Jumatano, 31 Januari 2018

MTULIA AZIDI KUITEKA KINONDONI ,SERA ZAKE ZAWA GUMZO

Posted by Esta Malibiche on JAN 31,2018 IN SIASA

Mgombea Ubunge katika jimbo la Kinondoni kupitia tiketi ya CCM Maulid Said Mtulia akinadi sera zake jukwaani na  kuomba kura kwa wapiga kura wa Kata ya Ndugumbi.

Image may contain: one or more people, people on stage, crowd and outdoor
Mgombea Ubunge katika jimbo la Kinondoni kupitia tiketi ya CCM Maulid Said Mtulia akinadi sera zake jukwaani na  kuomba kura kwa wapiga kura wa Kata ya Ndugumbi.
Mgombea wa ubunge jimbo la Kinondoni kupitia cha cha Mapinduzi ccm Maulid Mtulia akijinadi katika kampeni leo hii alisema  kuwa aliamua kujiondoa Cuf akiwa na akili tiamamu na wala hakushawishiwa na mtu, wala hakununuliwa kama  vyama vya upinzani wanavyodai.
'Kama Mtulia angekuwa amenunuliwa asingepewa tena dhamana ya kugombea Ubunge " - Mtulia na kuongeza kuwa
"Ningekaaje kwenye chama ambacho Mwenyekiti na Katibu hawaelewani, nimejitoa ili niwe na uhuru wa kuwatumikia wana Kinondoni." - Mtulia
Alisema  kuwa alijiuzuru Cuf  ili kuwaokoa Wananchi wa jimbo la Kinondoni na si vinginevyo
"Kuhama chama ili kujiunga na chama chenye maendeleo, huo ni usaliti?" - Mtulia na kuongeza kuwa
"Nilitoa hela yake mfukoni kujenga visima vya maji; Mtulia aliyefungua kesi mahakamani kuzuia bomoa bomoa; ndio Mtulia yule aliyeomba maghorofa ya Magomeni Watu waliojitokeza nyumba zao wakae bure" - Mtulia
"Mtulia mimi ni yule yule mkinichagua nitahakikisha naendelea kuwaletea maendeleo nikishirikiana na viongozi wenzangu na Rais wangu mpendwa Di. Magufuli " - Mtulia
"Ninaomba tena ridhaa ili nihakikishe nawaletea maendeleo wana Kinondoni kutokana na kugombea kwenye chama chenye ilani ya uchaguzi iliyoshikan dola" - Mtulia
"Naomba dhamana ya kugombea ili nikashirikiane na wenzangu kutekeleza ilani ya uchaguzi ya CCM 2015 - 2020" - Mtulia
"Kazi yangu mkinichagua ni kwenda kutekeleza ilani ya uchaguzi ya CCM na si porojo wala usanii" - Mtulia
"Ukichagua Mtulia umechagua maendeleo; ukimchagua Mtulia umejenga daraja kati ya Wananchi na Serikali" - Mtulia

0 maoni:

Chapisha Maoni