Posted by Esta Malibiche on NOV 15,2017 IN NEWS
Mgeni Rasmi-Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akizungumza wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Wadau wa Mazao ya Chakula wakati na baada ya kuvuna lililofanyika katika Ukumbi wa Nkuruma, Chuo Kikuu cha Dar es salaam. Picha Zote Na Mathias Canal
Na Mathias Canal, Dar es salaam
Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa leo Novemba 8, 2017 amefungua Kongamano la Wadau wa Mazao ya Chakula wakati na baada ya kuvuna lenye dhima ya kujadili masuala muhimu yanayohusiana na PHM na mchango wake katika uhakika wa chakula na kuchochea uanzishwaji wa viwanda nchini Tanzania kwa ajili ya kupunguza upotevu, kuimarisha usalama wa chakula na kuchochea uanzishwaji wa viwanda.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa kongamano hilo linalofanyika Katika Ukumbi wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam Naibu Waziri Mhe Mwanjelwa alisema kuwa anataraji kongamano hilo litakuwa na mjadala muhimu kujadili masuala muhimu yanayohusiana na Kuzuia Upotevu wa Mazao kabla na baada ya kuvunwa (PHM).
Alisema Serikali imeweka msisitizo wa kuweka mazingira mazuri kwa sekta binafsi na kwa Wabia wa Maendeleo kuwekeza katika eneo hilo la PHM.
“Serikali kwa kuzingatia umuhimu wa sekta binafsi itahakikisha mchakato wa kutekeleza Mkakati wa Kitaifa wa Kupunguza upotevu unakuwa shirikishi na unatekelezwa na wadau kwa ufanisi”
“Nadhani mtakubaliana na mimi kuwa hili ni tukio kubwa sana kwa Wadau wa Mpango wa kupunguza Upotevu wa Mazao baada ya Kuvunwa (PHM) nchini tangu jitihada za kushughulikia suala hili zianze na kwa sasa suala hili linaanza kueleweka kwa wadau wengi tofauti na uko nyuma ambako msisitizo ulikuwa juu ya uzalishaji na tija” Alikaririwa Mhe Mwanjelwa
Alisema, Kulingana na takwimu zilizopo bado kuna upotevu mkubwa wa mazao ya chakula ambao unafikia wastani wa asilimia 30 mpaka 40 kwa mazao ya nafaka na mikunde na kwa wastani wa asilimia 50 kwa mazao ya mboga na matunda.
Alisema ili kupunguza upotevu wa mazao ni muhimu sana na ni mkakati mzuri wa kuihakikishia nchi usalama wa chakula na lishe. Kuwepo kwa chakula cha kutosha katika Taifa na katika ngazi ya kaya ni msingi wa Taifa lenye uchumi imara, watu wenye afya nzuri na amani.
Alisema kuwa jitihada za kushughulikia UPOTEVU WA MAZAO BAADA YA KUVUNWA zilianza miaka ya 1980 baada ya kujitokeza kwa wadudu waharibifu wa mazao wajulikanao kama Dumuzi ambao walisababisha upotevu mkubwa wa mazao na kuhatarisha uhakika wa chakula nchini Tanzania.
Aliongeza kuwa Kuanzia wakati huo mabadiliko ya kisera katika sekta ya kilimo yalianza kujitokeza kupitia Serikali ya Tanzania hasa madiliko yanayolenga kupunguza upotevu wa mazao baada ya kuvunwa.
Sambamba na hayo pia alisema kuwa jitihada nyingi nchini Tanzania za kupunguza upotevu wa mazao zimefanyika zikiwemo Kujenga maghala kupitia Miradi mbalimbali, Kuanzishwa Kitengo cha Hifadhi na Usindikaji wa Mazao, chini ya Idara ya Usalama wa Chakula na jukwaa la wadau (TPMP), Kuanzishwa kwa mashirika ya kubuni teknolojia mbali mbali zinazohusiana na PHM kama vile SIDO, CAMARTEC, Kuigizwa kwa masuala ya PHM kwenye Programu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP), na Kuanzishwa kwa miradi na juhudi mbalimbali zinazohusu PHM kama vile MIVARF, GPLP, COWABAMA.
