Alhamisi, 25 Januari 2018

NAIBU WAZIRI MAVUNDE NA DC NDEJEMBI WAZINDUA KAMPENI YA UPANDAJI MITI MILIONI MOJA WILAYANI KONGWA

Posted by Esta Malibiche on JAN 25,2017 IN NEWS


Naibu waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu ,ambae pia ni Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Anthony Peter Mavunde  akipanda mti  katika kijiji cha  uzinduzi wa kampeni ya kupanda miti iliyozinduliwa leo hii na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Mkuu wa  wilaya ya Kongwa Deogratius Ndembeji.

Naibu waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu Anthony Peter Mavunde leo amezindua kampeni ya upandaji miti milioni moja katika kijiji cha Ibwagwa,Wilayani Kongwa Dodoma ikiwa ni muendelezo wa kampeni ya KIJANISHA DODOMA iliyozinduliwa na Mh Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan.

Mavunde amewataka wananchi wa Kongwa kuhakikisha wanatunza mazingira kwa kupanda miti mingi zaidi na kuwataka kuacha tabia ya kukata miti ambayo hali inayosababisha uharibifu wa mazingira mkubwa,Mavunde ametumia nafasi hiyo kuutaka uongozi wa Wilaya ya Kongwa kuhakikisha kwamba unasimamia utekelezaji wa sheria na kanuni mbalimbali za Mazingira ili kuinusuru wilaya hiyo na uharibifu wa Mazingira.

Akimkaribisha Mgeni Rasmi,Mkuu wa Wilaya wa Kongwa Mh Deogratious Ndejembi amemuhakikishia Naibu Waziri Mavunde kwamba kama watahakikisha miti yote iliyopandwa inastawi ili kufikia lengo la kui-KIJANISHA DODOMA na pia ameahidi kuwachukulia hatua kali za kisheria wale wote watakaobainika kuharibu mazingira hasa kwa ukataji miti na uchomaji wa misitu.

Mkuu wa Wilaya  ya Kongwa Mkoani Dodoma Deogratious Ndejembi akipanda mti
kijiji cha Ibwagwa,Wilayani Kongwa Mkoani Dodoma mara baada ya uzinduzi wa kampeni ya kupanda miti iliyozinduliwa leo hii Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Anthony Mavunde.


Naibu waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu,,ambae pia ni Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini kupitia Chama cha Mapinduzi Anthony Mavunde akizungumza na wananchi wa kijiji cha   Ibwagwa kilichopo Wilayani Kongwa Mkoani Dodoma wakati wa uzinduzi wa kampeni ya upandaji   miti leo hii.


Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mkoani Dodoma Deogratious Ndejembi  akizungumza na wananchi wa kijiji cha Ibwagwa kilichopo Wilayani Kongwa Mkoani Dodoma wakati wa uzinduzi wa kampeni ya upandaji miti iliyozinduliwa leo na Naibu waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu Anthony Mavunde .












Maoni 2 :