Posted by Esta Malibiche on JAN 25,2017 IN NEWS
Naibu waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu Anthony Peter Mavunde leo amezindua kampeni ya upandaji miti milioni moja katika kijiji cha Ibwagwa,Wilayani Kongwa Dodoma ikiwa ni muendelezo wa kampeni ya KIJANISHA DODOMA iliyozinduliwa na Mh Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan.
Mavunde amewataka wananchi wa Kongwa kuhakikisha wanatunza mazingira kwa kupanda miti mingi zaidi na kuwataka kuacha tabia ya kukata miti ambayo hali inayosababisha uharibifu wa mazingira mkubwa,Mavunde ametumia nafasi hiyo kuutaka uongozi wa Wilaya ya Kongwa kuhakikisha kwamba unasimamia utekelezaji wa sheria na kanuni mbalimbali za Mazingira ili kuinusuru wilaya hiyo na uharibifu wa Mazingira.
Akimkaribisha Mgeni Rasmi,Mkuu wa Wilaya wa Kongwa Mh Deogratious Ndejembi amemuhakikishia Naibu Waziri Mavunde kwamba kama watahakikisha miti yote iliyopandwa inastawi ili kufikia lengo la kui-KIJANISHA DODOMA na pia ameahidi kuwachukulia hatua kali za kisheria wale wote watakaobainika kuharibu mazingira hasa kwa ukataji miti na uchomaji wa misitu.
Naibu waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu,,ambae pia ni Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini kupitia Chama cha Mapinduzi Anthony Mavunde akizungumza na wananchi wa kijiji cha Ibwagwa kilichopo Wilayani Kongwa Mkoani Dodoma wakati wa uzinduzi wa kampeni ya upandaji miti leo hii.
Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mkoani Dodoma Deogratious Ndejembi akizungumza na wananchi wa kijiji cha Ibwagwa kilichopo Wilayani Kongwa Mkoani Dodoma wakati wa uzinduzi wa kampeni ya upandaji miti iliyozinduliwa leo na Naibu waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu Anthony Mavunde .
Vizuri ili Dodoma nayo istawi.
JibuFutaVizuri ili Dodoma nayo istawi.
JibuFuta