Alhamisi, 18 Januari 2018

MINAKI NA PUGU WAJIPANGA KWA MATOKEO MAZURI YA KIDATO CHA SITA MWAKA HUU 2018

Posted by Esta Malibiche on JAN 18,2017 IN  NEWS

 Wanafunzi wa shule ya sekondari Mibnaki wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo.
 Baadhi ya walimu na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Minaki wakiwa pamoja na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo alipotembelea shuleni hapo.
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akiwa na walimu wa Shule ya sekondari Pugu alipotembelea kukagua maendeleo ya ukarabati wa miundombinu shuleni hapo.
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akiwa na viongozi wa wilaya ya Kisarawe wakipata maelezo kutoka kwa Meneja wa Wakala wa Majengo nchini(TBA) wanaofanya ukarabati wa sekondari ya Minaki.
Miundombinu ya shule ya sekondari Minaki ikiendelea kujengwa.
 ............................................................................
Wanafunzi wa sekondari ya Minaki na Pugu wameahidi kufanya vizuri katika mitihani yao ya kidato cha sita mwaka huu kutokana na kusomea kwenye mazingira rafiki.

Kauli hiyo wameitoa kwa nyakati tofauti leo walipotembelewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tamisemi Selemani Jafo alipokuwa akikagua maendeleo ya ukarabati wa shule hizo.

Katika Shule ya sekondari Pugu imefanyiwa ukarabati mkubwa katika vyumba vya madarasa, mabweni, vyoo, jengo la utawala, maabara, pamoja na mifumo ya maji na umeme.

Aidha kwa upande wa shule ya sekondari Minaki ukarabati wake kama ilivyo kwa shule ya Pugu na wanatarajiwa kukamilisha kabla ya mwezi Mei 2018.

Kutokana na ukarabati, Wanafunzi wa shule hizo wamemuahidi Waziri Jafo kwamba serikali itarajie matokeo mazuri katika shule zao.


Zoezi la kuboresha shule kongwe hapa nchini limepokelewa vyema na jamii, wanafunzi pamoja na walimu kwa kuwa lina manufaa mapana kwa maslahi ya elimu ya Tanzania.

0 maoni:

Chapisha Maoni