Jumatano, 31 Januari 2018

ROTARY CLUB OF IRINGA YAPANDA MITI 134 YA MATUNDA KATIKA SHULE YA SEKONDARI YA WASICHANA IRINGA

Posted by Esta Malibiche on JAN 31,2018 IN NEWS

Rais wa Rotary Club of Iringa Miraji Vanginothi akiongoza zoezi la upandaji miti katika shule ya wasicahna ya Iringa (Iringa Girls) liliandaliwa na Kikundi cha Rotary Club tawi la Iringa kazi hiyo ikishirikisha wanafunzi wa kidato  cha tano na sita na uongozi wa shule siku ya jumamosi, ambapo zaidi ya miti ya matunda 134 ilipandwa. (Picha na Friday Simbaya)
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya wasicahna ya Iringa (Iringa Girls) wakishiriki zoezi la upandaji miti katika shule hiyo liliandaliwa na Kikundi cha Rotary Club tawi la Iringa kazi hiyo ikishirikisha wanafunzi wa kidato  cha tano na sita na uongozi wa shule siku ya jumamosi. (Picha na Friday Simbaya)


Rotary Club of Iringa imepanda miti ya matunda zaidi ya 134 katika ya wasichana ya iringa (Iringa Girls Secondary School) ikiwa mkakati kabambe wakupanda miti katika shule mbalimbali mkoani hapa. 

Zoezi la upandaji miti katika shule hiyo iliongozwa na rais wa rotary club of iringa Miraji Vanginothi kwa kushirikiana na MKUU wa Wilaya Iringa Richard Kasesela. 

MKUU wa Wilaya Iringa Richard Kasesela amesema kama watu watajenga utamaduni wa kuwaangalia na kuwasaidia watu wengine wataishi kwa furaha katika maisha yao. 

Kasesela ametoa kauli hiyo jana wakati alipokuwa akizungumza kwenye hafla ya upandaji miti katika shule ya Sekondari ya wasichana ya Iringa (Iringa Girls). 

Zoezi la upandaji miti katika shule hiyo liliandaliwa na Kikundi cha Rotary Club tawi la Iringa kazi hiyo ikishirikisha wanafunzi wa kidato cha tano nasita na uongozi wa shule. 

"Ngoja niseme mambo mawili,kwanza ukiwa Rotarian ni kumuungalia mwenzako,hilo ndo jambo la Msingi,ni jumuiya ya kimatifa na kikibwa ni kujitolea"alisema Kasesela. 

Kasesela aliwataka wanafunzi wa shule hiyo pamoja na vijana kujenga utamaduni wa kufanya jambo kwa lengo la kusaidia wengine na kwamba kwa kufanya hivyo watakuwa wamejijengea uwezo wa kutenda mema. 

"Hata leo tunapanda miti ,hii miti si kw aajili yetu ni kw aajili ya watu wengine,ndio sababu mi mara nyingi ninasema nivema kila unalofanya ufanye kwa ajili ya mwingine: 

:Umezaliwa na mtu mwingine,umepokelewa na mtu mwingine,utalelewa na mtu mwingine,utaolewa na mtu mwingine na utazikwa na mtu mwingine hivyo kila mtu akifanya kwa ajili ya mtu mwingine nchi yetu na dunia kwa ujumla itabaki kuwa na amani"alisema. 

Awali akizungumza katika zoezi hilo Rais wa Rotary Club Tawi la Iringa Miraji Vanginothi aliwashukuru watu waliojitolkea kupanda naa miti katika eneo la shule hiyo na kuutaka uongozi w ashule na wanafunzi kuitunza kwa faida yao na kizazi kijacho. 

"Tumepanda miti jukumu lenu ni kuhakikisha mnaitunza kwa aajili ya kizazi kijacho,miti niu kwa ajili ya kutunza mazingira miti ni kw aajili ya maatunda"alisema Vanginothi. 

Kwa upande wake Mkuu wa shule ya hiyo Blandina Nkondola alishukuru Rotary Club tawi la Iringa kwa uamuzi w akupanda miti katika shule hiyo na kuahidi kuitunza. 

"Tunawashukuru sana kwa msaada wenu wa kijamii,tumefurahishwa na uamzui wenu wa kizalenda wwenye lengo al kutunz amazingira yetu na tuwahakikishei tu kwua tutaitunza hii miti"alisema,Nkondola.

0 maoni:

Chapisha Maoni