Jumamosi, 6 Januari 2018

MKUU WA MKOA WA LINDI GODFREY ZAMBI AZINDUA KAMPENI YA UPANDAJI MICHE BORA YA KOROSHO

Posted by Esta Malibiche on JAN.6,2017 IN NEWS

 Mkuu wa Mkoa wa Lindi Godfrey Zambi akipanda Mche wa Korosho katika Shamba la Magereza lililopo eneo la ChemChem Wilayani Nachingwea,mara baada ya uzinduzi wa Kampeni ya upandaji Miche bora ya Korosho.PICHA NA ESTA MALIBICHE.

Mkuu wa mkoa wa Lindi Godfrey Zambi leo hii  amezindua  kampeni ya upandaji Miche bora ya korosho.
Uzinduzi huo umefanyika katika eneo la Chemchem wilayani Nachingwea katika mkoa wa Lindi ,ambalpo uzinduzi huo uliambatana na upandaji wa miche katika shamba la Magereza, zaidi ya miche 104  imekabidhiwa kwa wakulima   kwa ajili ya kupanda.

Viongozi mbalimbali wameshiriki katika uzinduzi huo  akiwemo Mkurugenzi wa Bodi ya Korosho Tanzania Hasaan Jarufu, Mwenyekiti wa bodi ya Korosho Mama Anna Abdalah,Makamu Mwenyekiti Edgar Maokola Majogo,Wakuu wa wilaya,wakuu wa Idara mbalimbali , viongozi wa Dini,Vyama vya Siasa na wananchi kutoka mkoa wa Lindi na nje ya Mkoa huo.

Mkuu wa Mkoa wa Lindi Godfrey Zambi akipanda Mche wa Korosho katika Shamba la Magereza lililopo eneo la ChemChem Wilayani Nachingwea,mara baada ya uzinduzi wa Kampeni ya upandaji Miche bora ya Korosho.PICHA NA ESTA MALIBICHE.

Mwenyekiti wa Bodi ya Korosho Anna Abdalah akipanda Mche wa Korosho.

Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Korosho Tanzania  Edgar Maokola Majogo akipanda Mche wa Korosho

Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea  Rukia Muwango akipanda Mche wa Korosho

Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea  Rukia Muwango akipanda Mche wa Korosho
Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa Joseph Mkilikite akipanda Mche wa Korosho

0 maoni:

Chapisha Maoni