Jumamosi, 20 Januari 2018

MGOMBEA UBUNGE JIMBO LA KINONDONI KUPITIA CHAMA CHA MAPINDUZI CCM AREJESHA FOMU KWA KISHINDO

Posted by Ssta Malibiche on JAN 20,2017 IN SIASA

Viongozi wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Dar na Wilaya ya Kinondoni,makanda wakiongozwa na Mnec wa Mkoa wa Dar  es slaam Yusuph Nassoro wakimsindikiza Mgombea wa Ubunge jimbo la kinondoni kupitia Chama cha Mapinduzi Said Mtulia kurudisha fomu ya uteuzi kwa ajili ya kuwania ubunge jimbo la Kinondoni.
MGOMBEA  ubunge  Jimbo la kinondoni owa  tiketi  ya Chama cha Mapinduzi CCM,SAid Maulid Mtulia mapema leo hii amerudisha fomu   ya uteuzi kuwania Ubunge jumbo la Kinondoni.

Mgombea huyo alisindikizwa   na viongozi mbalimbali wa chama ngazi ya Mkoa wa Dar es salaam na Wilaya pamoja na makada  wa chama cha mapinduziwwkiongozwa na Mnec wa Mkoa  wa Dar es  salaam Yusuph Nassoro.

Akizungumza mara baada ya kukabidhi fomu hiyo,aliwataka wanakinondoni  kumpa kura zote za ndiyo ili aweze kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili.

 Mtulia alisema  anasubiri kuapishwa kuwa mbunge wa jimbo hilo kutokana na mgombea aliyepitishwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kuwa mwepesi kwake.

Mgombea wa ubunge jimbo la kinondoni kupitia chama cha Mapinduzi CCM,Said Mtulia  akisaini fomu  katika ofisi za wilaya hiyo mapema leo hii . 





Mgombea wa ubunge  jimbo la Kinondoni kupitia chama cha Mapinduzi CCM Said Mtulia akisindikizwa na  viongozi wa CCM,makada  pamoja na Mnec wa Mkoa wa Dar  es salaam Yusuph Nassoro.













0 maoni:

Chapisha Maoni