Jumatano, 24 Januari 2018

RIDHIWANI KIKWETE:MIGOGORO YA ARDHI NI MOJA YA CHANGAMOTO KUBWA INAYOTUKABILI WANACHALINZE

Posted by Esta Malibiche on JAN 25.218 IN NEWS


Mbunge wa Jimbo la Chalinze kupitia tiketi ya Chama cha Mapinduzi CCM Ridhiwani Kikwete amefanya ziara   katika kijiji cha Kwamduma, Kata ya Kibindu ikiwa na lengo la kuangalia Athari za Migogoro Baina ya Kijiji na Hifadhi ya Uzigua.

Ridhiwani alisema Migogoro ya Ardhi ni moja ya Changamoto kubwa inayotukabili wana chalinze,hivyo inatakiwa intatuliwe kwa wakati.

 "Tumeona hitaji la kukaa chini na watu wa hifadhi na kujadili suala la Mipaka inayotembea" Alisema Ridhiwani na kuongeza kuwa

"Tumekubaliana na Serikali kuingilia hili jambo mara moja. Serikali imekubali kulishughulikia ndani ya kipindi kifupi." Alisema Ridhiwani
#kazi zinazoacha Alama #chalinzenikazitu #ccmnikazitu #magufulinikazitu #kwamdumanikazitu #kibindunikazitu







0 maoni:

Chapisha Maoni