libicheon JAN 22,2018 IN SIASA
Na Esta Malibiche,
Iringa.
Mwenyekiti wa Uvccm Taifa Kheri James amewataka vijana wasomi Nchini kutumia Elimu waliyonayo kuisaidia Serikali katika mambo mbalimbali , siyo kusubiri yaharibike ndipo waanze koukikosoa katika Mitandao ya kijamii.
Kauli hiyo ameitoa jana wakati akizungumza katika Mkutano maaluma wa Idara ya Vyuo na vyuo vikuu Mkoani Iringa, aliwataka wasomi kutumia Elimu yao kuleta Maendeleo Nchini.
"" Wasomi tunatakiwa tuwe chachu ya maendeleo kwa kulisaidia Taifa letu.Tusisubiri mambo yaharibike ndipo tuanze kukosoa na kulalamika,bali tushirikiane na Serikali kuhamasisha maendeleo Nchini kwa Maslahi mapana ya Taifa letu. "" Alisema Kheri.
Aidha katika mkutano huo maalum,Mwenyekiti wa Uvccm Taifa alipokea wanachama wapya 400 na kuwakabidhi kadi ya chama cha Mapinduzi ,kati yao 45 wakitoka vyama vya upinzani.
Pia Mwenyekiti wa Uvccm Taifa alikabidhi kiasi cha Tsh.1 Mill. kwa viongozi wa Idara ya vyuo na vyuo vikuu Mkoa wa Iringa kwa ajili yamkutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili,n,huku akimuomba Mnec wa Mkoa wa Iringa Salim Asas aweze kuwasaidia.
Awali akisoma taarifa ya kazi za Uvccm Mkoa wa Iringa,ktika ofisi za Uvccm Mkoa,Katibu wa Umoja wa Vijana ccm Mkoa wa Iringa,James Mgego alisema wanaendelea kufanya uhakiki wa mali zote za jumuiya pamojanna na miradi yote iliyopo katika mkoa wa Iringahuku wakitekeleza agizo la Mwenyekiti wa ccm Taifa Rias John Magufuli.
"" Ndugu Mwenyekiti,Uvccm Mko wa Iringa imefanya uhakiki wa Mali zote za jumuiya ndani ya Mkoa kuanzia matawi, Kata, Wilaya na Mkoa kwa ujumla""Alisema Mgeg
umna mrali zifuatazoShamba la Igumbilo Ekari 210 leny hati namba 43_Mbylr mali ya mako makuu,Nyumba ya umoja wa vijana ambayo iko Igumbilo yenya hati na. 434_MBYLR ,Kiwanja cha Mwembetogwa chenye hati na.215029/4,ambacho ndipo mradi wa vibanda vy32 vya Uvccm Mkoa wa Iringa vilipo,Vyumba viwili v katika jengo la Ccm Mkoa,Eneo la Chuo cha Ihemi_malimya makao makuu,,Pikipiki 1,Compyuta 2,Magari2, Printer1,Terevisheni moja,King'amuzi 1Sofa set 1,Vyerehani 4, Kabati la Chuma1, Kabati la mbao1, Meza kubwa 4, ,Viti 7, Mashati ya chipukizi 50,Suruali za Chipukizi 42, pamoja na Kofia za Chipukizi 34"Alisema Mgego"
Akizungumzia hali ya kisiasa kwa vijana ndani ya mkoa wa Iringa alisema katika kuhakikisha vijana wanakuwa na kukomaa kisiasa wamejipanga ipasanpvyo kuwafikia vijana wote na kutoa masomo na semina mbalimbali zikiwemo za ujasiliamali na madarsa ya itikadi.
Mgego alisema kuwa, Mkoa wa Iringa kwa sasa hali ya kisiasa ni nzuri kutokana na utendaji mzuri wa Serikali ya awamu ya tano inayoongozaa na Rais Dakt.John Magufuli ,wanaccm na wananchi kwa ujumla wamerudisha imani kubwa kwa Serikali na Chama cha Mapinduzi.
"Kutokana na utendaji huo wa Mh.Rais wetu kipenzi cha watanzania, mkoa wetu wa Iringa madiwani na wanachama wa vyama vya upinzani wameweza kujiunga na chama cha Mapinduzi ,ambapo amdiwani watano wa kata kutoka Chadema ,walijihudhuru nafasi zao na kujiunga ca CCM pamojamna madiwani watatu wa viti maalum nao wamejiunga na ccm"" Alisema Mgego.
Kwa upande wake Katibu wa Idara ya Vyuo na Vyuo vikuu Mkoa wa Iringa,Shabath Kapingaakisoma Risala ya Idara ya Vyuo na Vyuo vikuu alisema idara ya vyuo ina matawi matatu ya vyuo vikuu ambayo ni Chuo kikuu Mkwawa,Chuo kikuu Ruah na Chuo kikuu Iringa pia kuna matawi ambayo yamefunguliwa katika Chuo cha ualimu Kleruu.
Kapinga alisema katika kuhakikisha ustawi wa chama ndani ya vyuo na vyuo vikuu unaendelea na k(wa kitovu cha siasa borazenye tija kwa manufaa ya chama na Uvccm wanaendelea kuhakikisha wanafunzi wanapata mafunzo ya itikadi ambapo mwaka 2017 katibu wa Halmashauri kuu ya Taifa uhusiano wa kitaifa Canal Lubinga alitoa mafunzo ambayo yamekuwa na matokeo chanya kwa mwaka wa uchaguzi 2017.,hivyo Serikali zote za wanafunzi zinaongozwa na vijana wa chama cha Mapinduzi .
"Pamoja na mafanikio hayo,tunchangamoto ya ukosefu wa ofisi kwenye matawi ,Uhaba wa fedha za kuweza kutembela matawi ya mbali ya vyuo ya wilaya za nje ya Iringa mjini na kutoa hamasa"" Alisema Kapingu
Katibu wa Chama cha Malpinduzi CCM Mkoa wa Iringa,Christopher Magala akizungumza na Uvccm wanaosoma katika vyuo mbalimbali mkoani Iringa jana.
Mnec Mkoa wa Iringa Salim Asas akizungumza na Uvccm wanaosoma katika vyuo mbalimbali mkoani Iringa jana
Katibu wa Idara ya Vyuo na vyuo vikuuu Mkoa wa Iringa Shabath Kapingu akisoma Risala ya Idara ya Vyuo na Vyuo vikuu mkoa wa Iringa kwa Mwenyekiti wa Uvccm Taifa Kheri James.
0 maoni:
Chapisha Maoni