Mjini Nairobi nchini Kenya asubuhi hii ambako anamwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika sherehe za kuapishwa kwa Rais Mteule wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Uhuru Kenyatta zitakazofanyika leo katika uwanja wa Moi Kasarani Mjini Nairobi. 
Picha na Ikulu
…………….
IMG-20171128-WA0023

0 maoni:

Chapisha Maoni