Mhe Mwanjelwa alibainisha kuwa jitihada zote hizo hazikufanikiwa vizuri kwa sababu ya kukosa mfumo mzuri wa kuratibu kazi zote PHM zilizotekelezwa na wadau mbalimbali matokeo yake kukajitokeza wadau kutekeleza kazi zinazofanana bila kujuana na maeneo mengine hayakushughulikiwa kikamilifu. Hali hii ili sababisha matumizi mabaya ya rasilima na kushindwa kuwa na mipango madhubuti ya kutekeleza shughuli za maendeleo.
Aidha, aliwataarifa kuwa maandalizi ya Mkakati wa Kuzuia Upotevu wa Taifa yako hatua za mwisho ambapo Mkakati huo utaunganisha wadau wote wanaojishughulisha na kazi za kupunguza au kuzuia upotevu wa mazao ya chakula.
“Ni Imani yangu kama mkakati huo utatekelezwa kikamilifu upotevu wa mazao utapungua kufikia wastani wa asilimia 5 nchini Tanzania” Alisisitiza Naibu Waziri Mhe Mwanjelwa.
Ksatika hatua nyingine Mhe Mwanjelwa alilipongeza jukwaa la wadau (TPMP) kwa kushirikiana vizuri na Wizara ya Kilimo, HELVETAS, Swiss Inter-cooperation-Tanzania, ANSAF na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa maandalizi ya kongamano hilo.
Wadau wa Mazao ya Chakula wakati na baada ya kuvuna wakifatilia Kongamano lililofanyika katika Ukumbi wa Nkuruma, Chuo Kikuu cha Dar es salaam
Baadhi ya washiriki wa Kongamano la wadau wa Mazao ya Chakula wakati na baada ya kuvuna wakifatilia Kongamano lililofanyika katika Ukumbi wa Nkuruma, Chuo Kikuu cha Dar es salaam
Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akisiitiza jambo wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Wadau wa Mazao ya Chakula wakati na baada ya kuvuna lililofanyika katika Ukumbi wa Nkuruma, Chuo Kikuu cha Dar es salaam
Wadau wa Mazao ya Chakula wakati na baada ya kuvuna wakimlaki Mgeni Rasmi-Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa mara baada ya kuwasili kufungua Kongamano lililofanyika katika Ukumbi wa Nkuruma, Chuo Kikuu cha Dar es salaam
Baadhi ya washiriki wa Kongamano la wadau wa Mazao ya Chakula wakati na baada ya kuvuna wakifatilia Kongamano lililofanyika katika Ukumbi wa Nkuruma, Chuo Kikuu cha Dar es salaam
Mgeni Rasmi-Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akizungumza wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Wadau wa Mazao ya Chakula wakati na baada ya kuvuna lililofanyika katika Ukumbi wa Nkuruma, Chuo Kikuu cha Dar es salaam
Washiriki wa Kongamano la wadau wa Mazao ya Chakula wakati na baada ya kuvuna wakifatilia Kongamano lililofanyika katika Ukumbi wa Nkuruma, Chuo Kikuu cha Dar es salaam
Washiriki wa Kongamano la wadau wa Mazao ya Chakula wakati na baada ya kuvuna wakifatilia Kongamano lililofanyika katika Ukumbi wa Nkuruma, Chuo Kikuu cha Dar es salaam
Mgeni Rasmi-Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akizungumza wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Wadau wa Mazao ya Chakula wakati na baada ya kuvuna lililofanyika katika Ukumbi wa Nkuruma, Chuo Kikuu cha Dar es salaam
0 maoni:
Chapisha Maoni