Alhamisi, 11 Januari 2018

CHADEMA JIMBONI KWA PETER MSIGWA YASAMBARATIKA DIWANI OSCAR KAFUKA ANG'ATUKA

Posted by Esta Malibiche on JAN 12,2017 IN SIASA

Diwani wa kata ya Mkwawa  Manispaa ya Iringa, kupitia chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Oscar Kafuka akizungumza na vyombo vya Habari  jana  usiku

Diwani wa kata ya Mkwawa Manispaa ya Iringa,kupitia  Chadema Oscar Kafuka amejiuzulu nafasi zake zote ikiwemo  ya udiwani kupitia chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA
Akizungumza na vyombo vya Habari hapo jana jioni...alisema ameamua kuachana na siasa ili aweze kuitumikia familia yake ,huku akidai kuwa muda mwingi alikuwa anautumia katika Siasa hivyo kushindwa kumudu malezi ya familia yake.

"Nimeamua kwa moyo wangu wa dhati bila kushinikizwa na mtu yeyote kujivua udiwani  kuanzia leo na hatimae kuitumikia familia yangu"" AlisemaKafuka.
Diwani wa kata ya Mkwawa  Manispaa ya Iringa, kupitia chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Oscar Kafuka akizungumza na vyombo vya Habari  jana  usiku   




0 maoni:

Chapisha Maoni