Ijumaa, 19 Januari 2018

MKUU WA WILAYA YA MBULU CHELESTINO MOFUGA AIPONGEZA SHULE YA SEKONDARI YA JUMUIYA YA CHIEF SARWAT

Posted by Esta Malibiche on JAN 19,2018 IN NEWS



MKUU wa Wilaya ya Mbulu Chelestino Mofuga amewataka  walimu kuzingatia maadili ya utumishi na taaluma yao kwa kuchapa kazi ili shule iwe ya mfano Katika wilaya.

Kauli hiyo ameitoa Mapema leo hii wakati akizungumza na walimu, wanafunzi na bodi ya shule   ya jumuiya ya   Chief  Sarwat   na kusema kuwa serikali imetoa fedha kiasi cha Mill. 215 kwa ajili kujenga madarasa yatakayotumika kuanzisha kidato cha tano,mabweni na vyoo.

Wakati huo huo Mkuu wa wilaya aliwapongeza walimu wa   jumuiya ya shule ya Chief  Sarwat  kwa  Matokeo Mzuri ya mtihani wa  kidato cha pili kwa kufahuru wanafunzi kwa %95.

""Hatua hii imenifurahisha sana kwani tumevuka malengo tuliyojiwekea kwa pamoja"" alisema Mofuga""

Ongezeko la Ufahuru huo umetokana na Mkuu wa wilaya hiyo kuitisha kikao mwaka 2017 cha wakuu wa shule za Sekondari na kupanga mikakati ya kufundisha  kwa bidii ili wanafunzi waweze kufahuru,ambapo walipanga kufikia %80  na hatimae wamefikia %95.
Aidha Mkuu wa wilaya alikula chakula cha mchana na wanafunzi wa shule hiyo    kwa kuwapongeza  walimu kwa kufaulisha wanafunzi wa kidato cha pili Katika mitihani ya Taifa mwaka 2017, Kwa asilimia 95.







0 maoni:

Chapisha Maoni